TFF: Bei ya VAR ni Sh Bilioni 14.5, kamera ziwe 38, kila mechi timu zinalipia Sh milioni 7

Lupweko amekariri standard za FIFA halafu hajui ukomo wa standards za FIFA zinahusika katika ngazi zipi. Standard za FIFA zinafanya kazi kwa ngazi za kimataifa pekee.

Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia amezungumzia matumizi ya VAR wakati wa kufunga semina ya siku tatu ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya NBC iliyomalizika jana Februari 17, 2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Haya hapa ndiyo aliyoyasema Karia: “Unajua gharama za VAR? Sawa najua Serikali wanaliangaia hilo.

“Ili kupata ile VAR seti nzima ni karibu Sh bilioni 14.5, mbali ya kamera za Azam TV, VAR nao wanatakiwa kuwa na kamera zao kuanzia 33 hadi 38.

“Na tukiamua kuweka lazima tupate kibali kutoka kwao kwa kuwa siyo mali yetu, pia kila mechi klabu zinatakiwa kushea gharama ya kutumia hiyo VAR ambayo ni kama Sh milioni 7 hivi.”

Hatua hiyo inakuja kutokana na presha kubwa ambayo imekuwa ikiendelea hivi karibuni kutokana na waamuzi kadhaa wa soka kufanya makosa katika Ligi Kuu Bara msimu huu unaoendelea wa 2021/22.

Karia akaongeza kwa kusema: “Kuna mambo mengi yanazungumzwa, mengine kwa wadau kutojua sheria na mengine nayafanya makosa kweli.

“Mnafanya makosa nyie lawama zinakuja kwangu, sijawahi kutoa maelekezo kwa waamuzi hata mara moja.”


Kwa mashindano ya ndani kinachoangaliwa ni namna ya kufuata zile sheria za FIFA, kama ingekuwa kunakufuata standards za FIFA basi tungeona FIFA wanaingilia kati juu ya viwanja vyetu vibovu tunavyotumia kwenye ligi yet
 
Azam mvua ikinyesha inakuaje
 
Kwanza wakarabati viwanja kwa hizo pesa, hizi kelele za VAR ni mihemko tu ya Mwigulu na timu yake utopolo, siku utopolo nao wakifaidika na maamuzi ya refa kelele zao zote za VAR zitakwisha, nasisitiza hiyo pesa kwanza ikaboresha viwanja (pitch).
 
Bila shaka TFF wameona ushauri wako tusubiri utekelezaji
 
Karia anachanganya mambo makusudi, makosa ya marefa tunayaona kupitia replay za Azam tv. Siyo kosa replay tunazo ziona sisi na wao marefa wawekewe pale uwanjani walau kwa kuanzia. Implementation ya VAR hata huko Ulaya inatofautiana kwa baadhi ya nchi.
 
Ni kweli mkuu
 
V.A.R (Video assistance Refaree) kwani hizo replays za Azam nazo si ni Video? Au mpaka kutumia kamera za wazungu ndo zitaitwa Video
 
Uweke VAR kwenye viwanja kama madimbwi ya Samaki hebu tuwe serious kidogo.

Billion 14 itahudumia viwaja vingapi kuweka nyasi bandia na taa za usiku ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…