Lyrics Master
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 479
- 670
Kuna swali najiuliza, hivi team ikisajili mchezaji na kabla ya deadline huyo mchezaji huyu akawa mgonjwa, inamaana hairuhusiwi tena kusajili mchezaji mwingine kabla ya hiyo deadline?
Kama ni ndio basi kuna mahala kanuni zetu hazipo vizuri.
Sipo hapa kusema nani yupo sahihi nan ani hayupo sahihi ila kwa namna hii team ya Yanga ninaweza kuipongeza kwa kuibua mapungufu katika kanuni zetu. Kwanini?
Haiwezekani mchezaji amesajiliwa katika muda sahihi na kufuata taratibu zote halafu iwepo kanuni ya kumzuia mchezaji huyo. Hiyo kanuni itakuwa na mapungufu makubwa sana au itakuwa imewekwa kimtego kwajili ya ‘’watu flani’’ na kwa bahati mbaya watu hao wameingia kwenye kumi na nane za ‘’watawala’’ ambao kwa siku za hivi karibuni wanasema wanaongoza kwa mawazo yao na si kanuni. Kanuni hutumika tu pale “unapoonekana kushindana na mamlaka.”
Kwanini?
Ni vile tu tumekuwa wasahaulifu sana hasa hawa ndugu wa TFF wamekuwa wasahaulifu mno kupindukia,
Mwaka jana 2021, katika usajili wa dirisha dogo, SIMBA SC ilimsajili Perfect Chikwende na kufanya idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia wachezaji 13. Kilichofanyika Francis Kahata akatolewa kwenye usajili wa ligi ya ndani halafu Perfect Chikwende jina lake likaingizwa. Francis Kahata akasajiliwa kwenye mashindano ya kimataifa tu. Kitu ambacho this time around Yanga wamefanya hivyo hivyo.
Lakini wakati huo hatukusikia TFF ikikataa usajili huo.
Wachambuzi wenye ‘mbambamba’ nyingi kama akina Juma Ayo, Jemedari Said na Wilsom Oruma hatukuwasikia pia katika uchambuzi wa kujifanya wanajua kutetea sheria kama wanavyotetea sasa.
Hivyo hapa inaonekana kuna ‘ajenda’ ya siri kama ‘mungu mtu wa mpira’ alivyosema ukishindana na mamlaka wewe ndio utakaye umia. Ni wazi kuna watu wameanza kupata maumivu kwasasabu sheria ileile inayoibana team B sasa haikumbana team A.
Swali la msingi ni kujiuliza tu hizi sheria ni kwa team zote au kwajili ya team flani flani?