Mwaka huo kanuni zilikuwa zinaruhusu wachezaji 12 CAF na wachezaji 10 wa ligi ya Bara, kwa hiyo ukipeleka majina ya wachezaji 12 TFF inabidi useme nani akatwe. Kanuni za mwaka huu zimebadilika kwa upande wa TFF, na zimeruhusu kusajili wachezaji 12 sawa na wa CAF. Sasa ukipeleka majina 13, huyo aliyezidi atacheza ligi gani? Na kama haujasema nani akatwe, si anakatwa wa mwisho? Au ulitaka TFF ichague yeyote ili Tuisila aingizwe, je TFF ingemchagua Mayele, si mngeenda hadi kwa Mama Samia? Kwa nini msikate wenyewe