Kama ni kweli basi TFF wanatupeleka pabaya. Taarifa za awali ni kwamba Yanga walipeleka jina la Kisinda TFF toka August 30. Siku hizi mambo ni rahisi sana hata saa moja tu inatosha kukamilisha uhamisho na usajili wa mchezaji.
Hakuna namna unaweza kuustawisha mpira wa Tanzania huku ukiyakanyaga maslahi ya Yanga au Simba, vinginevyo na wao wataihujumu tu TFF.
Kwa wale ambao mlishawahi kuongoza taasisi mnajua, wakati mwingine unalazimika kushirikiana na hasimu au taasisi usiyo ipenda kwa sababu tu sheria na taratibu zinakutaka ufanye hivyo. Maadam Club anayo toka mchezaji walimruhusu kuondoka Club kubwa kama Yanga sidhano kama walishindwa kukidhi masharti ya usajili.
TFF wawe wanafanya mambo kama watu wazima na wasomi, visasi viiishie kuwa kati ya mtu na mtu siyo taasisi na taasisi kwa sababu siamini kama TFF wataiweza Yanga.