ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,553
Japo wengi watabisha lakini ukweli utasimama,yaonyesha wazi uwanja wa taifa/Mkapa Stadium umeharibiwa kwa nguvu za giza hasa goli la kusini mwa uwanja na hujuma hii ni wazi imefanywa na moja ya klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini.
Ushahidi umeonekana mechi ya leo kati ya Yanga na Zalan,wachezaji wa yanga karibu wote wamekosa magoli ya wazi kabisa ambayo wote tumeshangaa na hata wachezaji husika wote walibaki midomo wazi!
Mwanzoni tuliwalaumu wachezaji..lkn baada ya mapumziko hali ikabadilika wachezaji wale wale wakaanza kuporomosha mvua ya magoli upande wa goli la kaskazini,na katika hali ya kushangaza straika wa Zalan naye akiwa yeye na kipa Msheli mpira wake uliokua ukielekea golini ukakosa muelekeo na kugonga bomba na kurudi uwanjani kama ilivyomtokea Aziz k kipindi cha kwanza,goli lile lile na angle ile ile..
Tuombe uongozi wa shirikisho wawasiliane na mtumishi Mwamposa afike pale uwanjani katika siku mbili hizi ili kuondoa janga hili na kulinda hadhi ya mashindano,atakase uwanja mzima na magoli na hasa upande wa goli la kusini hilo limeathirika sana pale amwage mafuta mengi ya upako,
Nawasilisha.
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app