NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Sasa nimegundua ni kwa nini marefa wetu hawaitwi kuchezesha mechi za kimataifa.
Kuanzia mechi ya Azam FC dhidi ya Dodoma waamuzi waliochezesha ile mechi ni utumbo mtupu tena Azam FC wananyimwa goli sijui TFF na Bodi ya ligi mnaawaadhibu vipi hao marefa.
Tazama mechi ya Singida Fountain Gate FC dhidi ya Simba SC Kuna makosa mengi sana yaliyofanywa na waamuzi mpaka unajiuliza hivi hawa marefa huwa wanajifunza sheria kweli?
Ukifuatilia mpira kwa makini unagundua kuwa refalii wapo kwa ajili ya kuzilinda Simba na Yanga tu maana wao Wana mashabiki ambapo watakapo ona wanazulumiwa ni lazima wapige kelele kwenye mitandao.
Kwa uchezeshaji huu ni ngumu sana kwa marefa kuitwa katika mechi za kimataifa na ukizingatia ligi yetu inakua kila siku inaongeza wafatiliaji na mashabiki wapya kutoka nchi za jirani na kimataifa pia.
TFF na Bodi ya ligi Kama mtaendelea kukaa kimya juu ya huu utumbo Basi ni wazi mnaitia doa ligi yetu na wapenzi wa mpira tutaamini kuwa nyinyi ndiyo mnabariki haya Madudu yanayofanywa na marefa.