TFF na Bodi ya Ligi wapo kimkakati zaidi katika upangaji wa ratiba

TFF na Bodi ya Ligi wapo kimkakati zaidi katika upangaji wa ratiba

Mzee hujasoma ukaelewa au inawezekana hujafuatilia msimamo wa ligi. Simba huwa yupo nyuma kwa idadi ya mechi tokea mwaka jana kabla hata ya AFCON. Lakini pamoja na hilo bado Yanga anapangiwa ratiba ya idadi sawa za mechi na Simba. Na bado Azam nae wanamuendelezea kucheza mechi.
Kama tangia msimu unaanza simba yupo nyuma mechi moja, basi acha Yanga acheze kesho ili aendelee kuwa na mechi moja mbeleya simba.

Unataka Azam wasimuendelezee mechi wakati hana ratiba za kimataifa.
 
Hapo kwenye ratiba kuna namna na sio bure, kwa nini kwenye mechi za hivi vilabu lazima Yanga ndio atangulie kucheza mechi moja mbele ndipo Simba atafuata.

Msimu huu piga ua huwezi kukuta Simba anaitangulia Yanga kucheza mechi za ligi, ni kwa nini..? Ili Simba wajipange wakishajua matokeo ya mwenzie.🥸🥸
 
Huu mkakati upo kwaajili ya Simba, na anayekandamizwa zaidi anajulikana ni Azam. Niliwahi kuhoji kwenye huu uzi
Kwanza kwenye post yako hujaonesha malalamiko yeyote kwamba Azam ndio anayekandamizwa.

Pili kwenye post yako hujaonesha malalamiko yeyote kwamba kufuatia kiporo cha Yanga ni indication za kuonesha Yanga inabebwa na TFF.

Tatu ni post ambayo haijawa Quoted na mtu na wala wewe sio muanzisha thread, ipo asilimia kubwa ya wewe kuifanyia editing (japo kuna loose end) ili uitumie kama references.
 
Wewe ni balozi wa Simba humu JF hujawahi kusimama katika umbo la uanamichezo zaidi ya kusimama katika ushabiki wa timu. Sikushangai.
Hata swala la kila mwaka kulalamika sisi sikupingi ni kweli ni sisi ndio tunaolalamika kila mwaka na malalamiko yetu sio hilo tu bali yapo mengi ikiwemo GSM kununua wachezaji wa timu pinzani ili wacheze chini ya kiwango, bahasha kwa marefa, timu kutumia uchawi, na GSM kudhamini timu nyingi za ligi kuu. Hivyo ni kawaida yetu kulalamika.
Kila mwaka nyie ndio mna malalamiko ya TFF na Karia

Si mwaka jana hapo mlisema hamuwezi kuchukua ubingwa ikiwa Karia ataendelea kuwa Raisi wa TFF kwasababu anachuki na Yanga?

Lakini ubingwa mlibeba

Na huyo huyo Karia na TFF ndio walioinhia mkataba na GSM wa kudhamini ligi wakitaka watu wasihoji.

We ulitaka lipokelewe hilo jambo kirahisi?

Na ndio maana udhamini ule haukufika mbali ukatibuka. Tunatoa malalamiko pale tunapokuwa na reason sio pale tunapojiskia kupayuka
 
Back
Top Bottom