TFF na Bodi ya Ligi wapo kimkakati zaidi katika upangaji wa ratiba

Kama tangia msimu unaanza simba yupo nyuma mechi moja, basi acha Yanga acheze kesho ili aendelee kuwa na mechi moja mbeleya simba.

Unataka Azam wasimuendelezee mechi wakati hana ratiba za kimataifa.
 
Hapo kwenye ratiba kuna namna na sio bure, kwa nini kwenye mechi za hivi vilabu lazima Yanga ndio atangulie kucheza mechi moja mbele ndipo Simba atafuata.

Msimu huu piga ua huwezi kukuta Simba anaitangulia Yanga kucheza mechi za ligi, ni kwa nini..? Ili Simba wajipange wakishajua matokeo ya mwenzie.🥸🥸
 
Kwanza kwenye post yako hujaonesha malalamiko yeyote kwamba Azam ndio anayekandamizwa.

Pili kwenye post yako hujaonesha malalamiko yeyote kwamba kufuatia kiporo cha Yanga ni indication za kuonesha Yanga inabebwa na TFF.

Tatu ni post ambayo haijawa Quoted na mtu na wala wewe sio muanzisha thread, ipo asilimia kubwa ya wewe kuifanyia editing (japo kuna loose end) ili uitumie kama references.
 
Kila mwaka nyie ndio mna malalamiko ya TFF na Karia

Si mwaka jana hapo mlisema hamuwezi kuchukua ubingwa ikiwa Karia ataendelea kuwa Raisi wa TFF kwasababu anachuki na Yanga?

Lakini ubingwa mlibeba

Na huyo huyo Karia na TFF ndio walioinhia mkataba na GSM wa kudhamini ligi wakitaka watu wasihoji.

We ulitaka lipokelewe hilo jambo kirahisi?

Na ndio maana udhamini ule haukufika mbali ukatibuka. Tunatoa malalamiko pale tunapokuwa na reason sio pale tunapojiskia kupayuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…