TFF na NBC hazijawatendea haki wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania

Unafikiri wanaposema wanajadiliana, huwa wanajadiliana kuhusu maswala yapi?

Bid ikiwekwa mezani, anayetafuta biashara ni yule anayebid...

Highest bidder anawin tender...TFF hakuwa akitafuta business partner bali alikuwa akitafuta mnunuzi wa bidhaa yake ambayo ni ligi ya TZ
 
Mwenyewe natofautiana na TFF mambo mengi ila kwa hili nawapongeza sana, maana tunaelewa hali na mazingira yalivyo magumu kwenye biashara awamu hizi 2, kupata mdhamin wa kutoa 2.5 B per year si jambo la kitoto!
 
Habarini Za Wakati kama Huu…

Vilabu vyetu vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara huwa vinahangaika sana Kwenye kuhakikisha Ligi Yetu Inakuwa Bora na Yenye kusisimua, Haya huonekana Wakati wa Usajiri na wakati wa Maandalizi ya Msimu Mpya. Wamekuwa Wakihangaika Sana kutafuta wadhamini na Wadau mbalimbali kuhakikisha Timu inakuwa imara na yenye ushindani Lengo likiwa ni Kuifanya ligi yetu kuwa bora.

Kupitia Haya Vilabu vimefanikiwa sasa ligi Yetu inashika Nafasi ya 8 afrika kwa Ubora.

Je TFF wanafanya nini Kuhakikisha kuwa Ligi yetu inazidi kuwa Bora, kubwa na yenye kuvutia? Ni kuendelea kutafuta wadhamini.

Lakini Najiuliza ni KWANINI TFF imekubali Udhamini Wa Tsh 2.5 Billioni Tuuuu… Kwa Level ya Ligi yetu ilipofikia, Kumpokea mdhamini wa 2.5 Billioni Ni Kuidharirisha Ligi yetu na Kuto itakaia Mema.

Niwe Muwazi Nilipo anza kusikia Tetesi kuwa NBC anaenda Kuwa Mdhamini nilijua Tuu hapa hamna Pesa Ni Porojo. Haiwezekani Mdhamini wa Ligi kwa Miaka 3 akaweza 2.5 Billioni kwa Vilabu Karibia 16 huku ni kurudisha Nyuma Ligi yetu na Kutokuitakia Mema Ligi Yetu.

Kiukweli TFF mnahusika Kwa Asilimia 100 kuihujumu Ligi Yetu. 2.5 Billioni Kumbe hata Vunja Bei, Clouds, Wasafi na Wengine wangeweza kuweka Hilo dau na Zaidi.

Swali Ni je TFF mlikosa Mdhamini wa zaidi ya 2.5 Billioni? Au vigezo vyenu ni vipi katika hili? Mnafikiria hali halisi ya Tanzania na vilabu vyake na Ligi ilipofikia? Mbona Azam Aliweka Pesa ndefu kila mtu akanyanyua mikono juu?

Ifike pahala sasa TFF uchaguzi wake uwe unafanywa na vilabu na wadau wa soka ili tupate viongozi wenye akili wanaoweza Kuifikisha ligi yetu pahala fulani.

Kama Ligi Ina Mdhamini wa 2.5 Billioni unategema Kuna Club itakuja kutoka na kusajiri Mchezaji wa Zaidi ya 2.5 Billioni au hata Wa 1 Billioni?

TFF na NBC mmetupiga na kitu Kizito Kichwani wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania.

Karia OUT
Hivi hebu nieleweshen kipimo cha ubora wa ligi yetu ni club kutumia pesa nyingi kusajili au vilabu vyetu kufanya vizuri mashindano ya nje..

Maana swala la vilabu kutumia fedha nyingi.. Halipandishi hadhi ya ligi

Tukija kwenye Vilabu vyetu na mashindano ya nje... Ni Simba tu walau wamefika robo fainali ndan ya miaka 5...

Sasa unataka mdhamin aweke pesa ndefu kwa kigezo kipi ikiwa .. Huna viwanja vya mpira vya maana... Club zenu hazina structure ya kueleweka... mashindano nje ndio hivyo homa za vipindi

Bado mnataka mdhaminiwe kwa bilion 100.. Wakat uwanjan mashabiki hadi mechi kubwa
Ndo viwanja vijae...

Tatizo mnapima ligi kwa kuangalia Simba, Yanga na Azam.. Tunaweza tukawa namba nane kwa ubora sababu tuko kwenye kundi la wasiojiweza... Kwenye kundi la vipofu akiwepo mwenye chongo yeye ndo atakuwa kawazid wenzie ... Ila haimanishi kwamba yuko kamili

Nenden na uhalisia wenu... Ingekuwa ligi yetu ni bora kihivyo achilia mbali udhamin wa ligi ila vilabu vyote vingekuwa na wadhamin kwa pesa ya maana... Automaticaly mdhamin wa ligi angetoa peaa ndefu
 
Zawadi ya mshindi wa kwanza haifikii hata bajeti ya hizi timu kongwe ktk uendeshaji kwa msimu mzima

Tatizo ndio linaanza hapo
 
Zawadi ya mshindi wa EPL ambayo alichukuwa Man City msimu uliopita ni £150m. Wakati huo Man City wamemnunua Jack Grealish kwa £100m. Tafsiri yake zawadi waliopata hawawezi kununua kina Jack Grealish wawili. Bajeti ya timu kwa msimu lazima iwe kubwa kuliko zawadi ya ubingwa wa Ligi sababu bajeti inagusa vitu vingi. Klabu hazitegemei mapato kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye zawadi ya ubingwa. Ubingwa ndiyo unaleta fursa nyingine za mapato.
 
Tujadili hoja sio hivi vioja.

Ubora wa ligi unaanzia hata kupima gharama za vilabu wanazutumia katika kuwekeza.

Hiyo hela hata kwa msimu mmoja tu bado ni ndogo.

Tunapigania ushindani, ili timu ndogo zipate fedha na kuweza kushindana.

Mwisho wa siku ni Simba na Yanga zitaendelea kutawala soka.
Ulikwenda kuomba udhamini milango ya TFF ikafungwa kwako? Au ni kulalamika tu mishaona wengine wame act
 
Mwenyewe natofautiana na TFF mambo mengi ila kwa hili nawapongeza sana, maana tunaelewa hali na mazingira yalivyo magumu kwenye biashara awamu hizi 2, kupata mdhamin wa kutoa 2.5 B per year si jambo la kitoto!
Hali ngumu wapi.. katazame financials za CRDB na NMB kisha urudi hapa.

Umeona makusanyo ya TRA juzi. Unasemaje hali ngumu.
 
Zawadi ya mshindi wa EPL ambayo alichukuwa Man City msimu uliopita ni £150m. Wakati huo Man City wamemnunua Jack Grealish kwa £100m. Tafsiri yake zawadi waliopata hawawezi kununua kina Jack Grealish wawili. Bajeti ya timu kwa msimu lazima iwe kubwa kuliko zawadi ya ubingwa wa Ligi sababu bajeti inagusa vitu vingi. Klabu hazitegemei mapato kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye zawadi ya ubingwa. Ubingwa ndiyo unaleta fursa nyingine za mapato.
Zawadi ya mshindi wa kwanza ingekuwa unapata pesa ambayo unaweza ukasajili mchezaji mkubwa mmoja wa Afrika kwa bei ghali basi kungekuwa na maana

Ila bahati mbaya zaidi huwezi kusajili mchezaji wa kigeni hata mmoja kwa kutumia zawadi ya mshindi wa kwanza

Go east or west, Pesa ya mdhamini lazima iwe na chachu kwa namna yeyote ile endapo akipata na hapa kwetu ni tofauti
 
Hivi Watani zetu kutoka Jangwani mbona mna roho mbaya namna hii lakini?!

Yaani mipesa yote mnayolipwa na Azam kwa ajili ya haki ya matangazo tu, si zingetosha kabisa kudhamini ligi yetu kwa miaka nenda rudi?!
 
Habarini Za Wakati kama Huu…

Vilabu vyetu vinavyoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara huwa vinahangaika sana kwenye kuhakikisha Ligi Yetu Inakuwa Bora na Yenye kusisimua, Haya huonekana Wakati wa Usajiri na wakati wa Maandalizi ya Msimu Mpya. Wamekuwa Wakihangaika Sana kutafuta wadhamini na Wadau mbalimbali kuhakikisha Timu inakuwa imara na yenye ushindani Lengo likiwa ni Kuifanya ligi yetu kuwa bora.

Kupitia Haya Vilabu vimefanikiwa sasa ligi Yetu inashika Nafasi ya 8 afrika kwa Ubora.

Je TFF wanafanya nini Kuhakikisha kuwa Ligi yetu inazidi kuwa Bora, kubwa na yenye kuvutia? Ni kuendelea kutafuta wadhamini.

Lakini Najiuliza ni KWANINI TFF imekubali Udhamini Wa Tsh 2.5 Billioni Tuuuu… Kwa Level ya Ligi yetu ilipofikia, Kumpokea mdhamini wa 2.5 Billioni Ni Kuidharirisha Ligi yetu na Kuto itakaia Mema.

Niwe Muwazi Nilipo anza kusikia Tetesi kuwa NBC anaenda Kuwa Mdhamini nilijua Tuu hapa hamna Pesa Ni Porojo. Haiwezekani Mdhamini wa Ligi kwa Miaka 3 akaweza 2.5 Billioni kwa Vilabu Karibia 16 huku ni kurudisha Nyuma Ligi yetu na Kutokuitakia Mema Ligi Yetu.

Kiukweli TFF mnahusika Kwa Asilimia 100 kuihujumu Ligi Yetu. 2.5 Billioni Kumbe hata Vunja Bei, Clouds, Wasafi na Wengine wangeweza kuweka Hilo dau na Zaidi.

Swali Ni je TFF mlikosa Mdhamini wa zaidi ya 2.5 Billioni? Au vigezo vyenu ni vipi katika hili? Mnafikiria hali halisi ya Tanzania na vilabu vyake na Ligi ilipofikia? Mbona Azam Aliweka Pesa ndefu kila mtu akanyanyua mikono juu?

Ifike pahala sasa TFF uchaguzi wake uwe unafanywa na vilabu na wadau wa soka ili tupate viongozi wenye akili wanaoweza Kuifikisha ligi yetu pahala fulani.

Kama Ligi Ina Mdhamini wa 2.5 Billioni unategema Kuna Club itakuja kutoka na kusajiri Mchezaji wa Zaidi ya 2.5 Billioni au hata Wa 1 Billioni?

TFF na NBC mmetupiga na kitu Kizito Kichwani wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania.

Karia OUT
Mkuu ukiambiwa umlete mdhamini wa trilion4 kwa mwaka utamleta? Ok trilion4 nyingi mlete wa 3B kwa msimu ili nasisi tukuunge mkono kwenye hizi porojo zako
 
Bid ikiwekwa mezani, anayetafuta biashara ni yule anayebid...

Highest bidder anawin tender...TFF hakuwa akitafuta business partner bali alikuwa akitafuta mnunuzi wa bidhaa yake ambayo ni ligi ya TZ
Na mnunuzi kapatikana NBC
 
Tujadili hoja sio hivi vioja.

Ubora wa ligi unaanzia hata kupima gharama za vilabu wanazutumia katika kuwekeza.

Hiyo hela hata kwa msimu mmoja tu bado ni ndogo.

Tunapigania ushindani, ili timu ndogo zipate fedha na kuweza kushindana.

Mwisho wa siku ni Simba na Yanga zitaendelea kutawala soka.
Nakubaliana na wewe.
 
Ni muhimu kuwa na udhamini mkubwa kwenye ligi maana unamfaidisha mpaka mwenye uwezo mdogo kifedha. Ni muhimu kuwafikiria wadogo na kuwapigania ili ushindani uwiane
 
Back
Top Bottom