Hivi hebu nieleweshen kipimo cha ubora wa ligi yetu ni club kutumia pesa nyingi kusajili au vilabu vyetu kufanya vizuri mashindano ya nje..
Maana swala la vilabu kutumia fedha nyingi.. Halipandishi hadhi ya ligi
Tukija kwenye Vilabu vyetu na mashindano ya nje... Ni Simba tu walau wamefika robo fainali ndan ya miaka 5...
Sasa unataka mdhamin aweke pesa ndefu kwa kigezo kipi ikiwa .. Huna viwanja vya mpira vya maana... Club zenu hazina structure ya kueleweka... mashindano nje ndio hivyo homa za vipindi
Bado mnataka mdhaminiwe kwa bilion 100.. Wakat uwanjan mashabiki hadi mechi kubwa
Ndo viwanja vijae...
Tatizo mnapima ligi kwa kuangalia Simba, Yanga na Azam.. Tunaweza tukawa namba nane kwa ubora sababu tuko kwenye kundi la wasiojiweza... Kwenye kundi la vipofu akiwepo mwenye chongo yeye ndo atakuwa kawazid wenzie ... Ila haimanishi kwamba yuko kamili
Nenden na uhalisia wenu... Ingekuwa ligi yetu ni bora kihivyo achilia mbali udhamin wa ligi ila vilabu vyote vingekuwa na wadhamin kwa pesa ya maana... Automaticaly mdhamin wa ligi angetoa peaa ndefu