TFF na NBC hazijawatendea haki wapenzi wa mpira wa miguu Tanzania

Hivi unajua geti collection za baadhi ya timu hata 1M hua hazifiki? Mmkianza mgawanyo unakuta timu inatoka na laki tano! Je wako kama NBC watarudisha vipi pesa zao??
Mwaka jana ligi kuu sijui ilikuwa timu gani na timu gani ,walipata si zaidi ya elfu 17 (17,000) ,na tff wanataka mgao humo humo hela hata ya maji ya kunywa wachezaji haitoshi ,hizi timu ndogo zingine zinaambuliwa wakicheza simba na yanga
 
Unataka mtu aweke pesa zaidi ya 2.5 kwa lipi yaani?

Ukiitoa Simba pekee ligi nzima kuna klabu gani ya maana inayotambulika Afrika?

Ligi hii imepata angalau thamani kwa juhudi ya Simba SC.

Hicho kiasi kinastahili kabisa.
Matumizi tu ya Simba kwa mwaka nadhani ni sawa na thamani waliyoweka NBC ,piga mahesababu Safari zote za ndege ,vyakula na malazi
 
Asante sana kwa kumbukizi hii! Sasa hapa NBC watarudisha vipi pesa zao?? Timu ndogo za Ligi Kuu,zinapitia changamoto kubwa mno!
Sijawahi kufahamu kama mdhamini mkuu wa ligi naye huwa anakuwa na mgawo wake kwenye gate collection ,maana tff ni lazima ,Kodi ya serikali ni lazima ,viwanja vya ccm ni lazima kulipwa ,halafu tena mdhamini anataka chake ?
 
Hapo inawezekana NBC wamejiongeza kama tickets zitalipwa kwa mfumo wao basi watafaidika
 
Kitu mm nimeshangaa sjaona wakisema mshindi wakwanza atapata nn mshindi wapili nn na wengine sjaona zawad ya mchezaji Bora kuhusu NBC kuwa title sponsor sikutegemea Kama ataweza kutoa pesa ndefu huu ndo uwezo wao apo ukiangalia n Kama milion 100 kwamwaka kwa kila club
 
ligi imeanza na ilikuwa inaenda bila na mdhamini kujitokeza.. amejitokeza mdau kwa dau ndogo bado unalalamika?

heri kuwa na 0 Tsh ya udhamini au kuwa na 2.5b Tsh?
Hao ndio wabongo mkuu,tena ukizama ndani zaidi ni kwa sababu mdhamini nembo yake ni red,watz akili zao ni ndogo sna,bora mi nipo mpakani na nchi jirani,wenzetu wanajitahidi sna,hawana arguments za ajabu ajabu kama zetu
 
Hujatumwa Wewe na Kilo Mia nane Kweli...? Tuna Mashaka ...Huko Yanga ndo Mungu aliumba Watu Wenye Uwezo mdogo Kutafakari Mambo
 
Sijawahi kufahamu kama mdhamini mkuu wa ligi naye huwa anakuwa na mgawo wake kwenye gate collection ,maana tff ni lazima ,Kodi ya serikali ni lazima ,viwanja vya ccm ni lazima kulipwa ,halafu tena mdhamini anataka chake ?
No sio mdhamini anataka chake bali atataka kila kinachopatikana kinapitia kwake yaani tff, vilabu nk wawe na akaunti NBC, sasa mdau ndio kasema timu zinapata 17000 kama gate collection hata ikipitia NBC bado ni ngumu kwa NBC kufaidika
 
Ligi ya Tanzania inakosa msisimko kwa sababu kila mdhamini anataka either Simba au Yanga kutwaa ubingwa, they don't care kuhusu timu zingine.
 
Zawadi ya mshindi wa kwanza haifikii hata bajeti ya hizi timu kongwe ktk uendeshaji kwa msimu mzima

Tatizo ndio linaanza hapo
Hata kwenye ligi zingine kubwa duniani zawadi za mshindi huwa ndogo kuliko bajeti.

Ila vilabu hupata faida kupitia matangazo ya biashara, mauzo ya tiketi, udhamini wa klabu, mauzo ya wachezaji na uwekezaji wa matajiri/kampuni kwenye klabu.
 
Ni muhimu kuwa na udhamini mkubwa kwenye ligi maana unamfaidisha mpaka mwenye uwezo mdogo kifedha. Ni muhimu kuwafikiria wadogo na kuwapigania ili ushindani uwiane
Azam kafanya hayo kupitia mkataba alioingia na Tff wakuonyesha mechi za ligi, hivyo hata timu ndogo zitapata kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…