TFF na TAKUKURU waangalie hili suala la upangaji wa matokeo linalofanywa na Yanga wakishirikiana na washirika wao Singida Big stars

TFF na TAKUKURU waangalie hili suala la upangaji wa matokeo linalofanywa na Yanga wakishirikiana na washirika wao Singida Big stars

Naunga mkono hoja pia tff na takukuru waitazame yanga vs simba kuna upangaji wa matokeo..

Haiwekani timu kinwa kama Simba kufungwa mechi nne mfululizo, kuna dalili ya vinasaba.
Hili hata muhasibu okwi BOBAN SUNZU analijua.
Walishatazama ndio maana kina Kayoko hawaonekani
 
Bila ya kupepesa macho suala lililifanywa hivi leo na Singida Black stars linaonesha viashiria vyote vya upangaji wa matokeo katika ligi kuu ya NBC nchini Tanzania.

Yaani Singida BS wameanza na kikosi kwa kuweka nje nyota wake wote wapya ww kimataifa huku wakianza wachezaji wenye viawango vidogo na kawaida ili kuwarahisishia ushindi timu ya Yanga ,ishike usukani wa ligi kuu.

Bodi ya Ligi, TFF na TAKUKURU Waingilie kati sakata hili. Mbona Singida Black stars wakicheza na Simba na Azam huwa wanakamia sana mechi na kuanzisha strong first eleven tofauti na wakicheza na timu yenye vinasaba nao , Dar Young Afirika?

Kulikuwa na ulazima wowote wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Jonathan Sowah kukaa benchi?

Je kulikuwa na sababu gani ya Arthur ,imoro,chukwu n.k kukaa benchi dhidi ya Yanga?

Na tumeshuhudia first half jinsi walivyoiachia Yanga ipate goli mbili na kuifanya mechi kuwa imeisha.
Waanze na waliokesha uwanja wa JKT usiku kucha wakiwanga wakati mechi sio ya kwao.
 
Simba ndio timu inayoongoza kwa ushindi wa magumashi,, Fanya utafiti utajua ni timu Gani malalamiko yamekuwa mengi kwake,,sasa huo uongozi tunaousema sijui ni upi utaojitokeza wakati viongozi wenu ndio vinara wa kupanga matokeo!
Unategemea timu zinazofadhiriwa na GSM ziache kulalamika zinapokandwa na mnyama
 
Ushahidi upo, wawekeze kuutafuta. Yanga inapanga matokeo
Nani awekeze kuutafuta? Hilo ni wajibu wa kila mdau sio mtu mmoja au kikundi cha watu maalumu. Hata wewe unaweza kuanza kuwekeza kuutafuta kwasababu linakugusa kisha wadau wengine wanaopenda soka la haki watafuata. Msisubiri viongozi wafanye kuna matawi na magroup mengi tu ya Simba mkiamua hilo halishindikani chukueni maamuzi badala ya kila siku kulia lia
 
Suala la Yanga kupanga matokeo halina utatuzi. Bahati mbaya uongozi wa Simba unajisikia unyonge kukusanya ushahidi na kulikemea. Siku wakifanya hivyo ndio namlaka zitajifanya kustuka
20250217_185026.jpg
 
Suala la Yanga kupanga matokeo halina utatuzi. Bahati mbaya uongozi wa Simba unajisikia unyonge kukusanya ushahidi na kulikemea. Siku wakifanya hivyo ndio namlaka zitajifanya kustuka
Endeleeni kujenga team ili muwe washindani halisi, unyonge sio sifa njema mcje mkala chuma 5 kwa mara nyingine.
 
Hii kwa simba ndio nzuri sana, maana kama tunavyoona club bingwa na shirikisho tunavyotawala, hawa siku wakija kustuka Simba ameshaleta kombe ndio nao watakavyozinduka. Yuke kocha aliongea ukweli watu wakamzodoa
 
Kilicho fanyika leo ndo kilicho fachika kati ya Tabora united na Simba mkoani tabora.
Ligi ya hapa Nbc imejaa upangaji na yote hii ni kwasababu ya wanasiasa kujiingiza kwenye michezo kwa kutafuta umaarifu wa dezo.
 
Mbona milio imekuwa mingi humu! Mmesahau game ya Simba vs Tabora wachezaji muhim wa tabora kama akina Makambo walitoweka ghafla🤣
 
Ukiumia kuchomoa... Mlitaka singida afungwe bao 5 kama 5imba alivyo kojolewa na Yanga..?💩
 
Bila ya kupepesa macho suala lililifanywa hivi leo na Singida Black stars linaonesha viashiria vyote vya upangaji wa matokeo katika ligi kuu ya NBC nchini Tanzania.

Yaani Singida BS wameanza na kikosi kwa kuweka nje nyota wake wote wapya ww kimataifa huku wakianza wachezaji wenye viawango vidogo na kawaida ili kuwarahisishia ushindi timu ya Yanga ,ishike usukani wa ligi kuu.

Bodi ya Ligi, TFF na TAKUKURU Waingilie kati sakata hili. Mbona Singida Black stars wakicheza na Simba na Azam huwa wanakamia sana mechi na kuanzisha strong first eleven tofauti na wakicheza na timu yenye vinasaba nao , Dar Young Afirika?

Kulikuwa na ulazima wowote wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana Jonathan Sowah kukaa benchi?

Je kulikuwa na sababu gani ya Arthur ,imoro,chukwu n.k kukaa benchi dhidi ya Yanga?

Na tumeshuhudia first half jinsi walivyoiachia Yanga ipate goli mbili na kuifanya mechi kuwa imeisha.
Na huu ni mwanzo tu.
Muda si mrefu kelele zitahamia kwa Mangungu, Matola, Kapombe, na wachezaji wote wa Simba!! Na hii ndiyo hulka yenu.
 
Simba unavyowaona wanashinda kwa tabu kwa kuwa kila timu inaikamia hasa zile 7 zinazodhaminiwa na gsm
Matokeo yake hili linawakomaza kwani wameshajua kila mechi kwao ni kama fainali,ndio maana kimataifa wanafanya vyema.
Yani unacheza na kiluvya wa uarabuni alafu unakuja kutubania pua eti kimataifa tunafanya vizuri!!!!
 
wachezaji wanacheza kwa maelekezo kutoka kwa wamiliki wao
Vipi na Simba ilipofungwa mara 4 mfululizo na Yanga hiyo hiyo, wachezaji kama Mousa Camara, Aishi Manura, Kelvin Kijili, na wengineo wengi; walicheza kwa maelekezo ya Mo, au Mangungu?
 
Halafu hayo magoli ya vyura umeyaona sasa,ndio maana hawa wajuba kimataifa hawatoboi,maelekezo ni mengi sana

Mtu anapiga header peke yake wachezaji wa timu pinzani hata hawajigusi hata kuzuga kwa kuruka tu.

Halafu mbaya zaidi mpira umeisha michezaji ya SBS inatabasamu,yaani,hawaoni huzuni ya kupoteza wakati wangefungwa na Simba malalamiko ya Simba kubebwa yangekuwa ya kutosha tu
Ila Aziz Kii na Nzengeli wakiwatoboa akina Manula na Camara, wala hakuna shida!! Na yanakuwa ni magoli mazuri kweli kweli!! 😁 Kweli Rage alikuwa sahihi kabisa.
 
Ushahidi upo, wawekeze kuutafuta. Yanga inapanga matokeo
Na tarehe 8 mkusanye ushahidi wa kutosha. Nimepata taarifa muda si mrefu, kuna muendelezo mwingine wa upangaji wa matokeo kwa siku hiyo.

Haiwezekani timu moja, ifungwe na Yanga mara 4 mfululizo! Na hiyo tarehe 8 itakuwa ni mara ya 5 mfululizo!
 
Halafu hayo magoli ya vyura umeyaona sasa,ndio maana hawa wajuba kimataifa hawatoboi,maelekezo ni mengi sana

Mtu anapiga header peke yake wachezaji wa timu pinzani hata hawajigusi hata kuzuga kwa kuruka tu.

Halafu mbaya zaidi mpira umeisha michezaji ya SBS inatabasamu,yaani,hawaoni huzuni ya kupoteza wakati wangefungwa na Simba malalamiko ya Simba kubebwa yangekuwa ya kutosha tu
Walifika fainali unasemaje hawatoboi
 
Kwa timu gani hasa walizokutana nazo huko mnakokuita kimataifa
Mara ya mwisho kuiona Simba ikiishia makundi kimataifa ilikuwa lini?Simba imetoboa kwenye kundi lenye Al Ahly,AS Vita,Wydad na hata kuongoza kundi mbele ya Al Ahly
 
Back
Top Bottom