TFF tofautisheni ligi yetu na zile za Ulaya kwa mengi, mazingira ni tofauti

TFF tofautisheni ligi yetu na zile za Ulaya kwa mengi, mazingira ni tofauti

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Masaa 72 ya Ulaya na masaa 72 ya Tanzania ni tofauti kabisa. Think globally Act locally.

Masaa 72 ya kucheza baina ya mechi yamezingatia vitu mbalimbali ambavyo Tanzania havipo. Baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na:

1. Ubora wa viwanja vyao: Wachezaji hawaumii sana mara kwa mara kwasababu za uwanja.

2. Umbali vilipo viwanja vya mechi. Ulaya ina vinchi vidogo sana ambavyo timu zinatumia muda mchache kufika eneo itakapochezwa mechi.

3. Ubora wa huduma za afya/matibabu kwa wachezaji ni bora sana kuliko kwetu

4. Ubora wa lishe ya wachezaji. wachezaji wao wanakula vyakula vinavyoponyesha haraka mwili wa mchezaji

5. Ubora wa usafiri wao kwenda mechi zilipo ni bora kulinganisha na kwetu

6. Ubora wa wachezaji wa timu za ulaya. Wachezaji wa timu za ulaya wamepitia shule za mpira tangu utotoni, hivyo wanajua umuhimu wa kulinda afya zao na za wengine wakiwa uwanjani na nje ya uwanja.

7. Malipo makubwa. Mchezaji anaelipwa pesa nyingi ni rahisi kujitunza yeye mwenyewe, hana stress.

8. Ubora wa marefa wao ni bora kuliko kwetu. Hii inasaidia kulinda wachezaji bora wasikamiwe na kuumizwa mara kwa mara.

9. Vifaa bora vya mazoezi na wataalam wa mazoezi bora kuliko kwetu.

Mjumuiko wa supporting factors hizi huko ulaya ndio uliozaa masaa yao 72 kwa mechi kuchezwa. Je, hapa kwetu mazingira yetu yanaruhusu kanuni ya masaa 72 sawa na ligi kuu ya England, Ufaransa au Italy?

Tunakopi kila kitu kama madodoki; ujinga mtupu.
 
ni ama zipunguzwe timu kwenye ligi ziwe 12 au ligi ichezwe siku 365 kwa span ya wiki wiki.
Sio lazima kupunguza timu, bali unaweza kuondoa ushiriki wa timu kwenye mashindano yasiokuwa ya lazima yanayorefusha ligi bila sababu. Pili, bodi ya ligi ipange ratiba kwa kuzingatia hali ya viwanga mechi itakapochezwa na umbali timu itatakiwa kusafiri badala ya kupanga ratiba ya jumlajumla tu (generalization/stereotyping). Yaani unaenda case kwa case. Kwa viwanja vya da es salaam na timu za dar es salaam zisizohitaji kusafiri nje ya mkoa
 
Angalau timu zicheze mechi baada ya masaa 96
 
Wakati timu nyingine zinapangiwa ratiba mbovu hamkuona tatizo ila ilipowakuta ndio mkaona tatizo.
 
Wakati timu nyingine zinapangiwa ratiba mbovu hamkuona tatizo ila ilipowakuta ndio mkaona tatizo.
Hoja yangu hii sio malalamiko ya timu iliyoonewa, bali udodoki wa viongozi wetu wa mpira ambao wanaiga kila kitu kutoka mashirikisho mengine ya mpira bila kuiga pia mazingira yanayosapoti matukio hayo huko kwao.

Udodoki huu wa viongozi wetu hausaidii mpora wetu kwenye ligi na hata kimataifa kwakuwa unazalisha majeraha mengi kwa wachezaji na matokeo feki kwa mechi zetu.
 
wakati wa Uchebe Simba ilikuwa inacheza kila baada ya siku mbili hatukusikia malamiko, Simba ilitoka kucheza na Wydad Morocco kufika ikaenda Lindi kucheza na Namungo kwenye ligi baadae na Azam nusu fainali ya shirikisho Mtwara ndani ya wiki hatukusikia malalamiko, Simba tena ilitoka Morroco ikaunganisha Kigoma kucheza na Mashujaa shirikisho hatukusikia malalamiko.
unaweza kuwa na pointi lakini kama kipindi kile uliona ni sawa kwa Simba basi mtakuwa mnadeka.
 
Timu zina wachezaji 28 na zaidi wacheze wote kama unawachezaji wa kukamilisha idadi kazi ipo
 
Back
Top Bottom