kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Masaa 72 ya Ulaya na masaa 72 ya Tanzania ni tofauti kabisa. Think globally Act locally.
Masaa 72 ya kucheza baina ya mechi yamezingatia vitu mbalimbali ambavyo Tanzania havipo. Baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na:
1. Ubora wa viwanja vyao: Wachezaji hawaumii sana mara kwa mara kwasababu za uwanja.
2. Umbali vilipo viwanja vya mechi. Ulaya ina vinchi vidogo sana ambavyo timu zinatumia muda mchache kufika eneo itakapochezwa mechi.
3. Ubora wa huduma za afya/matibabu kwa wachezaji ni bora sana kuliko kwetu
4. Ubora wa lishe ya wachezaji. wachezaji wao wanakula vyakula vinavyoponyesha haraka mwili wa mchezaji
5. Ubora wa usafiri wao kwenda mechi zilipo ni bora kulinganisha na kwetu
6. Ubora wa wachezaji wa timu za ulaya. Wachezaji wa timu za ulaya wamepitia shule za mpira tangu utotoni, hivyo wanajua umuhimu wa kulinda afya zao na za wengine wakiwa uwanjani na nje ya uwanja.
7. Malipo makubwa. Mchezaji anaelipwa pesa nyingi ni rahisi kujitunza yeye mwenyewe, hana stress.
8. Ubora wa marefa wao ni bora kuliko kwetu. Hii inasaidia kulinda wachezaji bora wasikamiwe na kuumizwa mara kwa mara.
9. Vifaa bora vya mazoezi na wataalam wa mazoezi bora kuliko kwetu.
Mjumuiko wa supporting factors hizi huko ulaya ndio uliozaa masaa yao 72 kwa mechi kuchezwa. Je, hapa kwetu mazingira yetu yanaruhusu kanuni ya masaa 72 sawa na ligi kuu ya England, Ufaransa au Italy?
Tunakopi kila kitu kama madodoki; ujinga mtupu.