Kazitunayo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2013
- 3,782
- 3,199
Kagera walikata rufaa kua mchezaji wao hana kadi 3 leo imezibitika kweli alikua ana kadi 3 alafu point wanapewa only in bongo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Breaking Newzz: TFF yamfungia Haji Manara miezi 12
MUUNGWANA BLOG / 12 minutes ago

Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara.Pia nakulipa faini ya Shilingi milioni 9.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Hahahaa! Sio kwa hasira hizo mkuu inabidi mkubali tu ndio mpira huo.Mpira Tz kwishaaaa. Simba tunajiondoa kwenye ligi na kuwaachieni timu zenyu. Sote tunahamia UAR kwenda jiandikisha huko na tutakutana kwenye ligi ya dunia. Lazima alogwe mtu hapa. Aalah! Mnatuchezea?? Yanga mtafungwa goli 20 kila mechi ambayo mtacheza tangu leo. Mtaona
Mkuu, umenifanya nirudie kuusoma uzi upya; hapo kweny bold umepatoa wapi?Swala nimchezaji alikua na kadi au hana? mbona alivyoitwa kuhojiwa pamoja na viongozi wao kagera wanasema alikua na kadi 2 leo Tff wanasema ana kadi 3 ataitumikia mechi ijayo...wewe kiazi malinzi acha ukabila
Kwa hiyo kwenye hukumu suala la mchezaji kupewa kadi 2,1,0 au tatu ni exclusive kabisa? Yaani ukweli wa idadi kadi alizopewa mchezaji limekuwa nullified na kasoro hizo?
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuipoka Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.
Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 71.
Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na nsipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zimechangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo alisitaja kuwa ni:
“Malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa, malalamiko yao hayakuwa katika njia ya maandishi, rufaa ya Simba haikulipiwa ada, kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali kutokana na kuwashirikisha watu ambao hawana uhalali wa kuwa kwenye kikao.
“Kutokana na sababu hizo kamati imeamua kufuta maamuzi yaliyochukuliwa na Kamati ya Saa 72 na kurejesha matokeo kama yalivyokuwa, pia kamati imemuagiza katibu mkuu wa TFF kuwapeweleka baadhi ya wajumbe wa bodi ya ligi katika Kamati ya Maadili ya TFF kwa kosa la kwenda kinyume na kazi zao,” alisema Mwesigwa.
Hahaha hii a.k.a nimeipenda sana Wallah!Mezani fc
Huyu dogo mtoa povu miezi kumi na mbili haimtoshi.Breaking Newzz: TFF yamfungia Haji Manara miezi 12
MUUNGWANA BLOG / 12 minutes ago

Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara.Pia nakulipa faini ya Shilingi milioni 9.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]Nasikia Simba wamepanga kuandamana ili utaratibu ubadilishwe - mpira uchezwe mezani na ugali uliwe uwanjani.....
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] kwani halina ulinzi mkali.daa masikini mnyama sasa hawezi kuwinda tena sasa usubiri ufe tuu
au wamtafute Bashite akaliibe kombe pale TFF