Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa jamaa walidhani TFF ya babu yao, wanacheza halafu wanaenda kulala vitandani, wakichoka kulala ndo wanaenda kukata rufaa wakati muda umekwisha, tena kwa ulimi badala ya maandishi!! Halafu hata hela ya kulipia rufaa hawana, si wanamfadhili wao anaitwa MO?
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetangaza kuipoka Simba pointi tatu na mabao matatu ambazo ilipewa kutokana na mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar.
Wiki mbili zilizopita Simba ilipoteza mchezo dhidi ya Kagera kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara lakini baadaye ilikata rufaa ikipinga Kagera kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi ikidai alikuwa na kadi tatu za njano, ndipo ikapewa ushindi huo kupitia Kamati ya Saa 71.
Mara baada ya kamati hiyo kuipa Simba pointi Kagera ikaomba kupitiwa upya kwa suala hilo na nsipo TFF ikatangaza kuwa suala hilo sasa litakuwa chini ya Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ambayo ndiyo imetoa maamuzi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kuwa kuna sababu kadhaa zimechangia kuchukuliwa kwa maamuzi hayo ambapo alisitaja kuwa ni:
“Malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa kwa wakati muafaka tangu mchezo ulipochezwa, malalamiko yao hayakuwa katika njia ya maandishi, rufaa ya Simba haikulipiwa ada, kikao cha Kamati ya Saa 72 kilikosa uhalali kutokana na kuwashirikisha watu ambao hawana uhalali wa kuwa kwenye kikao.
“Kutokana na sababu hizo kamati imeamua kufuta maamuzi yaliyochukuliwa na Kamati ya Saa 72 na kurejesha matokeo kama yalivyokuwa, pia kamati imemuagiza katibu mkuu wa TFF kuwapeweleka baadhi ya wajumbe wa bodi ya ligi katika Kamati ya Maadili ya TFF kwa kosa la kwenda kinyume na kazi zao,” alisema Mwesigwa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Hans Pope nae saa hizi anakunywa supu ya miba anashushia na kokoto za kunduchi.
Ndio washaoshwa watulie kelele za nini?Simba wanakumbushiwa tu sakata la Lufunga kuwa na red card akawepo kwenye kikosi dhidi ya Police Dar, kamati hii inayoongizwa na Simba ikaitupa rufaa ya Police kwa kigezo cha kuletwa nje ya muda na haikulipiwa ada leo hii Simba nao wanakosa kumbukumbu yaani wanakata rufaa nje ya muda na tena sio kwa maandishi na hawakulipa ada.
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu nzuri, ni Simba hawa walimchezesha Ajib akiwa na kadi 3 wakadai wameiandikia bodi ya ligi mchezaji awe anachagua mechi.
Muosha huoshwa japo siikubali tff ila simba ndio waasisi wa hii michezo ya kitoto.
Mo alishakimbilia Singida United baada ya kushindwa kujimilikisha SSC!Hawa jamaa walidhani TFF ya babu yao, wanacheza halafu wanaenda kulala vitandani, wakichoka kulala ndo wanaenda kukata rufaa wakati muda umekwisha, tena kwa ulimi badala ya maandishi!! Halafu hata hela ya kulipia rufaa hawana, si wanamfadhili wao anaitwa MO?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji85] [emoji85] [emoji85]arsenal tumeshinda jana
Cha ajabu hawajaongelea hili, wanadai Simba hawakulipa 300,000 ya shitaka lao pia walichelewa kushtaki atiKatika hizo sqbabu hoja ya msingi haijaonyeshwa je anakadi tatu za njano?
Mpira uwanjaniMimi nilifikiri wameangalia SUBSTANCE ya madai yenyewe kumbe wamejikita kwenye FORM? irregularity hizo kisheria ni curable na ni maoni yangu kuwa wangetoa hukumu ya re trial tofauti na walivyofanya kuwatolea nje madai yao kwa technical ground.
Mpira Tz kwishaaaa. Simba tunajiondoa kwenye ligi na kuwaachieni timu zenyu. Sote tunahamia UAR kwenda jiandikisha huko na tutakutana kwenye ligi ya dunia. Lazima alogwe mtu hapa. Aalah! Mnatuchezea?? Yanga mtafungwa goli 20 kila mechi ambayo mtacheza tangu leo. Mtaona
huyu jamaa kafungiwa kwa kulilia point za mezani.
Aibu ya Maandamano Sc.
Mpira uwanjani
Wacheze mpira waache siasaHawa jamaa walidhani TFF ya babu yao, wanacheza halafu wanaenda kulala vitandani, wakichoka kulala ndo wanaenda kukata rufaa wakati muda umekwisha, tena kwa ulimi badala ya maandishi!! Halafu hata hela ya kulipia rufaa hawana, si wanamfadhili wao anaitwa MO?
Duh! nilikuwa oudated mkuu, kumbe MO alishasepa!.Ndo mana wanaweweseka...Mo alishakimbilia Singida United baada ya kushindwa kujimilikisha SSC!
Hii ni AfricaKwa hiyo kwenye hukumu suala la mchezaji kupewa kadi 2,1,0 au tatu ni exclusive kabisa? Yaani ukweli wa idadi kadi alizopewa mchezaji limekuwa nullified na kasoro hizo?
Kazi ipo!
Umesahau Polisi waliponyimwa points za mezani kutoka kwa simba kwa grounds hizo hizo? (1).kuchelewa kukata rufaa ndani ya masaa 72 (2) kutokulipia T sh 300,000 ambayo ni ada ya rufaa. mazingira ni hayo hayo na kanuni ipo....what goes around comes around,muhimu simba wakumbuke kuwa kinachokwenda na kukufaidisha,kikirudi na kukupa hasara inabidi uoneshe uungwana kwa kuwa mpole, kama inauma ni kuziangalia kanuni kwa pamoja na kuziondoa zilizo mbaya,zikishakaa kwenye mstari ni kujiandaa kunyolewa tu.Cha ajabu hawajaongelea hili, wanadai Simba hawakulipa 300,000 ya shitaka lao pia walichelewa kushtaki ati
TFF ilitoa na TFF imetwaa.Ndio washaoshwa watulie kelele za nini?