Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Ndo hapo sasa uone utofauti wa umakini kati ya askari wetu na askari wao.Kama kweli SA na TZ Wana Mikataba ya kiulinzi,mbona kuna wahalifu wengi tu wameharibu TZ na Wamejificha huko SA na Serekali ya SA wala haina habari nao!? Mfano mdogo tu ni Alex Masawe!!
Kweli kabisa. Askari wa Kenya ni njaa kali. Yani mtu unanunua haki yako mwenyewe ili mambo yako au kesi yako iende.Sema kwa William Ruto, the Hustler! Hana hata mishahara ya kuwalipa Askari, jamaa angeingia Kenya [emoji1139] angepewa mpaka Ulinzi, maana jamaa wana njaa ya hatari. [emoji23][emoji23][emoji23]
Hata Marekani taifa kubwa, tajiri, lenye nguvu, teknolojia na uwezo wa kila aina lakini limejaa wahalifu na inaongoza kwa mauaji ya kiholela.Sawa. Polisi wa Tz anafuatilia habari za mhalifu wa SA ili akija Tz amkamate huku akishindwa kupambana na wahalifu wa nchini kwake. Safi sana.
Nachosema ni kuwa "askari wa Tz yuko busy kufuatilia taarifa za mhalifu wa SA" huku hana taarifa za wahalifu wa nchini mwake.Hata Marekani taifa kubwa, tajiri, lenye nguvu, teknolojia na uwezo wa kila aina lakini limejaa wahalifu na inaongoza kwa mauaji ya kiholela.
Watu wanapigwa risasi kila siku mchana kweupe, hapo sijazungumzia wauza madawa, majambazi ya bank na uhalifu mungine.
Hakuna nchi inayokosa uhalifu duniani. Tembea uone, au fuatilia taarifa za habari ujifunze.
Maelfu ya wafungwa waliopo jela ni nani aliefuatilia taarifa zao na kuwakamata?Nachosema ni kuwa "askari wa Tz yuko busy kufuatilia taarifa za mhalifu wa SA" huku hana taarifa za wahalifu wa nchini mwake.
nashukuru kwa taarifa ila serikali ya ccm isipokuwa makini TANPOL itakuwa mbovu zaidi!!!Mkuu,SAPS ni takataka kabisaa,huwezi kuofananisha na @tanpol kwa namna yoyote,SAPS ni kitengo cha majizi tu,juzi hapo wamekamatwa wakihusishwa na utekaji wa magari ya kusafirisha fedha CIT,polisi wa South ni certified criminal,angalau bongo kuna polisi wanajali kidogo,ila sio hawa wa south
SA na TZ wana mikataba ya kiulinzi na usalama, ndio maana ilikuwa rahisi Mr Bester kukamatwa nchi TZ na kukabidhiwa kwa mamlaka ya SA.
Swala la dereva wa Lisu linatemea na nchi aliyopo. Kuna nchi ambazo hatuna mikataba nazo ya ulinzi na usalama. Kwahiyo hata serikali yetu ikijua kuwa dereva huyo yupo katika nchi hizo, kamwe haiwezi kuwa na uwezo wa kuingia katika nchi hizo na kumkamata dereva huyo. Hivyo swala la Lisu na huyu Mr. Bester ni mambo mawili tofauti.
🤣🤣🤣🤣 Kwamba serikali iache kuingia mikataba ya kiuchumi na maendeleo kwa faida ya taifa, badala yake iingie mkataba na Ubelgiji sababu tu ya kumkamata dereva wa Lisu?..toka mwaka 2017 mpaka leo 2023 ni muda mrefu na unatosha kuandikishana mkataba kati ya Polisi wa Tanzania na Ubelgiji ili dereva wa Lissu arejeshwe.
..suala lingine waliohusika kumteka Mo Dewji. Polisi wetu wanadai ni raia wa Afrika Kusini. Sasa mbona Tanzania haiwadai popote na hata kuonyesha sura na majina yao?
🤣🤣🤣🤣 Kwamba serikali iache kuingia mikataba ya kiuchumi na maendeleo kwa faida ya taifa, badala yake iingie mkataba na Ubelgiji sababu tu ya kumkamata dereva wa Lisu?
Anyway kila serikali huwa na mipango yake katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa kuwa serikali hii haijaingia mkataba na ubelgiji ili kufanikisha dereva wa Lisu kukamatwa, basi tusubiri siku ndugu Lisu au chama chake kitaposhinda uraisi kishughilie hilo swala la kuingia mkataba kumkamata dereva wa Lisu.
Sisi Interpol ni kama mbwa wa kitaa. Tukiona mwizi anatoka nduki tunaunga relay bila kujali ameiba wapi. Tunamuunganishia.
Ilikua rahisi kumkamata huyo Mchizi kwa sababu ya Demu wake, Demu ake alikua anaacha alama!
Huyo jamaa alikua ana Pesa, na ndo ambazo Demu alizitumia kumtoa Gerezani!
Sasa hapa Broemfontein, kasababisha Msala kwa Askari jela, 2 wameshakanatwa kwa kukutwa wanaendesha Magari ya bei mbaya tofauti na Mshahara wao!
Ndo hao walikua Zamu siku wanaruhusu Gari la kubeba Taka liingie mpaka Gerezani! (Ndo lililomtorosha Mtuhumiwa)
Wamempiga mtu Kiberiti, wakaunguza Selo, ili mtu mmoja hivi mharifu aweze kutoka.
Ndio maana nimesema kuwa kila serikali huwa na mipango yake katika utekelezaji wa mipango yake. Kama serikali iliyopo madarakani haijaingia mkataba huo na ubelgiji basi subiri siku Lisu na chama chake wakiingia madarakani waingie wao mkataba huo...kuingia mkataba wa kubadilishana wahalifu hakuzuii kuingia mikataba ya uchumi, and vice versa.
..kwa mfano, umedai tuna mkataba wa kubadilishana wahalifu na SA, lakini vilevile inaeleweka kwamba tuna mikataba nao ya masuala ya biashara na uchumi.
..Polisi wetu wamedanganya kwamba wanamhitaji dereva wa Lissu. Wangekuwa wanamhitaji wangeshachukua hatua stahiki kumfikia na kumrudisha Tanzania.
..Bado hujajibu hoja kuhusu waliomteka Mo Dewji. Polisi walidai ni raia wa Afrika Kusini.
Wanawake ni wajinga sana hapo kilichompeleka Kwa huyo mhuni kwanza ana sura na pia ni mpambanaji yaani hiyo Hali ya kujiamini ilimshika demu..Wanawake wanapenda sana ma gangster na mahuni yaliyoshindikana.
Sisi wastaarabu tunateseka sana duniani.
Ndio maana nimesema kuwa kila serikali huwa na mipango yake katika utekelezaji wa mipango yake. Kama serikali iliyopo madarakani haijaingia mkataba huo na ubelgiji basi subiri siku Lisu na chama chake wakiingia madarakani waingie wao mkataba huo.
Pili serikali haioni sababu ya kuendelea kumtafuta mtu alietoroshwa na muathirika mwenyewe wa tukio akishirikiana na viongozi wa chama chake.
Kama kweli angekuwa na lengo la kukamatwa kwa waliohusika na tukio lake basi asingekubali kurubuniwa na viongozi wenzake ili amtoroshe dereva wake.
Mfano mtu anaweza kufunguliwa kesi ya kubaka. Lakini inapofika steji mbakwaji mwenyewe hataki kufika mahakamani kuendelea au kusikiliza kesi yake basi yule mkamatwaji huachiwa kwa kuonekana kwamba huenda lile tukio lilipangwa sio la kweli nk.
Lisu alirubuniwa kumtorosha dereva wake mwenyewe ili asije akagundua kiini cha kweli cha shambulio lile. Kuna msemo mmoja wa kiswahili unaosema kuwa siku zote "kikulacho kinguoni mwako"
Dereva wa Lisu sio mhalifu bali ni mshuhudiaji tu wa tukio. Kwahiyo alitakiwa ahojiwe kuhusiana na lile tukio...hata kama walipanga kupigana risasi sheria inaelekeza wakamatwe.
..Na kama dereva alitoroshwa basi sheria inaelekeza waliomtorosha wakamatwe, na dereva akamatwe.
..Sasa hebu fafanua kwanini hao unaodai wamemtorosha dereva hawatajwi, na hawakamatwi?
..Sijui kwanini mnadanganya, halafu hamna mbinu nzuri za kudanganya.
Hiyo ni kazi ya Interpol, ndiyo wanaotoa descriptions na ndiyo wanao ongoza msako lakini arresting hufanywa na askari wa nchi husika (aliyokamatiwa) hata taarifa hutolewa na nchi ambapo mharifu amekamatiwa.
Wakati mwingine inaweza isiwe interpol lakini ikawa ni joint mission
Kuzunguka kote huko kuna haja gani kusema tu Hongera Polisi wa Tanzania? Interpol ni Taasisi tu ya Kimataifa ambapo Watendaji ni hawa hawa Polisi wetu wa Tanzania au unadhani Interpol ni kitu nje ya PT?
Nchi wanachama wanaki absorb hicho kitengo kuwa kati ya vitengo ndani Police service au Majeshi ya Polisi ya nchi zao zikitumia askari Polisi wa nchi hizo ambao wamekua trained at Interpol levels and ethics na kupewa access ya Interpol activities and files.Nataman sana kujua kazi za interpool na kwamfano hapa tz wanakua na ofisi au?
Ili waifanyie kazi nchi kama hivi africa kusini ilivyotokea manake serikal ya africa kusini imeripoti huko au?
Said mwema tu,alipoteuliwa u IGPBongo kuna ma pimbi wengi sana wanadhani Interpol ni polisi wengine toka ughaibuni, hawajui kua hio Interpol inatokana na hao hao polisi wa bongo ila jina tu. Informations zote zinatokana na polisi wa bongo, na ndio kazi walioifanya ya kuwakamata. Interpol ni jina tu, local police ndio wenye kazi yao kuna kitengo tu hapo..