Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa

We ukisikia INTERPOL unadhani ni wazungu, waamerika, siyo? Ungejua katika nchi wanachama wa Interpol kazi za Interpol zinafanywa na askari police wa nchi husika ambao wapo kitengo cha Interpol.

Yani kiufupi, hatoki askari New Zealand, US, Urusi au UK ndo awe Interpol. Ndani ya police Tanzania kuna kitengo cha Interpol pale makao makuu ya polisi kama vilivyo vitengo vingine Traffic, FFU, GD, STPU, intelligence, CID nk. Hao INTERPOL wa police Tz ndo hufanya kazi na Interpol wengine nchi nyingine huko duniani. Arrest ya mhalifu wa kimataifa hufanywa na yeyote hapa nchini, aweza kuwa local police au hata huyo Interpol police kwa kuwa na yy ni mmoja wa local police ila yupo katika kitengo cha interpol
Umemuelewesha vizuri sana.
 
Hawawezi kutumia passport watu wanaotafutwa kwa maana Nchi zote wanakua na taarifa ukipeleka Passport tuu wanakamata ndio maana wao walitumia gari mpaka Harare kwa kupita kwa kuhonga mpaka wanaingia Tanzania na kutoka...
Na hapo Zimbabwe kulivyokuwa na njaa, naamini hawakupata hata chembe ya shida kuvuka.
 
Hapo kuna tusi mkuu? Mi nimekueleza kwa uhalisia aliuemchinya mama yako au Baba yako, utapendelea afungwe kifungo cha maisha badala ya kunyongwa?
Msifunge akili zenu kisa mko upande ambao hamjafikiwa na hiyo kadhia ya kuuawa kwa mtu wako wa karibu.

Mimi mtu akimuua tu ndugu yangu, hata kabla ya mahakama kuamua nahikikisha namuua. Siwezi kulea ujinga
Umeshawahi ua mtu kabla!? Easier said than done. Kama ni hivyo hata haya magereza yetu yangejaa watu wenye mauaji ya kulipiza kisasi.
 
Hivi unafikiri mambo yanayofanyika duniani polisi wetu hawayajui? Hawafuatilii taarifa habari za nje na kujua wauaji na wafungwa wanaokamatwa na kuoneshwa kwenye vyombo vya habari?

Kesi ya huyo kijana ilikuwa ya wazi na watu wengi waliifatilia. Na hata hilo tukio la jamaa kushtukiwa kwamba ile maiti hauhusiani na huyo mfungwa pia lilitangazwa na msako nchini Afrika kusini ukaanza.

Cha kushangaza baada ya jamaa kugundua kwamba ishajulikana kuwa yeye hakufa kifo cha moto aliamua kutoroka bila kukamatwa na hao wanaowatafuta, pia nchi zote walizopita hawakuweza kugundulika na kukamatwa, ila walipofika kwetu ndo walipoanza kufuatiliwa na askari wetu waliobobea katika nyanja hizo na kufanikiwa kukamatwa.

Ndio maana kuna mchangiaji alisema laiti kama wangefanikiwa kuvuka kuingia Kenya basi mpaka leo wangekuwa bado wanatafutwa na hao interpol wenu. Kwa sababu inaaminika vyema askari wa Kenya wanavyopenda rushwa bila kujali madhara yatokanayo na rushwa.

Kama askari wetu wangekuwa mbumbumbu basi na hapo wangepita salama kama walivyopita huko kwengine.
Acha kuchekesha. Polisi wa Tanzania anajuaje huyu mtu mgeni ni mhalifu anayetafutwa nchi jirani bila kupewa taarifa na huyo jirani mwenyewe!? Acha vioja. Wale wezi tu walioiba Cash In Transit za NBC walikuwa wanazurula tu huku askari wakila rushwa ya pesa zilizoibiwa, askari ahangaike kukamata mhalifu wa SA halafu njaa yake aiache wapi!?
 
1) Ni nchi ngapi alipita kabla ya kufika Tanzania?
2) Je huko alipopita Interpol walikuwa wamelala na kuamka pindi tu alipofika Tanzania?
3) Kwanini interpol hawakufanikisha kukamatwa kwake pindi alipovuka boda kuingia Zimbawe, Zambia na kwengine alipopita?

Nafikiri ifike wakati tukubali tu kwamba askari wetu kwa namna fulani wako vizuri. Ndio maana hata chama cha upinzani Afrika Kusini EFF na nchi nyingi duniani zilitupongeza.

..utaratibu gani umetumika kumkamata Mr.Bester na kumrudisha Afrika Kusini?

..kwanini utaratibu huo haujatumika kumkamata dereva wa Tundu Lissu ambaye Polisi wanadai ametoroka nchini?
 
Statement yake ina ukakasi anaonyesha ana chuki na PT lakini pia anaamini INTERPOL ni Polisi toka sayari nyingine kitu ambacho siyo sawa,INTERPOL kwa nchi yoyote ni walewale Polisi wa nchi husika.
Sawa sawa kama Said Mwema yule mwamba alikua Interpol
 
"Informations zote zinatokana nan polisi wa Bongo" !? Hao Polisi Wa Bongo walijuaje kama hao jamaa ni wahalifu waliotoroka huko SA!?
Umeuliza swali la kipuuzi sana, unadhani polisi uwa wakienda kazini ni kukaa tu na kunywa chai au ??Polisi vituoni kuna kila aina ya informations wanapata kupitia mitandaoni , police magazines/newspapers, police videos za africa na duniani.Na nchi nyingi zilizo jirani au ukanda mmoja pia uwa wanashirikiana katika kupeana infos. Kuna infomations nyingi sana wanazipata wao kwanza kabla duniani wengine hawajapata. Ni hayo tu kujibu hoja yako.
 
Hata jibu lako nalo ni la kipuuzi sana. Maana ume_admit kuwa huwa wanashirikiana kupeana info kitu ambacho nimemuuliza niliyem_quote kuwa polisi wa Tz anajuaje huyu jamaa ni mhalifu kutoka SA bila polisi wa SA kuwapa taarifa. Next time usikurupuke maana huyo niliyem_quote amejaribu kuonesha kuwa polisi wa Tz walifanya tu hiyo kazi bila kupewa taarifa na wenzao wa SA kwa kudai kuwa "informations zote zinatokana na polisi wa Bongo"
 
Hiyo ni kazi ya Interpol, ndiyo wanaotoa descriptions na ndiyo wanao ongoza msako lakini arresting hufanywa na askari wa nchi husika (aliyokamatiwa) hata taarifa hutolewa na nchi ambapo mharifu amekamatiwa.
Wakati mwingine inaweza isiwe interpol lakini ikawa ni joint mission
Nakubaliana na wewe, always katika hili husema ilikua rahisi kumkamata huyo Mharifu kwa sababu ya Mwanamke wake huyo Doctor, alikua anaacha alama kila sehemu, na kwa vile alikua anaonekana hana Hatia.

Miezi kadhaa kabla ya kukamatwa walionekana wakifanya Shopping Sandton Johannesburg...

Kanunua gari ya R 1 million kaenda kuitelekeza Boda ya Zimbabwe....

Baadaye ikasemekana ameonekana Mozambique, so kwa vile Bwana ake alikua Wanted, wakajua tu pale alipo huyo Doctor, basi Bwana ake atakuepo.
 
Na hapo Zimbabwe kulivyokuwa na njaa, naamini hawakupata hata chembe ya shida kuvuka.
Mipaka yote hakuna anaeweza kusumbua ukiwa na pesa mkuu na Agent wale wa magari ndio wanapitisha watu hawa jamaa wamekamatwa washaingia Kenya kwa maana hiyo aliewapeleka ndio kachoma mzigo...
 
Mipaka yote hakuna anaeweza kusumbua ukiwa na pesa mkuu na Agent wale wa magari ndio wanapitisha watu hawa jamaa wamekamatwa washaingia Kenya kwa maana hiyo aliewapeleka ndio kachoma mzigo...
Kuna makosa madogo madogo sana Wahalifu huyafanya na hayo ndiyo husababisha kukamatwa,mfano mdogo tu ni matumizi makubwa ya pesa hasa sehemu za starehe,manjagu huvutiwa sana na kuweka hisia zao kwa wale wanaoenda sehemu za starehe na kuanza kujaza mezani vinywaji vingi wakitumia bila wasiwasi pesa,lakini pia mawasiliano ya simu yanawakamatisha sana Wahalifu.
 
Mtoa mada naomba tusaidiane kuweka ukweli hasa kwenye sensitive mada kama hii, nimefuatilia sana kuhusu issue hii na informations nyingi zinaonyesha kuwa, Mr.Bester hakuua mtu ili kufanikisha escaping yake, inaonekana walinunua maiti, means iliingizwa maiti ndani ya ile prison, kwa hiyo issue ya kuua kwa sasa haipo ila na fugitive huyu he just walk out from prison, SA ni LAZIMA wafuate sheria zetu kuhusu issue hii,nchi yangu is roll over kwa kuwaogopa hasa kwa wale wawili, Dr.Nandipa na Mozambiqueian (hawa ni illegals,wapelekwe mahakamani ,wapigwe faini au jela kama sheria zetu zinavyosema kuhusu illegals),but for Mr.Bester huyu ameshakua convicted kwa murder na raping (real men hawa rape),huyu ame cross line, kwanza ahukumiwe kwa kuwa illegal, then kama tuna mkataba wa kurudishiani fugitives na SA ,ni vema arudishwe haraka SA kwa pingu mwili mzima na mijeledi juu, honestly I hate rapist
Yoh... T Bag was a good guy 😂😂😂.. Ila tu yeye ni last line ya corrupt breed...
 
We ukisikia INTERPOL unadhani ni wazungu, waamerika, siyo? Ungejua katika nchi wanachama wa Interpol kazi za Interpol zinafanywa na askari police wa nchi husika ambao wapo kitengo cha Interpol.

Yani kiufupi, hatoki askari New Zealand, US, Urusi au UK ndo awe Interpol. Ndani ya police Tanzania kuna kitengo cha Interpol pale makao makuu ya polisi kama vilivyo vitengo vingine Traffic, FFU, GD, STPU, intelligence, CID nk. Hao INTERPOL wa police Tz ndo hufanya kazi na Interpol wengine nchi nyingine huko duniani. Arrest ya mhalifu wa kimataifa hufanywa na yeyote hapa nchini, aweza kuwa local police au hata huyo Interpol police kwa kuwa na yy ni mmoja wa local police ila yupo katika kitengo cha interpol
Ili akuelewe mrefushie neno interpol
 
Kuna makosa madogo madogo sana Wahalifu huyafanya na hayo ndiyo husababisha kukamatwa,mfano mdogo tu ni matumizi makubwa ya pesa hasa sehemu za starehe,manjagu huvutiwa sana na kuweka hisia zao kwa wale wanaoenda sehemu za starehe na kuanza kujaza mezani vinywaji vingi wakitumia bila wasiwasi pesa,lakini pia mawasiliano ya simu yanawakamatisha sana Wahalifu.
Sio makosa ni karma inawaumbua inawaweka wazi huyo jamaa kwa damu ambazo hazina hatia alizomwaga SA hawezi kufanya kitu na kikawa sawa lazima adakwe mbona watu wanaenda Nairobi kutoka Arusha wanaenda kununua bidhaa na kurudi bila passport kila siku maana wakikata pass ndogo kila safari inawakata ila kwa kuwa wanajulikana kazi yao maisha yanaenda ila wangekua waharifu kuvuka huo mpaka wa Namanga ungekua mzito...
 
Acha kuchekesha. Polisi wa Tanzania anajuaje huyu mtu mgeni ni mhalifu anayetafutwa nchi jirani bila kupewa taarifa na huyo jirani mwenyewe!? Acha vioja. Wale wezi tu walioiba Cash In Transit za NBC walikuwa wanazurula tu huku askari wakila rushwa ya pesa zilizoibiwa, askari ahangaike kukamata mhalifu wa SA halafu njaa yake aiache wapi!?
Bado unarudi kule kule kwenye hoja yangu, ila tofauti ni kwamba unakataa kukubaliana na kile ninachokiandika kwa sababu zako binafsi.
Nimekwambia haya matukio ya hawa jamaa kutoroka gerezani na ku fake kifo cha mtuhumiwa yalikuwa wazi. Vyombo vingi vya habari viliripoti hizo taarifa. Na kwa vile dunia ya leo ni kijiji kupitia habari mbali mbali hususa news za redioni, magazetini, redioni nk ikawa rahisi watu wengi hata wale ambao sio askari kufuatilia ishu za jamaa.

Swala la polisi wetu kula rushwa sio la wote. Haiwezekani katika taasisi yoyote watu wote wawe na tabia za kufanana. Hata majambazi wanapokwenda kuiba kuna wale ambao hupenda kuuwa baada ya kuiba na kuna wale ambao huwa hawajishughulishi na mauji baada ya kuiba. Unakuta mmoja anataka kuuwa ila mungine anamkataza asiuwe.

Hivyo hivyo kwa jeshi la polisi duniani sio nchini tu, wapo wala rushwa na wapo wasiokula rushwa. Ndio maana hata kwao ingawa alikuwa gerezani chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya ulinzi lkn aliweza kupenyeza chochote na kufanikisha deal lake la kumtorosha, ila hili wewe haujaliona.

Kwahiyo swala la rushwa sio la Tanzania tu peke yake kama unavyojaribu kukazia, bali ni la dunia nzima ndiomaana hata huko alipokuwa anatumikia kifungo chake rushwa ilitembea na jamaa akafanikiwa kutoroshwa katika mazingira tulioyaona ya ku fake kifo chake nk.

Kama unataka na kulazimisha tu sifa ziende kwa hao jamaa zako, mbona hao jamaa zako walishindwa kutumia hiyo njia unayoona waliitumia bongo kumkamata kabla hajavuka mpaka wao?
Imekuaje nchi yenye askari au wapelelezi makini (kwa mujibu wa mawazo yako) ilishindwa kutambua mapema kwamba kile kifo kilikuwa ni changa la macho muda wote aliokaa nchini kwao na mpaka akafanikiwa kutoroka kupitia mipaka yao?

Lkn pia kama ni wao ndio waliofanikisha kukamatwa kwake, kwanini kufanikisha huko kufanyike Tanzania tu na sio Zimbabwe, Msumbiji au nchi nyingine yoyote aliyopita?
 
..utaratibu gani umetumika kumkamata Mr.Bester na kumrudisha Afrika Kusini?

..kwanini utaratibu huo haujatumika kumkamata dereva wa Tundu Lissu ambaye Polisi wanadai ametoroka nchini?
Mr Bester ni mhalifu na tayari alikuwa ashahukumiwa kwa uhalifu wake, hivyo kukamatwa kwake ni halali.

Dereva wa Lisu sio mhalifu, bali ni mtu muhimu alietakiwa ahojiwe ili kumpata mhusika wa tukio hilo la Lisu.

Cha kushangaza mshambuliwaji mwenyewe akiwa ameshikiwa akili na uongozi wa chama chake akaamua kumtorosha dereva huyo ambae angeisaidia polisi kuufahamu ukweli wa shambulio lile.

Polisi sio Mungu ambae ana uwezo wa kujua kila kitu cha sirini na cha dhahiri.
Ili waweze kupata ukweli wa jambo ni lazima kwanza washirikiane na muhusika au shahidi ili kupata taarifa za kuwasaidia kupata chanzo cha jambo husika.
Sasa muhusika unapoamua kumtorosha mtu ambae angeisaidia polisi kupata mwelekeo wa kesi yako, unatarajia nini tena kutoka kwao?

Hapo unakuwa umewakomoa wao au umejikomoa wewe mwenyewe?
 
..basi Polisi hawamhitaji dereva wa Tundu Lissu, au hawachunguzi tukio lile.

..wangekuwa wanamhitaji wangetumia njia na taratibu walizotumia Polisi wa Afrika Kusini kumfikia.

..hata raia wa Afrika Kusini inaodaiwa walimteka Mo Dewji nao walitakiwa kukamatwa kwa kufuata utaratibu uliotumika kwa bwana Bester.
 
SA na TZ wana mikataba ya kiulinzi na usalama, ndio maana ilikuwa rahisi Mr Bester kukamatwa nchi TZ na kukabidhiwa kwa mamlaka ya SA.

Swala la dereva wa Lisu linategemea na nchi aliyopo. Kuna nchi ambazo hatuna mikataba nazo ya ulinzi na usalama. Kwahiyo hata serikali yetu ikijua kuwa dereva huyo yupo katika nchi hizo, kamwe haiwezi kuwa na uwezo wa kuingia katika nchi hizo na kumkamata dereva huyo. Hivyo swala la Lisu na huyu Mr. Bester ni mambo mawili tofauti.
 
Wasauzi bhana wao pana matapeli wamewaibia sana Watanzania wale wanauza matrekta mitandaoni pana mmoja alituma zaidi ya 25Milioni akaambiwa sijui atume hela ya Bima ndio akastuka akanifata kuniuliza utaratibu nikamweleza hicho kitu hakipo hao ni matapeli daah kwa kuwa nilikua karibu na ofisi zao za Interpol nikaenda kuwapa taarifa na jamaa wakawa bado wanatangaza biashara zao wale jamaa wa Interpol wakasema hiki kite do kimefanyika Tanzania kwa hiyo kesi ikafunguliwe Tanzania hawa watu sisi ni kuwakamata na kuwaleta Tanzania nilijua ni kitu kisichowezekana bado wapo wanaendelea kutangaza kwa bei ndogo na Interpol yao ipo na hawafanyi kitu...ila wao wakiguswa wanataka msaada
 
Back
Top Bottom