Thabo Bester maarufu 'Mbakaji wa Facebook' na Dkt. Nandipha Magudumana wakamatiwa Arusha Tanzania. Wafahamu kwa undani wapenzi hawa


Duh!! Dunia ina mambo sana!
 
Demu fight huyo, sio hawa matapeli wetu kila kukicha invoice kwenye majangaaa anakula hivi au hata anakuletea msala
Fighter wapi kilichokuwa kinamzuzua pesa za huyo bester. Huyo bester akiwa gerezani alikuwa anaendesha kampuni ya utapeli akijidai ni investor yuko newyork akishirikiana na huyo demu. Hiyo kampuni ya mambo ya real estate pia imepiga pesa za watu kwa mamilion ya dollar. Pia report zinaonyesha hata kabla ya kutoroka jamaa alikuwa anaingia gerezani na kutoka na hiyo nyumba demu aliyopanga kukaa na jamaa ilikuwa karibu na yalipo makazi ya raisi cyril.
Bester ana pesa nyingi ya upigaji ndio maana demu anamwelewa ila ndio demu mwenyewe kajiharibia maisha. Nilikuwa nasoma comments za wasouth wanasema background ya demu ni kwa kazaliwa ushagoo mjini ni wakuja ndio maana kazuzuka na mtu kama bester hadi kuharibu career yake
 
Demu ni risk taker..
 
Si wamechukua mikopo ya 40m kwa ajili ya kutengeneza movie kali au washanunua masimu ya gharama na uchafu mwingine?
 
Si wamechukua mikopo ya 40m kwa ajili ya kutengeneza movie kali au washanunua masimu ya gharama na uchafu mwingine?
Kwa aina ya akili zao zilivyo, ni wachache tu ndiyo wataitumia hiyo mikopo kwa matumizi sahihi. The rest wataitumia ndivyo isivyo.

Labda wapate semina elekezi kabla ya kukopeshwa.
 
Huyu dada hata kama ni u risk taker sio wa design hii imagine watoto wake maskini watakuwa bila mama
 
Hii inanikumbusha mapenzi ya bonnie &clyde majambazi waliokua wapenzi na wakapendana sana miaka mingi huko Marekani

Huyu dada hata kama ni u risk taker sio wa design hii imagine watoto wake maskini watakuwa bila mama
Halafu now wamevujisha voice note ya bester eti akiwa anamtishia asipofanya anachotaka ana watu nje ya gereza watamshughulikia eti ni vn ya wakati bester akiwa bado hajatoroka.
Yani wanatengeneza mazingira iwe kuwa alikuwa victim.
Hawa watu wanajua what they are doing.
Na ukiachilia mbali hilo, huyu dada alihusika kuiba maiti 3 ambapo moja alidai ni maiti ya baba yake akaenda kuitupa mtoni, na moja aliizika kwake na moja ndo ikatumika kuchomwa moto. Kisha baada ya tukio la moto akaenda kuidai eti maiti ya mumewe ambaye ni bester akaienda kuifanyia mazishi ya kuichoma moto kisha kudai insurance.
Hawa jamaa ni criminals wa kiwango cha movie ya netflix
 
Hata mkeo ukitaka akuelewe usimpelekee moto kama mke,mpelekee kama kahaba chumba na kitanda akione chamoto hutapata usumbufu
 
Graphic yako inasababisha mtu amkumbuke ripota mwingine wa online.

Buni kitu kipya
 
Basi baba msamehe amekosa.
 
Basi baba msamehe amekosa.
Hawa wapuuzi wanaojifanyaga wanaandika KiswaEnglish humu ni wale wameendaga kwenye vishule fulani halafu hawana akili, ndiyo alivyo huyo punguani, we panda juu uone michango yake utaelewa
 
Huyu demu anaonekana kamą ni mgonjwa wa akili
 
Thabo bester ambaye anafahamika kama mbakaji wa Facebook alipata umaarufu South Africa baada ya kukakamatwa kutokana na tukio la kumbaka na kumuua mpenzi wake mwanamitindo maarufu Namfundo

Bester alikuwa na tabia ya kutumia Facebook kuwarubuni wasichana kuwa atawasaidia kuwa wanamitindo WA kimataifa na mwisho kuishia kuwabaka na kuwaua.

Alitoroka jela mwaka 2022 alikokuwa akitumikia kifungo cha maisha baada ya kudanganya kifo chake , ilipita mwaka na dunia ilipatwa na mshituko baada ya kukamatwa April 2023 nchini Tanzania.

Taifa la Tanzania na viunga vyake ilipatwa mshituko kutokana kutowahi kuona tukio kama ilo na wasifu WA bwana thabo ambao unaonyesha ni mtu hatari zaidi kutokana na uharifu aliowatendea waliokumbana Naye na hafai kabisa kwa jamii.

Mwaka 2022 march ililipotiwa bwana bester amekufa Kwa moto kwenye chumba chake akiwa gereza la Mangaung correctional center karibu na Bloemfontein na iliiaminika amekufa mpaka alipodakwa April 2023 nchini Tanzania mkoani Arusha akiwa na mpenzi wake ambaye ni Dr Magudumana .aliyemsaidia kutoroka gerezani Kwa kudanganya kifo chake na ndiye aliyechora mchoro wote Kwa kuingiza mwili WA mtu aliyekufa tayari gerezani na Kisha kuwasha moto chumba na Kisha kuwaaminisha walinzi WA ilo gereza lenye ulinzi mkali kuwa mwili ni wa Thabo.

Ule mwili ulikuja kugundulika sio wa Thabo baada ya vipimo vya DNA kufanyika na harakati za kumsaka ndo zilipoanzia.

Thabo alikuwa ni mtu anayejimudu kifedha Kwa sababu alikuwa na kampuni ya kitapeli ya ujenzi aliyoianzisha Kwa ushirikiano na mpenzi WAke Dr.Nandipa Magudumana ambayo walikuwa wakiwahaidi kuwahudumia watu vifaa vya ujenzi na wakilipia hawahudumii, jamaa alikuwa na utajiri unaokadiliwa $500k za kimarekani na ndizo alizotumia kutekeleza uharifu wake.

Haifaamiki kama nandipha kama ni mke wake halali WA ndoa na taarifa za familia Yao hazifahamiki sana.

Baada ya kukamatwa walisafilishwa kuelekea south Africa ambapo wanaendelea kusikiliza hukumu zao kabla ya kurudisha gerezani Kwa kupigwa miaka ya kutosha kutokana na kuongeza makosa zaidi tofauti na awali.

 
Mimi nahitaji kujua Thabo na Nandipha walikutana vipi hadi kua na mahusiano moto moto wakati Nandipha alikua kaolewa na Thabo alikua gerezani???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…