WanaJF,
Maneno pole na samahani yakitumika katika muda muafaka kwa wanandoa yanachangia kuongeza au kuleta upendo na heshima. Mathalani mume au mke anapofika nyumbani toka kazini au safari,akikaribishwa ndani na kupokewa mizigo kisha akaambiwa pole kwa kazi au safari hufarijika sana kwani huona mume au mke anampenda,anamheshimu na kumjali!
Ni aghalabu sana kwa mume au mke kumpa pole au samahani mwenzake kwa kutomfikisha kileleni au kwa kutowajibika vyema mara baada ya kufanya kile wanandoa wanaruhusiwa kukifanya na ambacho wapenzi hukifanya kwa kuiba pasipo kuwa na kibari maalumu! Mume au mke akimkosea mwenzake anapaswa kuomba msamaha,kwani kutokufanya hivyo kunaondoa upendo na heshima na kusababisha ndoa kuvunjika au wapenzi kuachana!