Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu mada za kujenga kama hizi hawazitaki sijui kwanini?
Watu hudhani neno samahaniiii laonyeshaa inferiority so inakua vigumu kulitumiaa
Ni maneno mazuri sana ila kuna sehem nyingine kwa mwanaume kuomba samahani kwa mkeo hata kama una makosa unaonekana umejishusha sana na wanaweza kusema umetawaliwa na mkeo
Ila kwenye ndoa maneno hayo ni mazuri sana asante na samahani
Watu mada za kujenga kama hizi hawazitaki sijui kwanini?
Msingi mzuri wa ndoa ni kwa wanandoa kuwa na amani wakati wote kutolala na vinyongo na kutonuniana maana iwapo mtanuniana hata raha ya kuwa wanandoa inakuwa haipohe he he afadhali km umeliona hilo, ukwlei
waume ni wagumu sana kuomba msamaha/kutoa pole
wagumu sana, nadhani dada yangu atabahatika kwa kuwa umegundua siri
Msingi mzuri wa ndoa ni kwa wanandoa kuwa na amani wakati wote kutolala na vinyongo na kutonuniana maana iwapo mtanuniana hata raha ya kuwa wanandoa inakuwa haipo
Na sex haipaswi kuwa kiombea samahani yaani mnapeana unyumba kama kuombana samahani ila inatakiwa kuwa raha baina ya wanandoa
Kuombana sahamani ni jambo la msingi pale unapojigundua kuwa umefanya kosa na umeenda nje ya mstari ni muhimu sana
Na hata kwa mwanaume kama amewahi home kumpa mke wake pole nae anajihisi anapendwa na kuna mtu anamjali sio mkeo anakuambia amechoka hata pole hakuna wewe macho kwenye TV unaangalia mechi
shemeji yangu mimi alo muoa dada yangu huwa mkewe akimwambia naumwa kwanza anamuangalia, afu anakaa kimya baadae mkewe akimwambia tena baba fulani me naumwa, utasikia si uende hospital kwani me dokta!
Jibu baya hata lisilokuwa na afya yaani kama ni mgonjwa unamuongezea maumivu mara mbili
Kwani si angemwambia pole na twende nikupeleke kwa Doctor akakuchunguze ni wapi unaumwa