Thamani ya maneno POLE na SAMAHANI katika Mahusiano

Thamani ya maneno POLE na SAMAHANI katika Mahusiano

mi wangu ana jeurii moja matata......hata akosee haombi ng'o...dawa yake ipo jikoni

kuwa makini na dawa yako, kuna nyingne unaweza mpa na matokeo yake yakawa hasi zaidi ukataman bora usingempa hiyo dawa
 
madharau yasio na kichwa wala miguu tena kuna hiyo defense mechanism mtu anakosa afu anawahi kununa mxyuuuu hapo anajiwekea tahadhari asiulizwe uboya tu, umekosa sema sorry haibadili uanaume!!!

Mimi nikigundua nimekosa ninachofanya ni kuamka asubuhi sana na kujiandalia vitu vyangu mwenyewe bila kumuamsha majeruhi wangu naenda zangu job kimyakimya nikiwa nimeacha hela zaidi kuliko kawaida kwenye dressing
table,siku hiyo ntapiga sana simu kujua mambo yanaendaje hapo home au kazini kwake kama atakua kazini,ile nikitoka tu kazini moja kwa moja uchumi supermarket au mlimani city kuna vitu ambavyo ananipmbaga nimchikulie lakini najifanyaga nipo busy ila kwa siku hiyo namchukulia in excess,baada ya hapo moja kwa moja home tena nikiwa sober cpitii maeneo yetu yale!!!kama kuna mechi ya arsenal siku hiyo naangalizia yumbani sio jackeys tena.....basi hapo utamwona tu anacheka na kusema "we unajifanya mjanja sana,ukirudia teenaa...."..wanawake bwana!!!
 
Inabidi mzoee tu na kumsoma mwanaume wako kuwa yeye namna ya kuomba msamaha kwake ikoje ila kupiga magoti au kusema nisamehe ni ngumu kumesa
 
Next........................................????

Jeuri, kiburi, dharau, Ego and the likes..I think.

Baada ya hapo unampa muda wa kushusha pressure...ila isiposhuka unampandia na kumuonesha kuwa wewe ndiye baba mwenye nyumba..... Umeelewa?

Kuna kabila fulani wanatumia msemo kuwa, "Baba hashindwi kesi ...dhidi ya mke au mwanae"...Na ikitokea baba akashindwa basi hukumu inasomeka kuwa hakuna aliyeshindwa!

Ni somo dogo tu ila muhimu sana kuwaonesha kuwa "Men are not big boys"!!!!
 
umeona akijishusha sana ataonekana bushoke

Hivi mnajua kwa nini watu wa Malawi walichukia sana pale rais wao wa awamu iliyopita mwanamama Joyce Banda alipomsalimia Malkia wa Uingereza kwa kupiga magoti?

In short, ukiwa kichwa lazima uhakikishe kuwa unatetea heshima na hadhi ya kichwa hicho kwa gharama yoyote!
 
madharau yasio na kichwa wala miguu tena kuna hiyo defense mechanism mtu anakosa afu anawahi kununa mxyuuuu hapo anajiwekea tahadhari asiulizwe uboya tu, umekosa sema sorry haibadili uanaume!!!

na nikikosa fedha je inabadili?
 
Awe mpole niongee lugha zote nimalize!

Inategemea na kosa alilofanya pia,kama ni dogo mie nimeamua tu kulikuza basi awe tu mpole ila kama ni kubwa basi aombe radhi kwa namna yoyote inayofaa.

Samahani kila Mara akosapo zinanikera,zinapoteza maana na zinamshushia hadhi yake kwangu.
 
Umenena vema mamito...
 
Back
Top Bottom