Poleni wadau wa MMU,
Ukweli neno samahani ni dogo sana ila ni gumu sana kulitamka kwa mwenzio kwa kuhisi labda atakuzarau au kujihisi heshima yako itapungua,neno hili huwa ni gumu sana kulitamka kwa watu wazima hususani baba, mama au mtu yeyote alie kuzidi umri sijui kwanini huwa gumu na wakati anamakosa kweli.
Narudi kwa upande wa wapenzi,huku nako pia ni ligumu kulitumia neno hili hususani sisi wanaume,ila sio wote hata wenzetu nao pia huwa wagumu kuomba msamaha kama kakosa tena kama kashakuchoka ndo utajuta kabisa kumfamu.
Mfano mzuri ni rafiki yangu na mpenzi wake wamechuniana kisa tu msichana kashindwa kumuomba mshikaji msamaha,kosa lenyewe liko hivi jamaa kampigia msichana simu mida ya saa saba hivi, kumjulia hali lakini simu ilikuwa inaita pasipo kupokewa.
Akajaribu mara kibao lakini holla,ikabidi jamaa amsikilizie kwa sababu atakuta missed call lakini msichana kawa kimya,akampigia tena saa kumi nayo kimya,ikabidi jamaa akae kimya maybe ipo chaji cha ajabu mpaka siku inaisha msichana hakumpigia simu mshikaji.
Kesho yake jamaa akampigia simu saa nne asubuhi ikapokelewa ikabidi amuulize vizuri tu,cha ajabu tena eti msichana anamjibu simpo tu mshikaji ,eti hakuwa na vocha,jamaa akamwambia basi si ungenitumia hata tafazali nipigie, msichana kawaka amkamjibu hivi,nimekwambia sikuwa na vocha.
Hunielewi jamaaa akashangaa sana iweje msichana awe ndiyo mkali wa kumkaripia mchizi ili hali.yeye ndo mwenye makosa ikabidi jamaa amulize mbona unanijibu hivo,msichana akamwambia ulitaka nikujibu vipi.
Mchizi hoi akawa mpole akamwambia basi siku ukiwa na vocha nitafute,msichana akasema sitakuwa nazo mpaka mwakani.
Sasa wadau hapo nani mwenye makosa,maana mpaka sasa hivi watu hawaongei kila mtu anajua yeye yuko sahihi.Je jamaa aendelee kuwa kimya au amtafute na akimtafuta aanzeje kuomba msamaha.
Karibuni.