Mara nyingi sana katika maisha yetu tumejikuta tunafanya makosa ,makosa haya mengine tumeyafanya kwa kujua au kutojua lkn mwishon tunakuja kugundua tumefanya dhambi ,tumemkosea mpenzi ,wazazi ,marafiki ,ndugu jamaa !!.
Matokeo ya makosa haya hupelekea tuishi huku mioyoni mwetu tukijuta sana , wakati fulan ,lilikua nikosa ,umelifanya siri ,kwamiaka mingi , Moyo wako unauma sana ,unawaza Ukiri mbele ya ulomkosea kisha umwombe msamaha ili uwe na Amani ya Moyo wako !!.
LAKINI ,kabla ya kukiri kosa lako , umefikiria hatima yakukiri kwako itakuaje ??. Je utakapomuambia ukweli , Unahisi atakusamehe ?? Unahisi atakukubali na kukuamin kama awali ??. Je unahisi Jamii itakuamini tena nakukuona unayefaaa ??.
Ulikua unatafuta nani umuambie ,naakuelewe zaidi na bado akakuamini na akakupa Amani ??.
Kusema ukweli ,,baadhi ya ukweli utakaoukiri mbele ya MTU/watu ulowakosea Mwisho wake umekua kuzidisha chuki naroho yakisasi ,MTU anakusamehe lkn moyon anangoja siku ujisahau nayeye akupe pigo lakukuumiza !!.
Aiseeee nipende kusema ,, baadhi ya makosa kabla hujaliongea kwa wahusika ,Hakikisha unaliongea kwanza na Mungu !!.
Baadhi ya makosa yanapaswa umlilie Mungu wako tuuuuu Akusameheeee nayeye ndo atakupa furaha na amani ya Moyo wako .
Jifungie ndani pekee yako ,, piga magoti ,,ongea na Nafsi yako kwanzaaaa zungumza na nafsi yako ,, sononeka ,,umia na nafsi yako kwanza ,, alafu sasa Mwambie Mungu *Nisamehe na Unipe Amani Moyoni Mwangu*.
Umetoa mimba kadhaa ,,ukiri kwawatu nani atakusamehe na kukuamin ???.ongea na Mungu wako!!
Mkeo anakupenda sana , lkn umemsaliti , Ongea na Mungu wako !!
Umeingia ktk mahusiano Mapya , lkn huko nyuma umewahi kua changudoa na unampenda sana,, Ongea na Mungu wako !!.
Kwann Uongee na Mungu ? Kwasababu yeye atakupa Amani moyon na furaha nahivyo ATAKUEPUSHIA Athari ambazo Wenda zingetokea pale ambavyo ungesema!!.
Sio makosa yote yanaitaji Msamaha wawazi
KUNA WAKATI NILAZIMA UKWELI ,UUJUE WW NA MUNGU WAKO ,ILI KUZUIA ATHARI AMBAZO WENDA ZIKAATHIRI MAISHA YAKO NAJAMII YAKOO MILELE !!.