Thamani ya pesa yetu inazidi kuporomoka. Shida ni nini?

 
Mabenki kwasasa yameweka limit transfer za USD, wengine $5k , $10k per day! USD itapaa zaidi soon!
 
Huu ni uongo wa Hali juu December 2015 dollar ilikua 1169? [emoji3061]
 
Shida ni ileile siasa za walamba asali.

Taifa litapona siku watanzania wenyewe watakapoamka kutoka kwenye usingizi wa pono na kudai nchi yao iliyotekwa na familia fulani fulani.
 
Unamlisha jirani ambaye yeye aneacha kulima maana Kilimo hakiwalipi wakulima wake. Hivyo wakulima wakaamua kuwa wafanyabiashara wa nafaka na madalali wakichukua mazao kwako na kuongeza thamani na kuuza ndani na nje ya soko Lao. Halafu wewe eti unavuka mabara kwenda kununua nafaka nje. Hapa sielewi kama tuna watu huko wizarani Wana akili ya mahesabu au wenye akili waliajiriwa sekta binafsi? Inauma Sana Mkuu.
 
Kwani maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yameruhusiwa tena?
Ndiyo ila baadhi mitaji yao ilifilisiwa na yule mfilisi aliyetutoka na inatafutwa ilipowekwa na yule mfilisi bado haionekani. 🤣🤣🤣. Kua uyaone
 
Mabenki kwasasa yameweka limit transfer za USD, wengine $5k , $10k per day! USD itapaa zaidi soon!
Kuna ukata mkubwa Sana wa dola na dd ni kubwa i.e supply<demand ikiashiria excess demand maana biashara zinafunguka hivyo lazima bei ya dola ipande Sana. Impact ya suppression ya Uchumi 2015-2020 itatula maeneo mengi mno ikiwemo foreign exchange.
 
Hiyo rate kanunue kwenye tovuti,huku mtaani Dola 1 inanunuliwa kwa 2425 kama hautaki hauipati na utafeli.
 
Sukari kilo @3,500
Mchele kilo @3,800
Unga kilo @2,000
Nyama kilo@10,000
Mafuta Lita 1@3,000
Maharage kilo 3,800

Nani kama Mama!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…