Mwenyezi Mungu huwa ana makusudi kwa kila jambo linalokuja kwa wanadamu, zuri au baya! Imani yangu inanituma kuwa alimleta Kikwete ili Tanzania ipate ukombozi kamili toka kwa CCM (wakoloni weusi). Hizi ndo sababu zangu: -
1. Baadaya Kikwete kushindwa kura za maoni 2005 alianzisha mtandao wa kusaka urais tangia hapo. Mtandao ambao ndio chanzo cha makundi ya CCM na ambayo hayawezi kuisha ndani ya chama hicho. (Kikwete muasisi wa makundi)
2. Kikwete na mtandao wake walinunua wahariri wa vyombo vya habari ili kumpamba Kikwete na kuwachafua washindani wake. (Rejea kauli za Sumaye) Walipoingia madarakani na seriksli yao ikawa regerege wakawageuka waandishi wanaowakosoa na kufungia vyombo vyao. (Mwanahalisi, Kulikoni, Mwananchi, Mtanzania nk) Ccm ikatengeneza uadui na waandishi.
3. Kikwete katika uchaguzi uliopita baada ya kukabwa vilivyo na Dr Slaa, washauri wake na chama chake wakamshauri kuelekeza siasa misikitini kujaribu kuokoa jahazi. Yanayotokea baada ya hapo kila mmoja anaona. (Kikwete muasisi wa udini) Wenye macho wanaweza kuona CCM itakavyoangushwa na udini.
4. Kauli yake ya maisha bora iliwapa matumaini watanzania kuwa inawezekana wamepata mkombozi mpya. Matumaini yoa yanayeyuka kama barafu na sasa tafiti zinaonyesha watanzania hawana imani na serikali, Kikwete na CCM.
Yote haya yakiweza kufanyiwa kazi na upinzani sioni CCM ikiokoka. Ni mpango wa Mungu Kikwete kusababisha ukombozi?