Thanx God....17 yrs...Still getting stronger

Miaka ikienda mnakuwa kama mmekutana jana
Ya kweli haya? au wewe tu bahati yako? maana tunawaona wanafamilia wengi mtaani miaka hiyo wababa hawashikiki, hongera tena na tena
 
Shantel mdogo wangu kila mtu na bahati yake katika hili swala, na sio hiyo mikiki wengine hatupitii, tunapitia sana tu ila tunakuwa wagumu tu
unajua bila kupitia hayo nahisi unakuwa sio imara sana
 
Hi marafiki, wanajamii wenzangu, siwezi amini miaka inavokatika, nikiangalia naona kama ni juzijuzi tu, sijui wakati umeenda wapi, all in all namshukuru Mwenyezi Mungu sana sana kwani leo ni anniversary yetu na my hubby, namshukuru Mume wangu pia kwa kunichagua mimi kuwa mke wake, nawashukuru pia watoto wangu kwa kunipa sababu nyingine ya kuishi, nawapenda sana hawa watu walio katika maisha yangu. Our anniversary is a time to look back at the good times and to look ahead to live our dream...below is my story..

Nikirudi nyuma kabisa nakumbuka nikiwa msichana mdogo na kabegi kangu ka shule nakutana na huyu mkaka aliyehamia mtaani kwetu, na kupanga chumba nyumba ya jirani baada ya kumaliza masomo ya chuo, utani uleeee wa kizamani ukaanza, oooh mchumba, oooh hakuna shule hapo, oooh sijui nini badae nikaja kugundua huyu jamaa ananizimia, mwisho wa siku akaniambia ukweli wake, niliogopa sana...ukizingatia alikuwa mkubwa kuliko mimi.

Moyoni nilikuwa na mawazo sana hasa wasichana wengi wanajua kipindi ambapo wanafanya maamuzi ya kuwa na BF wa kwanza kabisa, nikammwaga,nilihisi bado wakati na siwezi kuwa na uhusiano na mkaka mkubwa,miezi ikaendelea, mara tunakutana dukani, mara kwenye chips mtaani.....miezi inaendelea...hatimae mwaka....jamaa kawa stable kidogo kazini anataka kuhamia chumba kingine eneo lingine kabisa, hapo ndio kimbembe kilianza

Jioni moja kaniita kanambia anahama keshapata chumba mahala pengine, na alipohama ndipo nilianza ku mmiss mpaka nikaumwa kabisa, kumbuka kipindi cha miaka ya tisini na hivi simu ilikuwa ni ishu, mawasiliano ni mpaka umtafute mtu, na wakunitafuta ni yeye coz mie alipohama nilijifanya sitaki kujua anahamia wapi,muda ukapita ila jamaa hakukata tamaa, akarudi siku moja mtaani nilipomwona mpaka machozi yalinitoka....... hapa ndio ule msemo wa "huwezi jua thamani ya kitu mpaka ukipoteze ndipo ulifika mahala pake"........kiss ya kwanza bonde la mchicha loooooooooo.....jamaa hakuamini... baada ya muda mfupi uhusiano ukaanza...

"Love for me is to trust yourself that your in love....thats what happened to me, pamoja nilikuwa mdogo ila nilijua kabisa huyu mwanaume nimempenda kwa dhati,love is trusting your partner enough to tell them everything about yourself,ukijumlisha na yale yooote you might be ashamed of, Love is feeling comfortable and safe with someone........thats what i felt when im around him Basi rafiki zangu, maisha yakaenda nikamaliza shule yaaani O level nikaolewa mwenzenu loooo.... yaliyofata kutokea hapo ni rahaaaaaaaaaa, uchungu ......rahaaaaaaaaaaaaa uchungu....... na sasa ndio raha kamili kila mahali....ndoa zina changamoto nyingi sana ni namna unavoichukulia wewe ndio itakuwa hivohivo, ndoa ni tamu asikwambie mtu, hata kama ni ndoano, ila ndoano yake ni ya aina ya pekee...

Nampenda sana Mume wangu mpenzi, Naendelea kuomba Mungu atupe afya mie na familia yangu, kwa maisha yetu yote, atulinde na mabaya yote, azidi kutupa nguvu na amani ndani ya ndoa yetu.......Ndoa yetu na iheshimiwe na watu wote,,,,AMIN

Herzlichen Glückwunsch . . . .!!!
Ich gratuliere . . . . zur Hochzeit!

. . . Alles Gute...
 
Congratulations Gaga,17 yrs is a lifetime,wengine hawajavuka hata five month's and for us ambao bado we have no clue what it's like to live with someone for that long
 
Herzlichen Glückwunsch . . . .!!!
Ich gratuliere . . . . zur Hochzeit!

. . . Alles Gute...
CPU huu ni uchoyo bwana, naomba nitafasirie
 
Congratulations Gaga,17 yrs is a lifetime,wengine hawajavuka hata five month's and for us ambao bado we have no clue what it's like to live with someone for that long
Huwezi jua mpaka uingie bushloiz, ahsante sanasana
 
Hongera sana Gaga msalimie sana Shemeji yetu na watoto.
nimeipenda hii post yako mungu awalinde awaitie nguvu muendelee kuwa imara ,..till end of time.
Nitakuja kuwatembelea mpenzi ....
 
Congratulations Gaga nataka next time ukiandika hapa useme "Thanx God.......50 yrs Still Getting Stronger"
 
Aisee hili yuziful sredi lilinipitaje hivihivi?

yaani Gaga hata kuniPM mshkaji wangu?

Hongera sana asee. Hongera sana mtu wangu....

Mi nshakata kumi. Siku nikifikisha 15 kama niko hai, wallah patakuwa hapatoshi.
 
Kila la kheri dada kaza uzi, shikilia ulichoshika ndicho chako ati.
 
Aisee hili yuziful sredi lilinipitaje hivihivi?

yaani Gaga hata kuniPM mshkaji wangu?

Hongera sana asee. Hongera sana mtu wangu....

Mi nshakata kumi. Siku nikifikisha 15 kama niko hai, wallah patakuwa hapatoshi.
Ahsante babu, nili ku promise lakini, unakumbuka?
wewe sijui ulipotelea wapi, na kuna watu walikuwa wanakutafuta sana uwajibu maswali
yao kwenye thread ya ulikuwa wapi siku zote......ukaingia mitini
 
Hongera sana Gaga msalimie sana Shemeji yetu na watoto.
nimeipenda hii post yako mungu awalinde awaitie nguvu muendelee kuwa imara ,..till end of time.
Nitakuja kuwatembelea mpenzi ....
Nitamsalimia aisee, karibu sana kwetu, wasalimie na wewe huko kwenu
 
Thankd Gaga for sharing thsi with us and Happy Anniversary, Sijui bado uko Hanemuni? LOL Keep going
 
Hi marafiki, wanajamii wenzangu, siwezi amini miaka inavokatika, nikiangalia naona kama ni juzijuzi tu, sijui wakati umeenda wapi, all in all namshukuru Mwenyezi Mungu sana sana kwani leo ni anniversary yetu na my hubby, namshukuru Mume wangu pia kwa kunichagua mimi kuwa mke wake, nawashukuru pia watoto wangu kwa kunipa sababu nyingine ya kuishi, nawapenda sana hawa watu walio katika maisha yangu. Our anniversary is a time to look back at the good times and to look ahead to live our dream...below is my story..

Nikirudi nyuma kabisa nakumbuka nikiwa msichana mdogo na kabegi kangu ka shule nakutana na huyu mkaka aliyehamia mtaani kwetu, na kupanga chumba nyumba ya jirani baada ya kumaliza masomo ya chuo, utani uleeee wa kizamani ukaanza, oooh mchumba, oooh hakuna shule hapo, oooh sijui nini badae nikaja kugundua huyu jamaa ananizimia, mwisho wa siku akaniambia ukweli wake, niliogopa sana...ukizingatia alikuwa mkubwa kuliko mimi.

Moyoni nilikuwa na mawazo sana hasa wasichana wengi wanajua kipindi ambapo wanafanya maamuzi ya kuwa na BF wa kwanza kabisa, nikammwaga,nilihisi bado wakati na siwezi kuwa na uhusiano na mkaka mkubwa,miezi ikaendelea, mara tunakutana dukani, mara kwenye chips mtaani.....miezi inaendelea...hatimae mwaka....jamaa kawa stable kidogo kazini anataka kuhamia chumba kingine eneo lingine kabisa, hapo ndio kimbembe kilianza

Jioni moja kaniita kanambia anahama keshapata chumba mahala pengine, na alipohama ndipo nilianza ku mmiss mpaka nikaumwa kabisa, kumbuka kipindi cha miaka ya tisini na hivi simu ilikuwa ni ishu, mawasiliano ni mpaka umtafute mtu, na wakunitafuta ni yeye coz mie alipohama nilijifanya sitaki kujua anahamia wapi,muda ukapita ila jamaa hakukata tamaa, akarudi siku moja mtaani nilipomwona mpaka machozi yalinitoka....... hapa ndio ule msemo wa "huwezi jua thamani ya kitu mpaka ukipoteze ndipo ulifika mahala pake"........kiss ya kwanza bonde la mchicha loooooooooo.....jamaa hakuamini... baada ya muda mfupi uhusiano ukaanza...

"Love for me is to trust yourself that your in love....thats what happened to me, pamoja nilikuwa mdogo ila nilijua kabisa huyu mwanaume nimempenda kwa dhati,love is trusting your partner enough to tell them everything about yourself,ukijumlisha na yale yooote you might be ashamed of, Love is feeling comfortable and safe with someone........thats what i felt when im around him Basi rafiki zangu, maisha yakaenda nikamaliza shule yaaani O level nikaolewa mwenzenu loooo.... yaliyofata kutokea hapo ni rahaaaaaaaaaa, uchungu ......rahaaaaaaaaaaaaa uchungu....... na sasa ndio raha kamili kila mahali....ndoa zina changamoto nyingi sana ni namna unavoichukulia wewe ndio itakuwa hivohivo, ndoa ni tamu asikwambie mtu, hata kama ni ndoano, ila ndoano yake ni ya aina ya pekee...

Nampenda sana Mume wangu mpenzi, Naendelea kuomba Mungu atupe afya mie na familia yangu, kwa maisha yetu yote, atulinde na mabaya yote, azidi kutupa nguvu na amani ndani ya ndoa yetu.......Ndoa yetu na iheshimiwe na watu wote,,,,AMIN

Asante kwa hadith nzuri, inapendeza. Hapo penye rangi nyekundu na maandishi makubwa ndio pamenigusa zaidi. Watu wengi hukumbwa na hilo, mfano mtu anaweza kumuacha mkewe ama mumewe kwa vishawishi au kwa kutomuona kuwa hapendezi. Kisha baadae aliyeachwa akipata mwengine, yule mume ama mke wa kwanza huanza kujuta kwa alimuacha na wakati mwengine hufikia hatua ya kuleta vurugu. Hii yote ni kwa kuwa aliyeachwa amepanda thamani baada kuachika ama kupotezwa na mume ama mke wa kwanza.
 
Utafika tu ila tuombee sisi ambao hata hatujaanza hiyo safari by the way honeymoon imeisha au bado lol!!!
Vijana wa siku hizi mnawezekana? unataka uwe na nyumba na gari ndio uoe, utajuaje sijui mtu kafata penzi, nyumba au gari, nawaombea sana aisee....honeymoon was mmmmmh yamy yamy na libonge la zawadi
 
Back
Top Bottom