Tanesco is a state owned company, not an independent or private company, which means it can easily secure financial guarantees from Serikali. Tatizo ni kuwa bado viongozi wetu wanaodai hawajui kwa nini Tanzania ni masikini hawajaweza kuoanisha umeme na uzalishaji mali ambao ndio msingi wa mapato.
Chukulia mfano kama umeme ukisambazwa nchi nzima na si mijini pekee, kutaleta msukumo mpya wa uzalishaji mali na huku mashambani, ubora wa mazao na hata uhifadhi utafanyika. Mashambani watu wataweza kufungua viwanda vidogovidogo vya kusindika na kuhifadhi vyakula, nalo litasaidia vipato vyao na kuondokana na mazoea ya kulima mazao ili yauzwe kwa Ushirika an sehemu nyingine. Basically we will be pushing processing industry into rural areas for food and cash crops. Sasa kwa hawa mabingwa wa Kilimo Kwanza, hawaoni kuwa tutajiongezea faida kubwa na ku-retain true value ya mazao badala ya sisi kupewa compensation through pricing or merely 25% of the true value of zao?
Expansion hii ya rural areas, itasababisha nako mijini kuwe na Domino effect, tutalazimika kuwa na ubunifu na kuanza kujituma zaidi ili kuzalisha zaidi.
Lakini nikirudi nyuma kwanza, kuna sekta kadhaa au huduma za jamii ambazo zitanufaika sana kwa umeme kupatikana kila sehemu. Sekta ya elimu, ambapo wanafunzi watakuwa na uwezo wa kupanua uwezo wao kielimu kupitia mitandao (si tunasambaza fibreoptics za SEACOM nchi nzima? je zitatumia kuni?) na vitendea kazi vingine. KUkua na kupanuka kwa wigo wa elimu ni msingi mkuu wa kuleta ushindani na ubunifu katika kila sekta.
Huko majumbani, nako umeme utasaidia kila mtu kwa mengi. Nadharia kuwa umeme ni kitu cha anasa na si cha ulazima ni lazima kifutwe kwa nguvu zote.
Nikirudi kwenye expansion ya umeme nchi nzima, uzalishaji utaongezeka maradufu na kutoa ajira maradufu na kuongeza pato la Taifa maradufu, it is as simple as that.
Now, why is CCM and its government not taking this opportunity to take Tanzania to a next level of development? jibu sina zaidi ya kuwa ni ubinafsi na upeo mfupi.
Hizi 100mw ni short terms projects ambazo miaka hii 25 ambayo tumekuwa tukizitumia, tungekkwisha maliza ujenzi wa project kubwa ya long term na yenye uwezo mkubwa kama Steigler Gorge Ruhidji au wind and solar farms kule Dodoma na Singida.
Time is money and time is not on our side. Serikali na Wananchi ni lazima wang'amue hili na tatizo hili la Umeme si la kisiasa pekee, au chama kimoja bali ni la nchi nzima.
Kamwe hatutaweza kuwa Taifa huru linalojitegemea kama dhana hii potofu hatutaondokana nayo. Na hata tukiweka hizo station nyingine, makosa tuliyoyafanya miaka 25 iliyopita ya kuzembea kufanya maintenance Mtera, Kidatu na power plants nyingine yasirudiwe.
Kama Serikali ina ni a ya kweli kutatua tatizo la umeme, jambo hilo si gumu, kama waliweza kununua VX kwa kila Mbunge na Waziri, kwa nini washindwe kuhakikisha umeme ni wa uhakika?