Kama unanisema mimi umekosea sana, mimi ni shabiki mkubwa wa michezo na kwa sasa Basketball. Niliwahi kuangalia soka wakati timu ya England ikipambana na Brazil mwaka 1970 (je ulikuwa umezaliwa?) Alikuwepo mchezaji moja wa Brazil anaitwa Pele au mchawi wa soka ila jina lake halisi lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, na kweli alikuwa mchawi wa soka. Wakati huo England inao wachezaji hatari kama akina Bobby Moore na golikipa machachari akiitwa Gordon Banks.
England walijua wazi kabisa kuwa Pele hawezekani na hivyo wakaamua kwamba kila mchezaji anayekutana na Pele ahakikishe kwamba kimoja tu kinapita...ama mchawi au mpira. Siku hiyo England walivunja rekodi kwa kumkata Pele madaluga hadi ilibidi Pele atolewe uwanjani. Pamoja na kufanyiwa vituko vyote hivyo, heshima ya Pele ilibaki pale pale kama mchawi wa soka. Hivyo hivyo ukiona vituko Curry anafanyiwa uwanjani awe na mpira au hana lakini pamoja na hayo Curry naye kaandika historia!