THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal

THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal

Screenshot (138).png
Screenshot (90).png



____NO_____4.

Eduardo alikuwa ameketi ndani ya ndege akisubiri ndege ianze safari ya kuelekea California-jijini San Fransisco
Hakuweza kujutia kitendo chake cha kuweza kuacha internship siku ya kwanza tu ilikusudi kuendelea na kaz yake ya kutafta wawekezaji na watu wa kutangaza kwenye web site ya thefacebook, aliamua kuacha internship ili aweze kuwekeza nguvu kwenye thefacebook kwa kuwa alitaka kuwa mfanyabiashara halisi hivyo katika siku zote ambazo amekuwa New York amekuwa akifanya kazi ya kuzunguka kwa watangazaji na wawekezaji na kufanya nao mikutano kadhaa ambapo alipata dili na kampuni iliyoitwa Y2M na kupata ahadi kubwa kutoka kwa makampuni mengine mawili
Alikuwa na hofu ya kutaka kufahamu kuwa ni kipi kilikuwa kinaendelea California kwa Mark na team yake, ni maendeleo yapi wameyafanya na kwa nini walikuwa hawampigii tena simu mara kwa mara

Aliona akifika California vitu flani vitarudi kuwa sawa thefacebook, yeye,Mark na timu yake watafanya baadhi ya vitu, kazi flani zitafanyika na kisha kila kitu kitakuwa sawa
Tena usiku huo wa kuwasili ulikuwa unaanza na shamrashamra, Mark alikuwa amemwambia kuwa kulikuwa na party ambayo wamepata kualikwa kupitia Sean Parker, ilikuwa ni sherehe kama ya wajasiriamali ambayo wangepata fursa ya kuonana na wawekezaji, watu wakubwa wa Silicon Valley pamoja na watu maarufu wa mtandao. Mark alimwambia Eduardo kuwa Sean amekuwa akiwapeleka kwenye party nyingi za aina hiyo tangu walipofika California, kwamba amejionea vitu vikubwa ambavyo Silico Valley vinaweza kuzaa matunda,kwamba wamepata kwenda sehemu mbalimbali zenye hadhi ikiwemo kuhudhuria party za hali ya juu jijini Los Angeles. Sean Parker alimfahamu kila mtu na kila mtu alimfahamu Sean hivyo kupitia yeye kila mtu alipata kumfahamu Mark, thefacebook haikuwa kitu kikubwa pale Silicon Valley lakini kidogokidogo ilikuwa inaanza kuwa gumzo la mji na ilionekana kama kila mtu alitaka kukutana na mtoto genius alietengeneza mtandao uliokuwa unazungumziwa sana.

Eduardo yeye alikuwa na shauku zaidi ya kufahamu maendeleo waliyofikia Mark na team yake, kwani ilikuwa kuwa kila alipompigia Mark simu angeskia kuhusu party au dinner ambayo ameikosa kwa yeye kuwa NewYork.
Eduardo ambacho hakukipenda ni kuwa, Mark alikuwa ni Mark, ni ngumu kumsoma hasa kwa kuongea nae kwenye simu, wakati mwingine ilikuwa ni kama kuzungumza na kompyuta, ataskia alichokisema, atakitafakari kisha atajibu kama atahisi jibu lilikuwa la lazima na wakati mwingine hajibu chochote kabisa. Hata Eduardo alipomwambia kuhusu dili na ahadi alizopata, Mark hakuonesha dalili yoyote ile ya kwamba amefurahi labda hata amestaajabu kwamba wataaenda kupata hela kwa kuzingatia kuwa kila siku the facebook ilikuwa inakuwa na ndivyo ambavyo matatizo yanazidi kuongezeka, walikuwa wanaenda kuhitaji pesa nyingi muda sio mrefu kwani bado walikuwa wakitumia fedha ambazo Eduardo aliweka wakati alipofungua akaunti benki
kwa kuongezeka kwa watu na kukua kwa thefacebook server zitahitajika zaidi na hawatahitaji interns wawili tena bali watatakiwa kuajili wafanyakazi halisi, kupata ofisi halisi na kuwa na wanasheria halisi wa kampuni, pamoja na vitu vingine vinavyohitajika.
Hivyo vyote ndo vitu ambavyo Eduardo alikuwa amejiandaa kujadili na Mark , kujadili akiwa peke yake kwani aliona kuwa Sean Parker hakustahili kuviskia, ni vitu ambavyo vilimhusu Mark na si mgeni wa Mark ,haijalishi alikuwa amewapeleka kwenye Party ngapi

Eduardo aliwasili San Fransisco baada ya ndege kutua, alimfuata Mark kuelekea mahali alipopark gari lake, gari ambalo lilkuwa ni baya lililochakaa na kuwa kama masalia ya vyuma ambapo hata halikutumia funguo kuwasha engine bali ilikuwa ni kusugua nyaya ndipo kuweza kuwasha engine, uchakavu wake na ubaya wake haikuhitajika hofu ya kwamba mtu angeweza kuliiba.
Eduardo aliweka mizigo yake na kuingia ndani ya gari hilo ambalo Dustin ndie aliekuwa akiendesha, Eduardo aliangaza na hakuweza kumwona Sean Parker popote pale, Mark alimwambia kuwa Sean ametangulia kwenye part na hivyo amewatunzia wao nafasi ya VIP na kuacha majina yao mlangoni kwa mlinzi
Eduardo aliona kuwa huo ndo ulikuwa ni muda sahihi wa kuzungumza na Mark huku wakiondoka pale uwanja wa ndege
Kama ilivyo kawaida ya uhusiano wao, ni Eduardo aliweza kuongea huku Mark akimsikiliza akiwa kimya, Edurdo alimwelezea kwa upana kuhusu mambo yote aliyoyafanya, dili na ahadi alizozipata, aliongea pia kuhusu mipango mingine ya kuwawezesha kupata fedha na mawazo ya jinsi ya kupata fedha zaidi kutoka kwa watangazaji ambao tayari walikuwa wanatangaza kwenye website yao,
Mark alionekana akiviingiza kila kitu kichwani huku jibu lake lilikuwa ni moja alilolizoea " inavutia" jibu ambalo halikusaidia hata kidogo, jibu ambalo halikuweza kumwambia Eduardo ni nini Mark alikuwa anafikiria, labda kumwelezea ni nini kimekuwa kikiendelea kwa mwezi mmoja ambao umepita na au hata kuhusu interns na kazi zinaenda vipi.

Hatimae walifika mahali palipokuwa na party, palikuwa ni kama club, walifanikiwa kuingia na kumwangaza Sean Parker ambae aliwaona na kuwapungia mkono, walimwona na kumfuata mahali ambapo palikuwa ni VIP

Walipokuwa wameketi wakinywa vinywaji vyao, Sean aliwasimulia kuhusu mara ya mwisho yeye kuwa katika club ile yeye na mwanzilishi wa Paypal, Sean aliongea haraka haraka kama kawaida yake wakati huo ambao Eduardo alikuwa akiangaza huku na kule.
Eduardo aliona meza iliyo pembeni yao ikiwa imekaliwa na wadada warembo sana ambao hajawahi pata ona, kwa jinsi walivyokuwa warembo haikumchukua muda kuwatambua wasichana wale kuwa walikuwa ni Victoria's secret models, kilichomshangaza zaidi ambacho hakuamini macho yake ni kuona msichana mmoja akimsogelea Mark na kuanza kuzungumza nae, 'jesus christ' alikuwa ni msichana anaevutia na alikuwa anaongea na Mark! Eduardo hakuhashumu labda mazungumzo yangeweza kuwa yanahusu nini ila alimwona msichana yule akiwa anafurahia, Mark yeye alionekana mwoga kama kawaida yake, hakujibu sana wala hakuongea sana lakini msichana yule hakuonekana kujali, sasa alimsogele Mark na kumshika mguu, Eduardo alivuta pumzi kwa mshangao huku akiacha mdomo wazi
hakujali tena story za Sean Parker ambae sasa alikuwa anaelezea jinsi ambavyo alivyotolewa Plaxo, jinsi ambavyo aliwekewa watu waliomfuatilia, kumtesa na kumlazimisha ajiuzuli- nani anajua kama ilikuwa ni kweli au sio kweli! Kiasi kwamba Sean Parker alikuwa ameapa kulipiza kisasi, kisha Sean aliongelea jinsi ambavyo thefacebook itaenda kuwa kitu kikubwa Duani na alionekana kuamini katika hili lakini kitu ambacho kilimboa katika website ile ni 'the' katika jina, aliona haikuwa muhimu kuwepo, kwani Sean hakupenda vitu ambavyo havikuwa vya muhimu kabisa.

Eduardo hakujali kingine, yeye aliendelea kumtazama Mark na msichana yule.
Kitu kilichofuatia kukiona ni Mark alisimama na model yule ambae alimshika mkono kumwongoza kutoka pale na kutoka ndani mle, Mark alikuwa ameondoka, Eduardo alikuwa akizungusha kichwa chake 'atakuwa ameona kitu ambacho alidhani atakiona kweli? Ni kweli kwamba Mark ameondoka mle club na msichana yule? Na kwani, alikuwa hadate tena na msichana yule wa ki Asia wa kule Harvard?!' ( Chuoni Mark alikuwa ameanzisha uhusiano na msichana wa ki Asia alieitwa Priscilla Chan )

'Holy shit' Eduardo alikuwa anauhakika kuwa alimwona Mark akiondoka na Victoria's secret model.
Eduardo akilini mwake akaona kuwa hiyo ni dalili wazi kwamba Sean alikuwa sahihi kuwa thefacebook ilikuwa inaenda kuwa kitu kikubwa Duniani

Baada ya siku nne Eduardo alikuwa ndani ya ndege tena akirudi NewYork.

Alikuwa amechoka, kila kitu kilimuuma, hakuwa na wa kumlaumu sababu aliyataka mwenyewe kwani ndani ya siku hizo nne alikuwa akifanya jitihada za kibiashara pamoja na kunywa kwa sana, kunywa pamoja na kwenda kwenye party nyingi akianzia aliyofikia usiku ule ambayo Mark aliondoka na Victoria's secret model na kutomwona tena mpaka kesho yake, alipomwuliza Mark kuhusu msichana yule, Mark hakuwa muwazi moja kwa moja lakini Eduardo alijua kuwa lazima kuna vitu vilifanyika. Baada ya hapo, hizo siku zingine zilikuwa ni zaidi ya party hiyo,Sean alikuwa akiandaa mikutano mbalimbali ya dinner, launch, breakfast na wawekezaji mbalimbali pamoja na wawakilishi wa software na watu mbalimbali wenye pesa walioonekana kuvutiwa na thefacebook kiasi kwamba walianza kuona offer halisi za mamilioni ya fedha zikitolewa
mbali na hapo walipata kwenda kwenye migahawa ya hadhi ya juu huku mara nyingi watu walioenda kuonana nao wakiwatumia magari mazuri mazuri kwa ajili ya kuwachukua.
ilikuwa ni siku moja ambayo gari bovu la Mark lilishindwa kuwaka asubuhi ile na kuwafanya wachelewe kwenye breakfast meeting na hivyo mwekezaji walietakiwa kuonana nae aliahidi kumnunulia Mark gari mpya.
Alikumbuka mkutano wa ajabu kuliko yote, siku moja kabla ya hiyo siku ya kuondoka, yeye na Mark walialikwa kwenye boat ya mmoja wa waanzzilishi wa Sun Microsystems ambapo walikuwa vyakula vya ajabu na kunywa pombe na mwanzilishi huyo, na baada ya jamaa huyo kulewa alianza kuwatamkia mamillion ya fedha ambayo yangewafanya yeye na Mark kuwa matajiri hasa lakini ilikuwa ni kwamba wamuuzie thefacebook.
Haikujalisha zilikuwa ni fedha kiasi gani, Eduardo hakuwaza kuiuza the facebook kwani alijua kuwa itaenda kuwa na thamani mbeleni, si yeye wala Mark hakuna alietaka kuiuza the facebook, Sean Parker-kwa vyovyote vile ni nani alijali alitaka nini?, hakuwa mmoja kati ya team ya facebook, alikuwa ni mshauri tu, alikuwa hahusiki, hakuwa chochote kile.

***

Tyler na Cameron walikuwa katika shindano la kusukuma mtumbwi,shindano ambalo hufanyika katika tukio lijulikanalo kama Henley Royal Regatta ambalo hufanyika kila mwaka katika mto ujulikanao kama 'River Themes' uliopo sehemu iitwayo 'Henley- on-Thames' England. Tyler alijua kushiriki katika tukio lile ilikuwa ni heshima kwa tukio lile lililoanza kuwepo tangu mwaka 1839, pia aliona kuwa angepata uzoefu ambao angeenda nao katika maisha yake yote.

Tyler,Cameron pamoja na team yao walijitahidi kusukuma mtumbwi dhidi ya team ya waholanzi, walisukuma kwa bidii zote mpaka dakika za mwishoni mtumbwi wao bado ulikuwa nyuma dhidi ya waholanzi ambao nao walikuwa wakifanya bidii. Dakika ziliisha na sekunde kwisha wakiwa nyuma ya Waholanzi ambao waliibuka kuwa washindi. Ilikuwa ni huzuni kwa Tyler kwa kutochukua ushindi ule lakini alijitahidi kuficha hisia zake

Sherehe za kukabidhi zawadi zilifanyika, sherehe ambazo zilihudhuliwa na watu wengi wa hali ya juu ambao walimsubiri Prince Albert of Monaco kwa ajili ya utoaji wa zawadi.
Tyler alipendezwa na kitendo cha Prince kumshika mkono na kulifahamu jina lake katika kumbukumbu zake, waliishia kushikwa mkono huku kombe likienda kwa waholanzi ambao walishangilia pamoja na hadhira iliyokuwepo, Tyler pia alionekana kuwapongeza kwa kushangilia pamoja na hadhira

Mwenyeji wa baba yao na kina Tyler alisogea na kuwatia moyo kina Tyler kwamba wasingeweza kushinda team zote mbili hivyo lazima mmoja angeshindwa
"Ahsante, ilikuwa ni kazi ngumu, wamestahili ushindi, walifanya kwa bidii" Tyler alijibu
"Vizuri, binti yangu alichukua picha nzuri lakini bahati mbaya ameshaondoka kwenda nyumbani "
"Labda anaweza kututumia kwenye e-mail" alisema Cameron
"Vizuri, nyie mpo kwenye thefacebook?" aliwauliza
Tyler aliganda kwa muda, yeah huenda amemsikia vizuri, ndio, amewasikia watu wengi wakiongelea kuhusu thefacebook lakini sio England, hakutegemea kuskia ikitajwa katika maeneo kama yale

"Samahani?" alitaka apate uhakika kama ameskia sahihi alichokiskia
"Unajua, web site. Mwanangu amekuwa akiniambia kuwa wanafunzi wote wa chuo Marekani wanaitumia, amerudi kutoka chuo Marekani, yupo kwenye hiyo web site muda wote, nafikiri mtamtafta kwenye hiyo web site muda wowote mtakao taka na atawatumia hizo picha"

Tyler alimwangalia Cameron ambae nae aliona hisia kama zake machoni kwake, hata hapa maelfu ya miles kutoka Harvard walikuwa wanaiongelea thefacebook! na kwa kuzingatia kuwa bado ilikuwa inapatikana kwa watoto wa chuo pekee nchini Marekani tena vyuo vingapi thelathini? Arobaini? Hamsini? Ilikuwa inakuwa kwa namna ambayo hakuna mtu angeweza kufikiri ambapo ConnectU ni kama iligandia getini, haikuweza kushindana na web site kama thefacebook, ukweli ukiwa kwamba watu waliipenda thefacebook, na mtandao kama connectU ulikuwa ni hakuna kitu katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii

thefabook ilikuwa ni kama jitu, tena Godzilla, linagonga kilakitu njiani

Tyler alilazimisha tabasamu na kujifanya kuongelea vitu vingine ili kupotezea mada ile.
Walikuwa wamejaribu njia zote za kutafta haki yao na kushindwa kupata walichostahili, uamzi pekee uliobakia ulikuwa ni kwenda mahakamani, uamzi ambao hawakuupenda hata kidogo, ulikuwa ni uamuzi halali ambao aliona ungekuwa mbaya kwani walijua ni jinsi gani vitu vitakavyotokea kwenye habari,ni kwa jinsi gani ambavyo watu wangeweza kuwaona yeye na Cameron pembeni ya Mark Zuckerberg. Walikuwa ni watoto mashuhuri kutoka familia tajiri na ya kisasa na Mark alikuwa ni mtoto wa kawaida na asiejasiri, aliejaribu kuiba njia yao ya umashuhuri na mafanikio, ilikuwa ni vita ambayo waandishi wa habari wasingeipuuza,watoto tajiri wenye fursa walioamini njia ya kufuata haki dhidi ya hacker ambae amekuwa akiwa tayari kuvunja sheria, Tyler alijua kuwa yeye na kaka'ke wataonekana vipi, lakini kama hicho ndo kitatakiwa kitokee ili kupata nafasi ya kupigania haki yao basi walikuwa tayari kwa chochote kile

Ndio ulikuwa uchaguzi pekee ambao Mark Zuckerberg amewaacha nao.

***

Eduardo alionekana ni mwenye hasira akikatiza katika mitaa ya NewYork, Alionekana alikuwa akienda kufanya kitu ambacho alihisi kingemwondolea hasira zake

Yote yakiwa yameanza siku tatu nyuma, baada ya yeye kutoka California kila kitu kilikuwa kinaenda sawa ambapo alijiskia vizuri kwa maendeleo aliyokuwa amesonga nayo na kampuni ya Y2M pamoja na mwekezaji mwingine, alimpigia simu Mark ili aweze kumwambia kila kitu, na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Eduardo hakuelewa kama Mark alikuwa sio mtu mwenye shukrani na jitihada za yeye kule New York au vipi, kwenye simu Mark alimsikiliza kwa nadra akielezea yote aliyoyafanya na mara alirukia kwenye story kuhusu party ambayo Sean Parker aliwapeleka, na baada ya hapo mazungumzo yalirukia kwenye wimbo wa Mark wa kila siku wa kumwambia Eduardo ahamie California kwa sababu kule ndo kila kitu kimekuwa kikitokea, computer coding, kuunganishwa na wawekezaji na wengine wengi, Mark alikuwa analazimisha kuwa Eduardo alikuwa akipoteza muda wake New York wakati kila kitu ambacho thefacebook ilikihitaji kingeweza kupatikana palepale Silicon Valley
Eduardo alijaribu kumwelewesha kuwa hata New York ilikuwa ni sehemu muhimu yenye vitu ambavyo kampuni inayokuwa ilihitaji, Mark hakutaka kumsikiliza hata kidogo, na kitu kibaya zaidi alichofanya ni Sean Parker kurukia kwenye simu na kuanza kumwambia kuhusu wawekezaji wa hali ya juu ambao alikuwa anaenda kuwakutanisha na Mark, aliongeza kuwa wawekezaji hao wataenda kutoa pesa kama watampenda Mark na kama Mark atawapenda, na tena itafanyika kwa haraka.
Eduardo alihamaki palepale kwenye simu kwamba yeye ndo anaendesha masuala ya kibiashara hivyo mkutano wowote na wawekezaji wowote lazima ahusishwe- sasa kwa vyovyote vile kwa nini huyu Parker alikuwa anapanga mikutano hiyo? Kwa Eduardo, haikuwa hata kazi ya Mark kutafta wawekezaji; alikuwa anatakiwa kuendesha upande wa kompyuta wa kampuni na pia Parker alikuwa hahusiki hata kidogo, alikuwa ni mgeni wa nyumbani tu tena mgeni wa nyumbani asiekuwa na maana

Baada ya simu ile, Eduardo, kwa hisia alizokuwa nazo ambazo zilikuwa zimeanza kuwa hasira halisi, kitu ambacho aliamua kufanya ili kuthibitisha hisia zake na kumfahamisha kuwa haikuwa sahihi kutomhusisha katika harakati zao,
Eduardo alimwandikia Mark barua akirudia kuuelezea uhusiano wao kibiashara, aliandika makubaliano ambayo walikuwa wamekubaliana kipindi wanaanzisha thefacebook, kuwa yeye ndie alikuwa mbadala wa masuala ya biashara ya kampuni na Mark masuala ya kompyuta, zaidi Eduardo akaongeza kuwa kwa kuwa anamiliki asilimia 30 za kampuni hivyo anauwezo wa kuzua mikataba yoyote ile ya kibiashara ambayo hatakubaliana nayo. Mark alitakiwa kukubali uhalisia hivyo Eduardo alitaka maandishi ya kuthibitisha kwamba yeye ndo mwongozaji wa masuala ya kibiashara.
Eduardo alijua kuwa ameandika aina ya barua ambayo mtu kama Mark asingeichukulia vizuri, lakini yeye alichoona ni kuwa alitaka kueleweka kama iwezekanavyo. Ndio Sean Parker amewapeleka kwenye parties nzuri za aina yake labda hata alimsaidia Mark kutoka na msichana wa Victoria's secret, lakini kwa mtazamo wa Eduardo ni kuwa Sean Parker alikuwa hahusiki na thefacebook, Eduardo alikuwa ni CFO, ameweka pesa ambazo zimeisaidia the facebook na mpaka muda huo bado alikuwa ni yeye anaefadhili shughuli zao California, japo alikuwa New York alikuwa bado anatakiwa kufanya maamuzi ya kampuni.

Baada ya kupokea barua ile, Mark alituma voice email nyingi huku nyingi zikimwomba Eduardo kuwa ahamie California, story nyingi kuhusu jinsi kule palivyo pazuri, uhakika mwingi kwamba kila kitu kilikuwa kinaenda sawa kwa kampuni na kulikuwa hakuna haja ya kubishana kwa vitu vidogo vya kipuuzi- 'vitu vidogo vya kipuuzi' kulingana na mtazamo wa dunia ya ajabu ya Mark.

Eduardo alimpigia simu tena Mark, mambo yalikuwa ni yale yale, Mark alimwambia kuwa amekutana na wawekezaji wawili ambao Sean Parker aliwahi kumwambia na kuwa walikuwa wako tayari kutoa pesa za mwanzo, kuipatia thefacebook pesa ili iweze kuendelea kukua kama kawaida, ilihitaji pesa kwa sababu ilikuwa inaenda kuingia katika deni la hatari, jinsi watu walivyoongezeka ndivyo ambavyo server zilihitajika kukabiliana na jam, na kitambo walikuwa wanaenda kuajiri watu ili kushughulika na kila kitu.
Lakini Eduardo hiyo ilikuwa ni nje ya point yake, yeye aliona kuwa Mark amepuuza hisia za kile alichokiandika kwenye barua na kuamua kufanya mikutano bila yeye kuwepo hivyo ni dhahiri kuwa alikuwa hakanyagi tu kwenye vidole vyake bali yeye na Sean Parker walionekana walikuwa wakijaribu kukata kabisa mguu yake
Huenda Mark alifikiri Eduardo hakuwa serious, labda barua yake ilikuwa ni njia tu ya kuondoa hisia zake au labda ilikuwa vyovyote vile lakini jinsi ambavyo Mark alichukulia mambo ilimkera Eduardo. Eduardo aliona kuwa walikuwa huko California kwa pesa zake, nyumba waliyokuwa wakiishi, vifaa vya kompyuta, Servers, lifestyle yake huko California, kila kitu kilikuwa kinatoka ndani ya akaunti ambayo Eduardo alikuwa ameifungua na kuweka pesa zake binafsi, alikuwa analipa kila kitu halafu Mark anamdharau,anampuuza, anamtendea utafikiri ni girlfriend waliekosana na kwamba alikuwa hamjali tena!

Kwa vyoyote vile, kwa hizo siku alipata uhakika wa kutaka kufanya kitu ili kumwonesha Mark hali halisi aliyojiskia.
Alitaka kutuma ujumbe ambao Mark hataupuuza

Hivyo kwa hasira zile akikatiza mitaa ya Newyork aliweza kwenda bank na kuingia moja kwa moja mpaka sehemu husika, banker yule alimuuliza amsaidie nini, Eduardo ambae altoa kitabu chake cha bank na kukitupia mezani pale huku akiwa serious, alisema-

"Nataka kusimamisha akaunti yangu ya bank na ukate cheque zote na njia zote za malipo zilizokuwa zimeunganishwa kwenye akaunti hii"

Mfanyakazi alianza kufanya vile maramoja.
Eduardo alijua kuwa anavuka mpaka lakini hii ilikuwa inaenda kutuma meseji halisi kwa Mark kwamba ni kiasi gani alikuwa serious. Akilini mwa Eduardo aliona kuwa ni Makosa ya Mark ndio yamefanya mpaka yeye akapata nguvu za kufanya vile, alitaka kumwonesha Mark ilimaanisha nini kuwa Partner mzuri, yeye hakujali kama kila kurasa ya thefacebook ilikuwa na 'Mark Zuckerberg production' ila kampuni ilikuwa ni jitihada walizoziunganisha, Eduardo alikuwa ni mtu wa biashara na hatua hiyo aliyoichukua ilikuwa ni ya kibiashara

Eduardo alipoangalia mfanyakazi yule wa bank akibofya vitufe kwenye kompyuta na kufunga akaunti, alipiga picha ya Sean na Mark California wakikimbia kwenye mikutano na wawekezaji na labda huku wakimcheka kwa jitihada zake za kutaka kuwaongoza.

Alipiga picha kuwa hawatacheka tena watakapojaribu kwenda kutoa pesa na kukuta tupu.

ITAENDELEA....
 
Back
Top Bottom