The Advantage of being a latecomer: Yanga tunalo la kujifunza kwa Simba

Mimi nafikiri nguvu kubwa tuiweke hapo kwenye scouting. Tuwe sharp kuwaona wachezaji wazuri na kuwqsajiri kwa gharama ndogo kabla hawajaonwa na hao wakubwa lakini ukisema tumwage hela kushindana na hao wakina al ahly na mamelod hatuwezi. Kumbuka uchumi wa nchi zao ni mkubwa ukilinganisha na uchumi wetu na uchumi wa nchi unaeleza uchumi wa vilabu. Ukimuweka pembeni Mamelod sundowns kwa sasa Yanga anaweza kuzipiga klabu zote za South afrika lakini ukija kwenye msuli wa pesa kuna klabu kama orlando pirates, keizer chiefs ambazo zimemuacha yanga mbali sana kiuchumi. Tukitaka kushindana kiuchumi na hao jamaa hatuatweza tuimalishe tu vitengo vyetu vya scouting.
 
WakatibRoman anainunua Chelsea hakukuwa na Cole,Terry wala Super Frank mkuu.

Labda Uweke Zola, Flo na Petrescu
Uache ujuaji... Terry alikuwapo, Lampard alikuwapo, Cole alikuwapo ... Wote hao walikuwapo pamoja na Petit, Carlton Cole, Jimmy Floyd Hasselbaink, Crespo, Gronkjaer, Makelele, eidur gudjohsen, Adrian Mutu, Scott parker , veron wengi mnooo .... Acha kudanganya watu...
 
Mimi nafikiri nguvu kubwa tuiweke hapo kwenye scouting. Tuwe sharp kuwaona wachezaji wazuri na kuwqsajiri kwa gharama ndogo kabla hawajaonwa na hao wakubwa lakini ukisema tumwage hela kushindana na hao wakina al ahly na mamelod hatuwezi.
Nakubaliana na wewe. Lakini hii inahitaji Scouting Network kubwa na yenye weledi sana, ambavyo vyote hivi vinahitaji ADMINISTRATION NZURI YA CLUB & ADEQUATE FINANCING—Ambayo haya ni matatizo yetu makuu.
Hivi chief, ni kweli kabisa kwa football culture iliyopo Tanzania, hatuwezi pata uwekezaji wa kufikia level ya walau ¾ ya Mamelodi?
 
Natamani huu uchambuzi ufanyike pale Azam Tv na usiongezewe Wala kueditiwa chochote.
 
Ndugu yangu ubarikiwe Umeongea Fact tupu mwenye Masikio na asikie
 
kutengeneza scoting nzuri tunaweza kumudu mfano usajiri wa Mayele tuliweza kumuona kabla ya wakubwa lakini kwenye kushindana nao kumchukua mchezaji hatutaweza watatuzidi tu kwenye dau kuhusu wawekezaji wa level za mamelod bado hatujafika uko mkuu. Uchumi wa nchi tia maji tia maji kwaiyo tuna kundi kubwa la wananchi masikini wenye hali za kawaida ni wale wanaoweza kupata mahitaji muhimu tu mfano mimi jezi ya mwisho ya yanga kununua ni ya msimu juzi sio kwamba sipendi kununua jezi ya kila msimu lakini uchumi wangu unanikwamisha kufanya ivyo, tukija kwa hao wawekezaji kumbuka lazima waangalie na faida yao pia. Sasa mashabiki hawalipi kadi za uanachama, hawanunui jezi origino, kujaza uwanja ndio mpaka wakutane simba na yanga. Hao wakina mamelod na al ahly uchumi wa nchi zao ni mkubwa kwaiyo automaticaly hata expending power ya mashabiki ni kubwa.
 
Sawa lakini uhalisia unabaki kwamba Katika Ligi alilopo Man utd,.... Man city ndo hubeba kombe sambamba na Liverpool ambao wote hao wana misuli ya kiuchumi na Vikosi ghali sana,

Kwa upande wa Psg wao uwekezaji wao umezaa matunda kidogo maan kwenye ligi lao yeye ndo mwenye makombe mengi na pia Hata Uefa hayuko mbali sana maan alifika fainali ya Uefa japokuwa akafungwa ila kimalengo yupo karibu sana kufanikisha lengo la kuwa bingwa ulaya,

Ukitaka kuamini hilo Angalia katka mitandao mbalimbali ya Football Prediction & statistics utaona katka Timu 8 zinazopewa Uwezekano wa Kubeba Uefa basi Psg ipo kwenye List,

Ila Tukija upande wa Caf hata katka Timu nne zinazopewa uwezekano wa kubeba Caf champions League Simba wala Yanga Haipo.

Tukirejea Uefa jarbu kuangalia washindi wa Uefa kuanzia miaka ya 2009 mpak leo ? Utagundua washindi wote ni vilabu vyenye Squad ya gharama sana... Na ukitak kuamin hilo angalia Atletico alifungwa mara mbili Fainali na Madrid....ni kutokana na Squad quality tu na si vinginevyo.

Mpira kuanzia miaka ya 2005 kupanda juu umebadilika sana ni mwenye kikosi ghali na Team management nzuri ndo hupata Mafanikio tofaut na hapo Ni Kwenda kuzuga tu kwenye mashindano.
 
kutengeneza scoting nzuri tunaweza kumudu mfano usajiri wa Mayele tuliweza kumuona kabla ya wakubwa lakini kwenye kushindana nao kumchukua mchezaji hatutaweza watatuzidi tu
Sasa hapa hatuwezi endelea.
Kama tunakuwa tunasajiri wachezaji wenye viwango kisha hatuwezi wamantain tunaingia gharama kubwa zaidi tukimuuza kuliko kummantain—Kwanza tunasajiri mchezaji hatuna guarantee ya mchezaji kuperfom mf Konkon, pili inahitaji muda kuingia kwenye mfumo wa Timu— fikiria Gharama za Konkon kumsajiri, kumvunjia mkataba na tatu tunasajiri mwingine AMA Kuongeza kile alichokuwa anakitaka mayele kama ongezeko la malipo yake ipi ni maamuzi ya busara zaidi? Hii ndio ninaita Ukariakoo uliopo kwenye uongozi wa Simba na Yanga—KARIAKOISM.
 
Kwanza ni dunia nzima, washabiki ni wengi kuliko wanachama.

Nchini kwetu Wanachama ni wachache kwa sababu hizi:
1. Hakuna uwajibikaji vilabuni.
Hakuna mtu anayeweza lipa hela yake bila kujua inaenda fanyia nini na aone kweli kitu hicho kimefanyika. Bila kuwa na uwajibikaji mzuri, bado mashabiki watakuwepo ila si wanachama hai.

2. Hakuna Engagement kubwa ya Wanachama na Timu zao. (Huku matawini).

3. Shabiki hatuoni faida ya kuwa na kadi.
Mfano, Timu zikiweka utaratibu kuwa ukinunua tiketi au jezi kwa Kadi unapata punguzo fulani, unadhani shabiki ataacha kuwa na hiyo kadi?

Kitu kingine bado vilabu vijafanya vya kutosha, kugeuza huu Usimba na Uyanga kuwa hela. Mfano, Hivi unajua Simba au Yanga wakiingia mkataba tu na Dume Condoms na wakatengeneza Condoms zenye pakiti yenye usimba na Uyanga, ni revenue kubwa kwa Club?

Ni kweli wengi hatuwezi nunua jezi ya sh elfu 50. Lakini hatushindwi nunua Jambo Juice/Sayona ya sh 500 ikiwa na usimba au Uyanga ndani yake.

Ushawahi waza kuwa unaweza shawishi waajiriwa, kila mwisho wa mwezi wakuchangie hata Buku tu kwenye mishahara yao? Kwa hiari kwa kutengeneza automated systems ambazo vilabu vinapokea moja kwa moja kama vile NHIF wanavyoipokea?

Bado naamini katika 'ujero jero' wetu huu, bado vilabu vinaweza tengeneza mabilioni ya Shilingi na kuwa na financial power kubwa.

Shida iko wapi, Simba/Yanga ikaajiri Consultant, si lazima atoke nje, hata Chuo Kikuu chochote hapa hapa Bongo chenye uwezo, wakafanya tafiti namna gani ya kutumia Fan base yetu kuongeza mapato ya Timu.
 
Ndio gharama za kuwa masikini izo mkuu. Hauwezi kuafford kuwa na kitu kizuri ambacho mwenye pesa anakitaka. Hata yanga hakupenda kumuuza Mayele ndio ivyo mchezaji anataka kwenda kwenye malisho mema
 
Ni kweli mkuu uwajibakaji na uwazi ni mdogo sana kwenye masuala ya hela lakini naamini ni mwanzo tutazidi kupiga hatua ila kumshawishi mtanzania atoe hela ni rahisi kwa kuongea lakini kwa vitendo ni ngumu sana.
 
Ndio gharama za kuwa masikini izo mkuu. Hauwezi kuafford kuwa na kitu kizuri ambacho mwenye pesa anakitaka. Hata yanga hakupenda kumuuza Mayele ndio ivyo mchezaji anataka kwenda kwenye malisho mema
Chief, mimi naamini Yanga haikushindwa mlipa hiyo M47—inayosemwa—hatukuwa na final say na huyu mchezaji. Haiingii akilini ushindwe mlipa nyongeza ya M300 kwa Mwaka halafu unaanza hangaika sajili tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…