The Advantage of being a latecomer: Yanga tunalo la kujifunza kwa Simba

The Advantage of being a latecomer: Yanga tunalo la kujifunza kwa Simba

Ni kweli mkuu uwajibakaji na uwazi ni mdogo sana kwenye masuala ya hela lakini naamini ni mwanzo tutazidi kupiga hatua ila kumshawishi mtanzania atoe hela ni rahisi kwa kuongea lakini kwa vitendo ni ngumu sana.
So far tumepiga hatua fulani. Tunaingia Phase 2 sasa.
 
Kwanza ni dunia nzima, washabiki ni wengi kuliko wanachama.

Nchini kwetu Wanachama ni wachache kwa sababu hizi:
1. Hakuna uwajibikaji vilabuni.
Hakuna mtu anayeweza lipa hela yake bila kujua inaenda fanyia nini na aone kweli kitu hicho kimefanyika. Bila kuwa na uwajibikaji mzuri, bado mashabiki watakuwepo ila si wanachama hai.

2. Hakuna Engagement kubwa ya Wanachama na Timu zao. (Huku matawini).

3. Shabiki hatuoni faida ya kuwa na kadi.
Mfano, Timu zikiweka utaratibu kuwa ukinunua tiketi au jezi kwa Kadi unapata punguzo fulani, unadhani shabiki ataacha kuwa na hiyo kadi?

Kitu kingine bado vilabu vijafanya vya kutosha, kugeuza huu Usimba na Uyanga kuwa hela. Mfano, Hivi unajua Simba au Yanga wakiingia mkataba tu na Dume Condoms na wakatengeneza Condoms zenye pakiti yenye usimba na Uyanga, ni revenue kubwa kwa Club?

Ni kweli wengi hatuwezi nunua jezi ya sh elfu 50. Lakini hatushindwi nunua Jambo Juice/Sayona ya sh 500 ikiwa na usimba au Uyanga ndani yake.

Ushawahi waza kuwa unaweza shawishi waajiriwa, kila mwisho wa mwezi wakuchangie hata Buku tu kwenye mishahara yao? Kwa hiari kwa kutengeneza automated systems ambazo vilabu vinapokea moja kwa moja kama vile NHIF wanavyoipokea?

Bado naamini katika 'ujero jero' wetu huu, bado vilabu vinaweza tengeneza mabilioni ya Shilingi na kuwa na financial power kubwa.

Shida iko wapi, Simba/Yanga ikaajiri Consultant, si lazima atoke nje, hata Chuo Kikuu chochote hapa hapa Bongo chenye uwezo, wakafanya tafiti namna gani ya kutumia Fan base yetu kuongeza mapato ya Timu.
Chief kusema ni rahisi ila utekelezaji wake sio mrahisi kiivo km hilo la vinywaji sidhani kama sheria za nchi zinaruhusu
 
Nimekumbuka maoni yangu, SIMBA inakwamishwa na MO.
 
Miaka ya 2000 Mwanzoni, Mpira wa Uingereza—ligi fuatiliwa zaidi duniani—ulikuwa umetawaliwa na Klabu Mbili tu; ARSENAL na MANCHESTER UNITED.

Liverpool alikuwa msindikizaji, Manchester City alikuwa bado 'chandimu'. Chelsea walikuwa na timu nzuri sana—Frank Lampard, John Terry, Joe Cole, Petr Cech—lakini haikuwa chochote mbele wakubwa hao wawili. Lakini mambo yalibadilika mwaka 2003, Roman Abrahamovich alipoinunua timu hiyo. Kuingia kwa tajiri huyo wa kirusi kulifuatiwa na Kuja klabuni hapo, kutoka Man U, kwa Peter Kenyon kama Mtendaji Mkuu.

Watu hao wawili walipoingia Klabuni ulikuwa ndio mwanzo wa mafanikio ya Timu ya Chelsea hadi kuwa hivi ilivyo leo. Uwepo wa watu hawa, ukakamilisha mawili ya LAZIMA—mbali na wigo mpana wa mashabiki—ya maendeleo ya timu yoyote ile dunia; FEDHA YA KUTOSHA na UTAWALA WA KIWELEDI (FINANCIAL MUSCLES and PROFESSIONALISM IN MANAGEMENT).
View attachment 2825231

Turejee kwetu. Toka mwaka 2018, club ya Simba imekuwa na mafanikio makubwa sana ya Mpira barani africa. Leo inacheza African Football League, kama kigogo wa Kanda hii ya Africa Mashiriki kutokana na record yake ya miaka mitano nyuma. Mafanikio haya yametokana na Uwekezaji Mkubwa wa fedha uliofanywa na Mohamed Dewji ambao wote tunaufahamu. Amekuwa na CEOs bora kama Senzo na Babra Gonzalez ili tu kukamilisha Utatu Mtakatifu wa mafanikio ya timu yoyote (Mashabiki, Muwekezaji/Tajiri na Utawala). Lakini sasa Simba inashuka. NDIO SIMBA INASHUKA. AMELETWA BENCHIKHA, LAKINI BADO SIAMINI KAMA ITAFANYA LOLOTE.

Mohamed Dewji ni tatizo. Ukitazama upangaji wa makundi ya CAFCC, Utaona kuna Teams 1, 2, 3 na 4 haya ni madaraja ya ubora.
View attachment 2825833
Timu kama Al Ahly, Mamelodi, Wydad Na Esperence de Tunis hawa ni Daraja 1, Teams kama Simba ni Daraja la 2, Yanga ni Daraja la 3, Medeama ni daraja la 4. Sasa hapa Simba ilipo, ni matokeo ya uwekezaji mkubwa wa kifedha wa Mohamed Dewji—Kusajili, Kuhudumia na Miundombinu ya michezo ya timu. Ili Simba, iwe ya daraja la kwanza (African level kuwa sambamba na kina Al Ahly, Mamelodi, Wydad au ES Tunis), inabidi tajiri wa Timu afungue Pochi haswa.

Mfano, kwa mujibu wa Tovuti ya Transfermarket, Mamelodi na Al Ahly vikosi vyao vina thamani ya Shilingi Bilioni 80, Wydad na ES Tunis zina Shilingi Bilioni 47. Kikosi cha Simba kina thamani ya Shilingi Bilioni 8 tu. Huku Yanga kikosi chake kina thamani ya Bilioni 4 tu. Tazama maana zaidi ya hizi namba; Simba yeye ni wa Pili kwa ubora, wa chini yake (watatu) Asec Mimosas wa Ivory Coast kikosi chake kina thamani ya Shilingi Bilioni 3 na wanne kwake ni Jwaneng Galaxy ya Botwasana ina kikosi chenye thamani ya Milioni 210.

Hivyo ukweli ni kuwa ili tufike viwango vya juu kabisa Africa, ni lazima tuwe na vikosi vyenye thamani kubwa sana. Tutaweza sajili wachezaji wenye hadhi ya juu kabisa wa ndani na nje ndipo hapo tutaweza kaa meza moja na kina Al Ahly na Mamelodi. Mohamed Dewji amewekeza kuifikisha Simba Daraja la Pili-Chini au tuseme Daraja la Tatu-Juu. Hakuna uwekezaji anaofanya sasa wa kuipeleka daraja la Kwanza. Simuoni kama Mohamed Dewji ni muwekezaji serious wa kuifikisha Simba Daraja hilo. Kwanini simuoni kama ni muwekezaji Serious, Bilioni 50 kwake ni kiasi anachokimudu, kwani utajiri wake Trilioni 3 kwa mujibu wa Forbes. Namuona kama ni mfanyabiashara aliyeridhika/aliyehitaji/anayehitaji nafasi hii tu iliyopo sasa—kwake inamlipa kibiashara ndio maana anafanya mambo ya kijanja janja ya kupumbaza mashabiki na kuzima moto ili kumantain Status quo. Ni aidha Mo abadilishe mindset na kuwaza Daraja la Kwanza au Simba itafakari muwekezaji Mpya mwenye kuweza kutupa Squad yenye thamani ya walau Bilioni 50.

2. Utawala wenye weledi.
Mwaka jana, aliyewahi kuwa mchezaji wa Super Sport United wa Africa Kusini, alihojiwa na Gazeti la The Citizen la Afrika Kusini hlompho Kekana, akielezea mafanikio ya Timu ya Mamelodi Sundowns. Maoni ya kekana ni kuwa mafanikio ya Mamelodi, sehemu kubwa yaliletwa na kuwa na Scouting Team nzuri, yenye mtandao mpana iliyoleta wachezaji wazuri na sahihi kuweza kutengeneza timu imara.


Kwenye timu yoyote ya mpira, kimsingi Mtendaji Mkuu (Chief Executive Office) huyu ndiye injini ya kuendesha timu. Kwa Simba ni mtu kama Imani Kajula, kwa Yanga ni Andrew Mitine kwa Azam ni Abdulkarim Amin au Popat. Sasa, hawa Kimsingi huongozi idara tatu—Idara ya Uendeshaji ( utawala, mapato na matumizi ya Timu mfano kutafuta wadhamini, kulipa mishahara n.k), Huduma za klabu (Ustawi wa klabu mfano Ulinzi, matibabu n.k) na Tatu ni Idara ya maendeleo ya Mpira (soka lenyewe kwa ujumla). Sasa kwenye Hizi idara kunakuwa na Vitengo mbalimbali, Mfano Kitengo cha Michezo, ambacho Kocha wa Timu huwa chini ya kitengo hiki, Pia kuna Kitengo cha Kutafuta wachezaji (Scouting Team). Sasa ili timu iwe na kikosi kizuri, rejea maneno ya Kekana hapo juu kuhusu Scouting. Na Scouting team ili ipate wachezaji wazuri wa kufit na timu lazima wawe na masikilizano na kocha, pia lazima wawe na mtandao mpana, yaani wasambae maeneo mengi duniani hivyo lazima wawezeshe kifedha (IDARA YA UENDESHAJI & TAJIRI), wawe na utaalamu na weledi na wawe na Usimamizi bora wa kiweledi (CEO COMPETENT). Ndio maana unaona Mamelodi wamefanikiwa hapo walipo—HELA ZA PATRICE MOSEPE na MANAGEMENT BORA. Ndio maana Chelsea iliamka kuanzia 2004—HELA ZA KUTOSHA ZA ROMAN ABRAHAMOVIC na MENAGEMENT BORA YA PETER KENYON. Bahati mbaya sana Management bora inategemea na Utashi na Ufanisi wa Tajiri. Hivyo, Simba inaenda kuporomoka hapa ilipo, isipoachana na Mohamed Dewji huyu wa sasa—mjanjamjanja na kuwa Mohamed Dewji Mpya—Serious Investor au kutafuta Tajiri mwingine aliye serious kuweka mzigo wa maana.

Sasa, sisi Yanga tuna bahati kubwa. Tumechelewa. Ukichelewa una faida ya kujifunza kwa aliyetangulia. Simba ametutengenezea nafasi ya 'heshima'. Sasa tujifunze kwake, anapokosea! Sina shaka na trend ya Yanga, lakini kila nikitazama. Nikirejea hulka za 'kikariakoo', nahisi nasi tutapita njia ya Simba.

Muda ni muamuzi mzuri.
Una point ila mwisho huku sijui umechoka, umeamua kufupisha kwa ku balance usionekane unapendelea upande mmoja.
 
Una point ila mwisho huku sijui umechoka, umeamua kufupisha kwa ku balance usionekane unapendelea upande mmoja.
Hakuna nilipopendelea. Nimekua wazi kutoa angalizo kwa timu yangu ya Yanga. Tujifunze kwa Makosa ya Simba.
 
Back
Top Bottom