Geog-language
Member
- Oct 22, 2023
- 8
- 9
Tanzania ni nchi yenye wasomi wengi sana wenye maarifa ya hali ya juu,uwezo mkubwa katika proffesional zao na vyeti ambavyo vina watambulisha kuwa wamefuzu katika fani zao walizo somea kama Ualimu , Afya na nyenginezo.
Ila mbaya zaidi wasomi hao wengi wana maisha ya chini sana na wengi wao Hawana ajira mpaka leo wengine wanakaribia umri wa kustaafu . Hali ambayo ime ifanya Tanzania kuwa na uchumi ambao sio mzuri sana tukiangalia maisha ya mwananchi mmoja mmoja
Mfano Kwenye "RIPOTI YA HALI YA UCHUMI WA TANZANIA" ya mwaka 2023 inayo tolewa kila mwaka na BENKI YA DUNIA (WB) . Katika uzinduzi wa toleo la 20 la taarifa ya hali ya uchumi wa Tanzania ime onyesha
"mwaka 2018 takribani waTaanzania milioni 14 walikuwa wakiishi katika umasikini lakini kufika mwaka 2022 idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia milioni 17 na ilipofika Desemba 2023 idadi hiyo iliongezeka nakufika milion 17.3 World Bank ime Kadiria idadi hiyo itaongezeka zaidi kila baada ya miaka 23 huku kukiwa na uwezekano wa kufikia watu milioni 140 ifikapo 2050 " by Mkurugenzi mkazi wa WB Nathan Balete
Ili Uchumi wa Tanzania uweze kubadilika ni lazima tuwekeze katika vijana na kuwawezesha. Vijana wana hali mbaya na wengi ni wasomi wazuri , wenye maarifa ila ajira ndio kikwazo kwao kwani elimu waliyo ipata ime jikita kwenye KUAJIRIWA ndio waweze KUTOBOA KIMAISHA . Wakati ajira ni ngumu na nyingi zinahitaji una mjua nani na sio unajua nini.
Hata hili lime thibitishwa katika kauli ya CDF mstaafu Mheshimiwa venance mabeyo
" vijana wetu wako hoi wana hangaikia ajira "
Ni wazi tume kwama kwa kiwango fulani katika ku support vijana tulio watengeneza wenyewe na hii lina nitafuna hata mimi kama muandishi kuona kijana mwenye degree ya ualimu aliye someshwa kwa gharama nyingi na wengine mikopo ya serikali kabisa , wanakaa mtaani zaidi ya miaka 9 bila ajira nahii ime kuwa kama desturi kuwa kijana akimaliza masomo ya elimu ya juu ni ngumu kuajiriwa moja kwa moja .
Nashukuru kwa jamii forum kutoa fursa hii kwa watanzania wazalendo watoe maoni yao juu ya Tanzania tuitakayo . Leo nita changia wapi tuna kwama na nini kifanyike ili kuipata Tanzania bora katika miaka mi 5 au 25 ijayo
1 . Kupata viongozi wenye hofu na Mungu na wafanye kazi kwa nia ya kuwatumikia kweli watanzania. Mwalimu aliwahi kusema
“Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM” Dodoma, 1995.
Viongozi wengi wanaongoza kuwa na maisha mazuri kwa upande wao kupitia nyadhifa walizo pata kitu ambacho kime tamanisha wengi kutaka nafasi hizo ili wanufaike wao nasio kwa nia ya kutumikia jamii nzima. Hivyo ili tuipate Tanzania nzuri tuanze kuwapa vijana elimu ya kuwa viongozi waadilifu na walio juu wafanye walicho agizwq na wananchi hali sio huku mtaani .
2. Vijana wapewe nafasi katika nyadhifa kubwa ya kuwa sehemu ya wafanyaji wa mambo mbali mbali katika serikali na siasa kiujumla. Mwalimu akiwa na miaka 39 aliweza kuikomboa Tanganyika hii Ina onyesha vijana wana uwezo na nguvu kubwa ya utendaji.
Ila kwa sasa tunaona niwazi tumekosa njia kubwa ya kuwashawishi na kuwatengeneza vijana wawe na hamu ya uongozi japo kuna jitihada kama vile kuwepo kwa vyuo vya uongozi ila uitikaji wao ni mdogo . Asilimia kubwa ya wafanyaji kazi serikalini na wenye nyadhifa mbali mbali ni watu wa makamo yaani sio vijana . Huku kundi kubwa la vijana likiwa bado halija aminika kupewa nyadhifa fulani wakionekana hawana ufanisi ,uzoefu au uwezo kitu ambacho sio kweli
3. Viongozi walio madarakani na walio ahidi kutimiza agenda za vijana na jamii nzima wajitathimini .
Roma mkatoliki anasema
" anaye chelewesha msafara siku zote ni ng'ombe wa mbele ila huwa anapigwa wa nyuma na ndiye anaye piga kelele" nipeni maua yangu .
Wenye nyadhifa za juu na walio juu ambao ndio wawakilishi wa wananchi wajitathimini utendaji wao wakazi na kuangalia matatizo yanayo wakumba wa Tanzania badala ya kupendezesha maisha yao binafsi maana ni wazi mtu yeyote mwenye nyadhifa ya uongozi kama ubunge au uwaziri sio level zako au nani anionyeshe mtoto wa mbunge ambaye ni boda boda au mchoma mkaa au muuza mitumba .
Hivyo sababu kubwa ya hali ngumu kwa vijana na jamii ya Tanzania kiujumla, ni kutokuwa na kawaida ya kutathimini utendaji wa ahadi wanazo ahidi kipindi cha uchaguzi nivyema ikaundwa tume ambayo itakuwa ina kagua utendaji wa kiongozi mmoja mmoja
4. Ni kwa Vijana wenyewe ambapo wana wajibu waku badilisha taswira mbaya katika jamii iliyo dhidi yao.
Muda mwengine vijana wanakosa nafasi serikalini au kwenye miradi mbalimbali katika jamii kulingana na wao wanavyo jiweka hivyo ili tufikie mabadiliko katika miaka 10 au 20 ijayo ni lazima vijana wawe watu walio staarabika kuanzia mavazi ,matumizi ya lugha na matendo ili jamii iweze kuwaamini
Pia vijana inapaswa washiriki katika makongamano na vikao mbalimbali vya kiserikali kwenye ngazi ya kata ,wilaya au mkoa .
CONCLUSION: TUMEWATENGA SANA VIJANA NAFASI NYINGI SERIKALINI NI ZA WATU WA MAKAMO , VIJANA HAWANA FURAHA NA ELIMU ZAO , TULIO JUU TUTUMIKIE TAIFA , KEKI YA TAIFA NI KUBWA TULE WOTE MBINGUNI HATUTAENDA NA MALI YOYOTE TULEGEZE KAMBA TUTA WAUA HAWA WATU WACHINI.

Attachments
Upvote
5