The Best FIFA Football Awards 2019: Messi atwaa tuzo ya Mchezaji bora, Klopp awa Kocha bora

Naona Mkuu umeamua usipepese macho, umepiga penyewe.
 
Naona post zako haters wanazikimbia, aibu imewashika wanashindwa kukujibu.
 

Yes, sehemu nyingine zote nimekuelewa kuhusu hao wachezaji wengine ila hapo kwa Messi hapana.

Unaposema Messi hakuwa na kiwango bora last season unamaanisha nini?
Nani mfungaji bora wa uefa?
Nani mfungaji bora la liga?
Nani top assist uefa?
Nani top assist la liga?
Nani mfungaji bora ulaya/Dunia mzima?

Siku nyingine jifunze kutofautisha kati ya kubeba makombe na overall perfomance ya mchezaji.

Kumbuka unaweza kuwa na msimu mzuri ila usibebe makombe, na tumeyaona hayo kwa misimu kadhaa nyuma, Luis Suarez hakubeba kitu chochote ila alikuwa player of the year akiwa liverpool kwa ligi ya england.

Kwa mwaka huu hakuna mchezaji ambae alimkaribia Messi, labda kidogo Bernado Silva kwa kiwango bora na kwa hao alioingia nao top 3 kiukweli andunje alistahili kubeba hiyo tuzo.
 
Mbona hao UEFA hawakumpa? maana haya yote kayafanya Europe ije kuwa FIFA ambao hatujui vigezo vyao.

Jibu: Uefa wanaandaa UCL, EUROPA LEAGUE kwa ngazi ya vilabu so lazima focus yao ingekuwa hapo kwenye kubeba champions ligi na sio overall perfomance na tumeona hivyo kwa misimu kadhaa nyuma.

Kumbuka kubeba uefa hakukufanyi wewe uwe bora bali ubora wako unatokana na overall perfomance ya msimu mzima.

Yaani fifa wampe mchezaji bora beki? Kwa kazi gani ambayo anafanya? Yaani kusimama na kupiga vichwa mipira na zile tackling huku akiwa kakimbia kilometre 3 ndani ya dakika 90?

Hapana, hapana, hapana kwangu mimi mchezaji aliekuwa kwenye kiwango bora last season kwa Liverpool ni Sadio Mane na Bernado Silva kwa mancity ila kwa Dunia mzima Messi alikuwa best zaidi ya hao niliowataja na takwimu zinambeba, kumbuka mpira ni mchezo wa namba
 
Namba hazidanganyi kabisa.Shida ni tunaukwepa ukweli kisa tu tuna mapenzi.Haya mambo ndio yanatupoteza sana huku bongo.
 
Watakuelewa tu.
 
Eti VVD hakustahili kuwa huruma basi....Angekuwa mchezaji bora wa EPL?????kwan B.silva,Mane Hawakuwepo??????.....FIFA NI UOZO IPO KIBIASHARA BASI.....
 
Hujui Maana ya UEFA....Labda nikwambie tuu UEFA ni Kama CAF Afrika au Kama CONCAFA amerika kaskazin au kama CONMEBOL amerika kusini...So haiongozi vilabu tuuu...hadi Nationa team na michezo yote Barani Ulaya ya Football
 
Hahah! Mkuu umemaliza kila kitu, jamaa anaupiga mwingi kwa miaka mingi mpaka wamezoea wanaona kawaida sasa ....

Wakiongelea ndoo basi waseme anaestahili ni B. Silva, Mahrez au Allison kwa mbaaali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…