Tatizo huyu jamaa kawa kwenye kiwango kwa muda mrefu so watu wamemchoka kila siku kuona anapata yeye, watu wanataka mageuzi bila hata ya kutoa jasho.
Last year tuzo aliyopewa Modric watu hawakuzungumza kwakuwa alipewa mwingine nje ya cr7 na Messi ila walisahau kama walitaka apewe mwenye mafanikio kwa kubeba makombe basi wangempa Varane.
Wengi wetu tunaotaka apewe Virgil ukiuliza kwanini apewe yeye lazima tutasema kwakuwa kabeba uefa na huku tumesahau kuwa Alisson becker kabeba uefa na copa america sasa kwanini tusimpe alisson becker kama issue ni kubeba makombe?
Kwa mwaka huu, nje ya Bernado Silva na kidogo Reheem Stearling sioni mwingine ambae alikuwa na kiwango bora than La Pulga.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Messi alistahili hii tuzo, yaani mtu akimbie kilometre 8, afunge magoli zaidi ya 40, assist zaidi ya 15, hatrick za kutosha, vyenga vya kutosha afu tuzo apewe mtu kakimbia kilometre 3, kazi yake ni kusimama na kukaba tu na kwenda kufunga magoli ya vichwa?
Hapana, suluhisho ni kwa mabeki kama walivyo makipa watengenezewe tuzo zao, huwezi linganisha kazi wanayofanya Salah na Mane na kazi wanayofanya Matip na Virgil.
Usain Bolt au Tyson gay apewe tuzo yake na David Rudisha apewe tuzo yake, kuwapa malipo sawa wakimbiaji wa marathon(Messi) na hawa wa mita 200 (Virgil) si haki kabisa.