Kwa kweli jana FIFA wamechemka, mimi mpaka leo nashindwa kujuwa vigezo. Navyojuwa inaangaliwa msimu mzuri kwa mchezaji mwaka ule sio history. Ok ni kweli Messi ni mchezaji bora sana lakini hakufanya vizuri mwaka huu lakini wamempa na mbaya zaidi jana bahasha haijafunguliwa Messi kishafika nyuma ya stage je majibu yanapangwa? nisieleweke labda simkubali Messi hapana ni bora sana tu lakini sio mwaka huu. tuache huko FIFA 11 eti Marcelo kachaguliwa jamani kwa lipi? kuna full back 2 za Liverpool walikuwa bora kabisa mwaka huu. Marcelo??? team 4 za EPL zilikuwa final leo wanakuja wanasema wachezaji wawili wa Ajax sababu tu walikuwa na msimu mzuri kuisaidia Ajax nusu final sasa wale waliofikisha team zao final? Sadio Mane kaisaidia Liverpool ubingwa wa ulaya na Senegal final za Africa nje. kweli nimeamini Nike na Adidas ndio wanaushawishi mkubwa. ndio maana Ronaldo jana hata kwenda hakwenda utasema aliambiwa Messi atapewa ingekuwa VVD angeenda. FIFA watuambie tu vigezo ni nini? eti Modric sijui Marcelo kwa lipi hasa team zao wanapigwa bench hii kuwakosea heshima wachezaji wengine. Ramos alikuwa na msimu mbovu na Real eti beki bora hapana kwa maoni yangu jana sio sawa. Messi mchezaji mzuri duniani? Yes. je mwaka huu alikuwa best? NO
Mkuu unaonekanwa ulichelewa kuwaelewa hawa jamaa. Tunzo ulaya zotezipo kisiasa tu na uhalsia wa mazingira. Mimi nimekua nikikushangaeni miaka kuendelea kutoa mapovu kwa hizi tunzo na kuchukua kipima cha tunzo kama ndio ubora wa uchezaji. Most of these awards are fixed.