The Bible Fraud & Secret in the bible...!!!

The Bible Fraud & Secret in the bible...!!!

Mkuu wewe elimu yako umeisomea chuo gani rasmi ?
Ninavyojua kuanzia shule za msingi hadi vyuoni vile vya kiserikali tunajifunza mambo yaliyogunduliwa na Wazungu, ya kwetu ni kidogo mno.
Wazungu nao wanaiga lakini ni wazuri wa kujifanya kila kitu wamegundua wao,ustaarabu wa wanzo duniani,kuanzia dini na mambo mengine umeanzia Egypt,wazungu mpaka leo hii wanapinga kuwa yale magofu ya Pyramid yamejengwa na mtu mweusi..

Ukiangalia na kutafakari,Nabii Musa ambae alizaliwa Egypt nae alikuwa mweusi,Nabii Ibrahim alikwenda Egypt na kupewa mke Hahar(Hajir) mke nae alikuwa mweusi,Hagar aliezaa na nabii Ibrahimu wakamzaa Ismael,.Isa(Yesu) alikuwa mweusi,ukisoma biblia wasifu wa Isa(Yesu) ni kama wasifu wahabeshi(Waithiopa),nikisema weusi hapa namanisha na wasifu wa wahabeshi au wasomali,hawa watu ni weusi lakini wana nywele kama za manyoya ya kondoo...

Historia ya dunia kaandika mzungu kwa kujipendela yeye ili binaadamu wengine wamuone yeye bora,tafakari
 
Inaelekea aliyetoa uzi huu hata Biblia haijui, na pia hajui kwamba kuna vitabu vingi vimetungwa baadaye kwa ajili ya kupotosha.
Kwanza lazima afahamu Biblia au vitabu vilivyomo ndani mwake ilikuwaje vikapatikana na kukubalika kuwa ndio Neno la Mungu. Fuatilia kwa karibu ukiwa Mkristo au usipokuwa Mkristo cha msingi, elewa wenyewe Biblia inasemaje na kujua wakati huo ilikuwa na maana gani, ili kutafsiri katika leo. Imani haturukii bila kujua nini unaamini (hasa Ukristo). Wakristo ambao ni watu waliosoma na wamekaa katika kweli si rahisi kudanganya. (Tusichanganye na watu ambao hawaenendi Kikristo na kujjita Wakristo, watu ambao hata kusoma Biblia hawasomi, watu ambao kazi yao ni kusikiliza tu, toka kwa watu, wahubiri), watu kama hao nilirahisi kupotoshwa. Uisome uone kweli kama Yesu alikuwa mwongo, mjanja, je alikuwa na akili timamu?. Biblia ni kitabu cha kihistoria (hilo limethibitshwa), ingawa ni cha kiroho. Maeneo yote yaliyotajwa kwenye Biblia yalikuwepo wakati wake wa kuandikwa, ingawa maeneo mengine yamepotea, Wanaakelojia wanendelea kugundua maeneo hayo siku kwa siku. Usikurupe ndugu, hivyo vipo na vingi tu, lakini anayelewa juu kwanini vitabu viliandikwa na aliyeandika yukoje hawezi kustuka na hayo. Hata wazushi kuhusu Ukristo wapo hata leo na wengine wamo katika Ukristo (wanajifanya).
 
Issa ( Yesu) hakupata kuoa, wala hakupata kuwa na watoto, na wala hakuuwawa, badli walifananishiwa mfano wake na alipaa mbinguni kwa Mola wake kwa baadhi ya tafsiri
 
Mi nilisha acha kutambo tu kuingia kwenye misikiti Na makanisa, ukweli tuna leta shobo kwenye imani za watu, imani gani hadi uitwe omary au John? Ukane asili ya ukoo Na mababu zako, sijaona mzungu anaitwa gwahinda, kundabatwale, au katulebe hivyo imani nachukulia kama ni ukoloni mbaya sana.
Mkuu ushawahi kuona madawa ya hospitali yana majina yenye asili ya kiafrika?
 
Haya mambo ya copy and paste huwa yananiboa kweli kweli...
Uko sahihi mkuu.......... Nafikiri nimpe jibu la copy and paste pia ila nahisi nitakuwa narudia ujinga

Nimeamua kuachana naye tu
 
Issa ( Yesu) hakupata kuoa, wala hakupata kuwa na watoto, na wala hakuuwawa, badli walifananishiwa mfano wake na alipaa mbinguni kwa Mola wake kwa baadhi ya tafsiri
Leta ushahidi wa kimaandiko.
 
Issa ( Yesu) hakupata kuoa, wala hakupata kuwa na watoto, na wala hakuuwawa, badli walifananishiwa mfano wake na alipaa mbinguni kwa Mola wake kwa baadhi ya tafsiri
Mmekaririshwa upumbavu. Na waliowakaririsha wanajua ukweli.
 
Vitabu vyote vya dini ni uzuishi tu, si Qu'an wala Biblia...vyote ni utata mtupu. Binafsi siviamini hata kidogo kwani vimeandikwa kwa lengo la kuwaabudu wazungu, wayahudi na waarab tu. Ndiyo maana inasemwa history is always written for the victors si wafuasi, wafuasi wanabaki kuwa mabumbuwazi tu.
Waarabu lugha yao imetumika kwenye Qur'an na mtume ametoka kwao,ila sijajua mahusiano ya wazungu na ukristo ama biblia huwa yanakujaje mpaka iwe pakizungumziwa hizi dini mbili basi lazima atajwe mzungu kuhusishwa na ukristo au biblia.

Je,ni ukoloni tu ndiyo umetuathiri hivyo sababu ya kutawaliwa nao au kweli kuna mahusiano ya wazungu na ukristo?
 
wewe ndio hutumii akiri ungekuwa na akiri ungejua nilishafuatilia u feki wa dini kuja kujibashana na mimi unaonyesha na upeo mdogo wa kufikiri grow up
Mkuu umefuatilia dini zote zilizokuwepo duniani?
 
dini zote ni feki
Mkuu ukisema kitu fulani ni feki maana yake kuna original na ndiyo maana ukaweza kugundua feki yake,sasa unaweza kutuambia dini ya kweli ambayo ndiyo halisi ipo wapi au ilipotelea wapi?
 
Labda nianze kwa kukushukuru kuleta hoja yenye vielelezo vya kihistoria inayojaribu kuaminisha kuwa habari za Biblia ni hadithi za Wazungu zilizo na makosa mengi na kwamba sio za kuaminika! (HABARI ZA UONGO).
Ukweli ni Upi sasa?
Ukweli ni kwamba iwapo IMANI haikujaribiwa haiwezi kuwa thabiti na imara.
Kuna imani nyingi sana ambazo hazijawahi jaribiwa na bado zipo na watu wanazidi kuziamini imani hizo.(IMANI ZA UPOFU - Ukiihoji tu unaacha kuiamini siku hiyohiyo).

Naomba Nieleze Kidogo kuhusu Ukristo na Kitabu chake kikuu rejea ambacho ni BIBLIA.
Ni Dini pekee ambayo Kitabu chake cha Maarifa na Imani ni kimoja tu.
Dini zingine kwa mfano Dini ya Wayahudi ina kitabu zaidi ya kimoja - TORAH na TALMUD. Huezi kushiba maarifa ya imani hiyo bila kusoma kitabu cha ziada.
Hivo hivyo Uislam - Quran na HADITH.

Ukristo umepigwa vita na Watu wengi sana katika historia;Watawala(mfano NERO),Imani zilizokinyume chake,Kuchomwa kwa nakala za biblia,Kubanikwa kwa wote waliojiita Wakristo (Wafia dini ulimweguni kote - Hawa waliuwawa kwa kukiri kuwa wao ni wafuasi wa Yesu Kristo - Kanisa la kwanza) Kukatazwa kuabudu na mambo kadha wa kadha yanayofanana na hayo. Lakini mpaka leo bado ukristo ni imani pekee ambayo mafundisho yake yasipopotoshwa yanaleta Uzima na Amani sana.
Nafurahi kwa sababu Ukristo Umesemwa vibaya sana! Umetukanwa mno! Umebezwa sana! Umedharauliwa sana!
Naomba niwataje baaadhi ya waandishi maarufu sana ambao iwapo maandishi yangekuwa na nguvu yangesha uuwa Ukristo Duniani.
1. Bertrand Russel
2.Richard Dawkins
3.George Bernard Shaw
4.Karl Marx
5.C.S Lewis
6.Lee Strobel
7.Malcom Muggeridge
LIST NI NDEFU!....
Lakini cha ajabu sasa baadhi ya hawa waandishi walibadili gia angani na kuukubali Ukristo kwa Mikono Miwili.

HOJA NINI BASI JUU YA UKRISTO.
Hoja ni Ndogo sana "Kubwa sanaaaa' - YESU.
Shida ni Huyu Bwana Mkubwa - YESU.
Iwapo wangeweza Kumdiscredit YESU basi Imani ya Wakristo ingekuwa ni Bureeeeeeeeeeee.

Wanatumia Makosa madogo madogo sanaa ya Watafsiri wa Biblia - (Trivial errors and innocuous one) toka Lugha moja hadi nyingine = Kiebrania (Hebrew) - Kiyunani (Greek Septuagint) - Kilatini (Latini Vulgate) mpaka kwenye versions za kiingereza Kama vile NIV,KJV,SV na nk.

Pseudo Historical Narratives.
Ooh sijui Hadithi za Wamisri wa kale - Kabala na uongo mwingine.
Na hoja zingine nyingi ambazo kisomi "zinamashiko ya Kishule" Welevu wa kidunia sio wa kiimani( Research is only refuted by another research).
Iwapo wewe ni Mkristo wau Mwislam swali ni moja tu! Je Imani yangu inafanya unachokiamini?
- kama hamniamini Mimi basi aminini kwa kazi ninazofanya -Yesu Kristo
Faith is all about experience and revelations.
Kwa sababu binadamu wamekuwa na masikio ya kuwasha sana! hawataki kuamini Biblia basi aminini kwa kusoma Habari toka kwa Wasioamini Kristo ambao walikutana na Experience ya ajabu wakakubali.
Imani za wazazi wetu au jamii zetu ndiyo huleta athari kwenye imani zetu kwa maana nasi hufuata imani hizo,je ni dalili zipi zenye kukufanya uone ukweli kwenye imani uliyonayo?

Yapi yanakufanya ujione upo sahihi kabisa ?
 
Wazungu nao wanaiga lakini ni wazuri wa kujifanya kila kitu wamegundua wao,ustaarabu wa wanzo duniani,kuanzia dini na mambo mengine umeanzia Egypt,wazungu mpaka leo hii wanapinga kuwa yale magofu ya Pyramid yamejengwa na mtu mweusi..

Ukiangalia na kutafakari,Nabii Musa ambae alizaliwa Egypt nae alikuwa mweusi,Nabii Ibrahim alikwenda Egypt na kupewa mke Hahar(Hajir) mke nae alikuwa mweusi,Hagar aliezaa na nabii Ibrahimu wakamzaa Ismael,.Isa(Yesu) alikuwa mweusi,ukisoma biblia wasifu wa Isa(Yesu) ni kama wasifu wahabeshi(Waithiopa),nikisema weusi hapa namanisha na wasifu wa wahabeshi au wasomali,hawa watu ni weusi lakini wana nywele kama za manyoya ya kondoo...

Historia ya dunia kaandika mzungu kwa kujipendela yeye ili binaadamu wengine wamuone yeye bora,tafakari
Unafikiri waafrika hatukuandika historia kwa sababu gani?
 
Biblia na Inijili ni vitabu viwili tafauti,..Biblia ni neno la kigiriki lenya maana "Maktaba",Biblia ni mkusanyika wa vitabu 77 kwa wale wenye imani ya kikatoliki na ni mksanyika wa vitabu 66 kwa wenye imani ya nyengine kama Protestant nk..

Yesu hajawahi kuandika kitabu hata kimoja,alikuwa anahubiri watu wanaandika anayohubiri,huu mfumo umefanywa na mitume yote,Hawa akina Matayo,Marko,John nk,na wao vile vile hawakuandika chochote katika kitabu cha biblia,..

kwani katika biblia wanasema biblia kwaniaba ya Matayo au kwaniaba ya Luka,kwa maana hiyo sio wao walioandika kuna mtu au watu wameandika,vitabu vya biblia vimeandikwa na zaidi ya watu 40 wasiojulikana(anonymous)

Injili ni mfundisho(gospel) ya Isa(yesu) ambayo yamepotea,Mungu kafanya hivyo makusudi,kwasababu alijua atatuma kitabu cha mwisho kwa mwanadamu,Biblia ni maandishi ya watu zaidi ya 40,yaliyoandikwa miaka 600 baada ya kifo cha Yesu..
Uko sahihi kuhusu idadi ya vitabu vinavyotokeza biblia ila hauko sahihi kuhusu walioandika vitabu hivyo kitabu cha Mathayo kimeandikwa na mathayo mwaka 41AD, marko kimeandikwa na marko 65AD, Yohana kimeandikwa na Yohana 98AD, matendo kimeandikwa na luka mwaka 61AD na vile vitabu vya kwanza vya biblia viliandikwa na musa kuanzia mwaka 1513BC hadi1473bc...hiyo dhana kuwa vitabu viliandikwa miaka 600 baada ya Yesu kufa sio kweli kwa maana Yesu au Issa alikufa mwaka wa 33AD miaka 8 baadae Mathayo anakamilisha kitabu chake yaan mwaka 41AD.
 
Huwa najiuliza, kwanini nguvu nyingi, fedha, juhudi na maarifa ya hali ya juu yatumike kupinga uwepo wa Mungu? Kwa hali halisi kuna cha kujifunza, kuna haja ya kuyatafuta maarifa kadri mtu atakavyoweza. Kwa bahati mbaya sana kuna mabingwa wa upotoshaji, ukaaminishwa hata mambo ambayo kwa akiri ya kawaida yanatia shaka. Lengo hasa la kupinga uwepo wa Mungu kwa nguvu nyingi ni lipi? Aina inayotumika upingaji wa uwepo wa Mungu inatia shaka, ikitaka kuwaaminisha watu pengine wapotoke! Binafsi sio mtaalamu sana mambo haya, ila sidhani kama aina hiyo ya vitabu vitaniaminisha kutokuwepo kwa Mwenyezi Mungu.
 
Waarabu lugha yao imetumika kwenye Qur'an na mtume ametoka kwao,ila sijajua mahusiano ya wazungu na ukristo ama biblia huwa yanakujaje mpaka iwe pakizungumziwa hizi dini mbili basi lazima atajwe mzungu kuhusishwa na ukristo au biblia.

Je,ni ukoloni tu ndiyo umetuathiri hivyo sababu ya kutawaliwa nao au kweli kuna mahusiano ya wazungu na ukristo?

Ni ukoloni kwani wazungu ndiyo waliotumia ukristu kututawala na kutupumbaza huku wakituibia rasilimali zetu. Walifuata nyayo za waarab.
 
Back
Top Bottom