Sijaelewa unavyosema biblia ni injili unamaanisha nn? But ninachoelewa injili ni vile vile vitabu vinavyohushu mafundisho ya Yesu pamoja na mitume ambavyo vinaanzia na kitabu cha mathayo mpaka vitabu vile vya Yohana ukitoa kitabu cha ufunuo. Pia wakati Yesu anaishi hapa duniani lugha iliokua inatumika ya kimataifa ilikua ni kigiriki ndio sababu vitabu vyote vya agano jipya vimeandikwa kwa kigiriki isipokua kitabu cha Mathayo ndo kiliandikwa kwa lugha ya kiebrania...Yesu alitumia maandishi ya kiebrania ambayo ni kuanzia kitabu cha mwanzo hadi malaki vitabu vya injili havikua vimeshaandikwa Yesu akiwa hapa duniani....kwaiyo unaposikia neno biblia hiyo inamaanisha mkusanyiko wa vitabu vyote kuanzia mwanzo mpaka ufunuo.
Biblia sio Injili,Biblia ni mchanganyiko wa vitabu vilivyoandikwa na watu zaidi ya 40 wasiojulikana,Asili mia 70 yaliyomo katika Biblia ni maneno na mawazo ya Paulo,Biblia neno la Kigiriki(Biblos) maana yake maktaba..
Injili ni yale aliyokuwa anahubiri Yesu "Gospel" kwa wana wa Israel,ambayo haipo duniani,Mungu hakutaka Injili ihifadhiwe kwasababu alijua ataleta mtume mwengine,kama vile alivyomleta Yesu baada ya Musa, Injili iliteremshwa kwa wana wa Israel waliopotea tu,sio kwa binadamu wote,haya yote yameandikwa kwenye Biblia
Lugha iliyokuwa inatumika kimataifa wakati Yesu anaishi ilikuwa "
Kilatini" Lugha ya Warumi(Romans),kwa wakati huo utawala wa Kirumi(Roman Empire) ulikuwa unatawala nusu ya
Ulaya,Mashariki ya kati,Afrika kaskazini,Ugiriki ilikuwa imetawaliwa na Warumi,
Kigiriki kilikuwa sio lugha ya Kimataifa..
Lugha ya Yesu aliyokuwa anazungumza ilikuwa lugha inayoitwa
Aramaic,ni kiyahudi kilichochanganyika na Kiarabu (Jewish Palestinian
Aramaic),Yesu hajawahi
kuandika kitabu,Yesu alikuwa anahubiri,yale aliyokuwa anahubiri yalikuwa yanaandikwa na wanafunzi wake au watu walikuwa wanahudhuria vikao vyake..,Mitume yote wametumia mfumo huo kufikisha yale walitumwa na Mungu kuwafikishia Binadamu
Hao akina Matthew(Matayo),John(Yohana),Luke(Luka) na wao hawakuandika hivi vitabu vya biblia,,Unaposoma biblia unasoma "
Biblia kwa niaba ya Matayo,kwa niaba ya Luka nk" .Agano la kale ni vitabu wanavyotumia waisrael,Agano la kale ni Taurat(Torah) maana yake "sheria" kwa lugha ya Kiyahudi
Soma uzuri dini yako na historia yake uifahamu,utaiona njia ya haki,njia iliyonyooka