The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

The Bold & Nifah: Happy Six Months "Anniversary"!

Daahh the bold mie ni msomaji wako yaani kwa kifupi nafuatilia sana thread zako kila niendapo huwa nakaa nazisoma sana...mungu wajalie kila lililo jema muishi maisha marefu yenye furaha tele
 
Nimesoma uzi huu sijaumaliza kwakua nahisi wivu moyoni aisee hasa pale ulipomalizia cheupe ndo nikaumia zaidi why sikuwa ni mimi ninaemkamatia mtoto mzuri huyo ila Hongereni sana nyie watu
 
Kwa ulivyo mtaalam wa kupanga lugha kwenye story mm nitasemaje sasa.



Nifa mwenyewe mhhh sio mdogo kwenye hio IQ sasa mmekutana hapo hata mkijipanga mkaleta ID ya mtoto wenu akathibitisha tutaelewa maana sjui mnatulogezea kwanza....



Ila all in all kila la kheri kwenye mausiano yenu na tathnia yenu
 
Nimesoma uzi huu sijaumaliza kwakua nahisi wivu moyoni aisee hasa pale ulipomalizia cheupe ndo nikaumia zaidi why sikuwa ni mimi ninaemkamatia mtoto mzuri huyo ila Hongereni sana nyie watu
Acha tamaa, huyu cheupe alikuwa hapa JF muda kibao hakuna mtu aliyekuwa anamtolea macho. Hasa hasa mlikuwa mnabishana naye kwenye siasa kumuita nyumbu etc.. kumbe ni almasi.. sasa hivi tokwa tu na midenda watu ndio wameshamuweka cheupe ndani
 
Hongereni sana Bold & Nifah kwa kuwa katika mahusiano kwa muda wa miezi sita mfululizo, japo ni muda mchache kulinganisha na changamoto zilizomo katika mapenzi na maisha kwa ujumla lakini ni mwanzo mzuri, ushauri wangu ni kuwa halalisheni kwa kufuata taratibu husika ili mtambulike rasmi kwa jamii mjiepushe na uzinifu. NAWATAKIA MAISHA MAREFU YENYE KHERI NA BARAKA TELE.
Shukrani mkuu kwa kututakia kheri..


In shaa allah tuko kwenye hatua za kuhalalisha mkuu! Soon tutawapa update... And usikose tafadhali kwenye pilau
 
Nifah ni hv The Bold ni mtunzi mahiri, asije kuwa aliwaza before hajakuaproch ili ili story iwe na wahusika live, nikimaanisha wewe mwenyewe na the bold. Nataka iwe forever bond, vinginevyo,Nitasimamia adhabu yk, copy?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mkuu yani jinsi huyu mtoto alivyoniteka... Siwezi hata kujinasua! This is forever... In shaa allah
 
it is possible. mimi nimeshakutana na watu wengi tu ambao tumeanza mahusino (siyo ya kimapenzi) kwenye mitandao ya kijamii.

hongereni bwana. ila vipi kuhusu wivu? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
The Bold & Nifah,nasubiria kadi ya kuchangia na mualiko wa ubwabwa!

Swali kwa The Bold: Lile jina lako halisi (ulilopewa na wazazi wako) litabadilika? au bibie Nifah ndo atabadili jina lake kukufuata?
Sisi wote tuna majina ya kiislamu... So its good there!

And bibie nifah atabeba surname yetu mwishoni mwa jina lake kama ilivyo desturi..
 
Kila la kheri lakini naamini hamjawahi kukutana ni PM tu... Sasa cku ya kukutana nae ukakuta ni mwenzio halafu anatokea pale kwenye ukuta mrefuuu wenye maghorofa mengi ndani.. Hapo chachaaa.. Na kama ulidis kwenye post zako mmmhhh
PM??? Ilikuwa mwezi mmoja wa mwanzoni tu..

Kwa sasa we are almost living together... Yaani tuko pamoja most of the time
 
The bold/nifah hongereni sana wakuuu.ila najaribu kuvuta picture siku ya kwanza kupeana miadi ya kuonana(kama hamkuanza kwanza kutumiana pictures)hakukua na kutegeana kufika kwanza eneo la tukio?,ilikuepuka shambulio la moyo[emoji2] .

Wanyamwezi husema bhangi bhulyaa bhangi bhutumula misooo,itabidi na mimi shemeji/wifi yenu wa kiromije nimshawishi ajiunge jf[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]

I wish you the best nyie viumbe.
Unajua mimi na Nifah tulianza kupendana before hata hatujuani kiundani au mwonekano (I know its sounds strange... Ila ndio tulipendana hivyo)..
So baada ya hapo huko PM ndio tukatumiana Picha na nini... Na maelezo mengine ya kujuana kiundani inside out...


So mpaka siku tunaonana tulikuwa tayari tunajuana A-Z...


Its was one of the happiest days katika maisha... Will never forget that day!
 
Kwanza hongereni na mmefanya ionekane vitu/mahusiano yanaweza jengwa popote lakini kubwa tunaomba halali ipite ku imarisha mlichoanzisha pia nahisi upande wa "Nifah" ni "Nikah" inahusika sijui kwa Mr Bold au itakuwa kwa mkuu wa Wilaya?
Shukrani kwa pongezi mkuu..


Sisi sote ni "mujahedeen" so ni mwendo wa ubani tu kwa sheikh..
 
Daa! Safi sana nimependa namna uhusiano wenu ulivyoanza atleast mnakitu cha kusimulia, kazi mliyonayo ni kuthibitisha kwmb uhusiano unaoanzia kwenye mitandao unaweza kuleta very bold and strong familia
Inshallah mkuu... Nadhani tutakuwa mfano mzuri kwa wengine..
 
Back
Top Bottom