The bold: Waraka

The bold: Waraka

Acha movie iendelee! Pole sana Emma!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Ni mojawapo kati ya post zinauma sana nilizowahi kusoma JF, hii post ina mengi mengi ya kutufumbua macho!!!! Emma mdogo wangu JIPE MOYO UTAYASHINDA YANA MWISHO UTAYASHINDA huu wimbo wenu uliwainspire wengi na kutoka hapo mkaelekea kilele cha mafanikio, naomba wimbo huohuo ukawe faraja kwako sasa katika mapito haya unayopitia USIKATE TAMAA DHALIMU HATAISHINDA HAKI
 
hehe hakuna kitu kama hicho..mwezi wa nane tupo Iringa na helcopter watch me

Huko Iringa machangudoa kutoka nchi nzima watahamia kama wanavyohamia Dodoma. Si wameishasikia mchungaji anahonga milioni tisa na milioni kumi na nane... Watakuja mikutanoni wamejiremba kikahaba ili kumtamanisha kahaba mwenzao Gwajima. Kumbe lile zee fuska Sana, linamtanguliza mume wa mtu Dar linabaki linatafuna mkewe...
 
Nimesoma kwa makini mno huo waraka, nimejaribu kuvaa uhusika, aisee imeniuma sana. Nilipojaribu kumsikiliza katika uzi mwingine anaosema Flora amekomba kila kitu kuanzia documents hadi kapeti na mashuka yaani ndio nimezidi kuumia hadi nikahisi kutokwa chozi.
 
Huko Iringa machangudoa kutoka nchi nzima watahamia kama wanavyohamia Dodoma. Si wameishasikia mchungaji anahonga milioni tisa na milioni kumi na nane... Watakuja mikutanoni wamejiremba kikahaba ili kumtamanisha kahaba mwenzao Gwajima. Kumbe lile zee fuska Sana, linamtanguliza mume wa mtu Dar linabaki linatafuna mkewe...

mchungaji hafai huyu.....
sa hivi inabidi kuwa making sana na hawa wachungaji majina
 
ujue nn mm ningeweza kumwamini huyu jamaa kama akisema ukweli lakini anadanganya wazi; Mbasha na mkewe waliodoka na mama Gwajima na watoto wa mchungaji Gwajima kurudi Dar for xmas then wakarudi tena kilombero ambapo tuliondoka nao tarehe 30 sasa kusema flora alibaki Moro ni uongo ambao unanifanya niamoni kuwa the bold si mbasha na kama ni mbasha wanamtumia kupata data ili wazigeuze... okay sikulazimishi uamini ..lakini ndio ukweli huo... Gwajima aongei chochote maana hamna hoja ya kujibu hapo..ni uongo tu..

mbona mwanzo ulikua unang'angania Mbasha ndio bold leo umekuja kubadilika
 
na tarehe tafadhali sawa

na ni kipindi gani

na kuwe na udhibitisho kama ni kweli wanatoka moro

usije ukatupa link wapo katika gari tu sawA

maana issue ni je alirudi nae au alimua ha mchungaji akawa nae kipindi hicho

tunahitaji tujue mbivu na mbichi

mtumishi wa bwana awe salama au si salama dont logout till we make it down tonight

siwezi kukulazimisha kuamini maana ungetaka ukweli ungemuhoji the bold atoe ushahidi juu ya anayoongea... Najifunza mengi kupitia hizi story za uongo zaidi sana napata kujua kuwa hata story nyingi za wanasiasa ni uongo unaotungwa na watu wachache tu...
 
We Danganywa Tu Ila Elewa Na Atoe Jibu Kabaka Au Hakubaka, Asitake Kuonewa Huruma Kwakuunganisha Stor Za Uongo, ANGEKUA KWELI ANAJIELEWA ANGEELEZA KWANINI ALIBAKA NA SI POROJO ZAKE IZO

Kwa mimi naona hakubaka. Angekuwa amebaka dhamana isingetolewa kwa masharti rahisi. Kwa sasa angekuwa bado mahabusu. Kuna namnanamna between.
 
siwezi kukulazimisha kuamini maana ungetaka ukweli ungemuhoji the bold atoe ushahidi juu ya anayoongea... Najifunza mengi kupitia hizi story za uongo zaidi sana napata kujua kuwa hata story nyingi za wanasiasa ni uongo unaotungwa na watu wachache tu...

mkuu uongo upo na ndio unaotawala hii dunia,kumbuka story ya jana juu ya kifo cha kawambwa,mtu kajitungia tu na kuweka hewani,wapo wafungwa wengi wanaotumikia vifungo kwa makosa yasio yao ndio dunia ilivyo
 
Acha kumfundisha uoga wewe,hakuna Mtumishi wa Mungu Sampuli hii huyo ni Wakala wa Shetani.

Haswa anatumia comed mara nafufua watu misukule ya miaka kumi inaongea kama sio sanaa ni nn?


Sent from my iphone using jamii forum
 
Gwajima ni tapeli, alikuwa anadanganya watu eti ana uwezo wa kufufua misukule. wizi mtupu. sasa kaingilia wake za kondoo wake. nasikia hata yule pale mwenge wa kanisa ka EFATA aliwahi kumdanganya dada mmoja akampangishia chumba hotel moja hapa Dar eti aweze kusali na kuomba vizuri kuepuka furugu za watu, baadae akamtokea lkn baadae alimnunulia kiwanja na kumjengea nyumba.
 
Wakuu,

mimi ni mme wake dada yetu muimbaji, na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

nitapambana na nitakushinda!!!
Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo,
ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."

- The bold
Mkuu The Bold, kwanza pole dana kwa yote!.
Kiukweli nimeguswa sana!, and I think I can help somewhere somehow!.

Kwa wenye mashaka, naomba niwathibitishie "this is bonafide genuine!".

Naomba kutoa usaidizi mfupi namna ya kuipambanua "bonafide genuine" from "fake"
Unaweza kuijua tuu kwa kuusikiliza moyo wako!, listen from your heart!.
Pasco.
 
Tafadhali: mods nimejitahidi kadili niwezavyo kutotaja majin ya watu kuepuka kuviolate sheria za jf, naomba muache huu uzi!!


Wakuu,

Kwa makusudi kabisa nimekuwa nikiliepuka kujibu swali kaka mimi ni mme wake dada yetu muimbaji ama la, laiti ningekuwa ndiye ningependa yeye na mchungaji wasome hapa;

“ mchungaji, ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya ‘utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwako.

Mchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!

Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!

Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha?? Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo?????

Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa! Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!! Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!! Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!! Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!

Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani??? Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!! Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!

Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako??? How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje??? Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea??? Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda???

Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!

Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!! Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu??? Fedha??? Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe???

Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii??? Ni nini kilichokuoata mkewangu??
Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!

Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!

Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!
Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!

Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!! Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!! Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!! Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti! Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!

Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda.."


- The bold

Ingawaje Moyo Wako unavuja damu, God will make a way
 
The bold, every challenge comes with an opportunity.

Kama una access na Emma mwambie kwa muda huu apoze mawazo yake kwa kuandika kitabu juu ya maisha yake (yao) na Flora Mbasha na masahibu yaliyotokea. Nina uhakika atatengeneza faida isiyopungua milioni 20. Zitamsaidia katika kesi na zitaisaidia familia yake...

Inabidi Mbasha afanye hivyo, Lakin mpaka hapa sina uhakika tena kama ntakuja kuoa maana kwenye hili sakata nimejifunza mengi tena zaiddi nazidi kuogopeshwa with a thing the so called ndoa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ninamfahamu vizuri huyo mtu wa kwenye avatar yako hapo, he was my classmate pale Tambaza. Majina yake yanaanzia na H and B ni wewe au umeamua tu kutumia bila yeye kujua mkuu???

Tambaza mwaka gani mkuu, maana sisi ni matunda ya hiyo shule ya ukweli. Hata mimi hiyo sura si ngeni kabisa.
 
Watch "Kafara ya damu part 2" on YouTube -
https://www.youtube.com/watch?
v=XcQ4...e_gdata_player hii video inamuonyesha
Mbasha na Flora wakiwa eneo ambapo mkutano
ulihamia mara baada ya kutoka kwenye viwanja
ambavyo tulihama sio kwasababu ya maneno ya
uchochezi ni kwasababu eneo lipo karibu na
hospitali... wakasema wagonjwa wanasumbuliwa
na kelele..huyu ni muongo asilimia mia ..
jaribu kuicopy hiyo link then follow

Wagonjwa badala ya kufurahia neno la Mungu kuwa jirani yao wenyewe wanaita makelele, HAMJISHTUKII???? Mnasubiri wafe ndiyo mjifanye kuwarudisha misukule badala ya kwenda kuwaombea afya njema kabla hawajafa.

Hivi ile ishu ya mtikila muliimaliza vipi???

Ya Amina Chifupa Je???

Nyie jamaa fiksi nyingi sana, halafu eti mnakimbilia kusema tusimsemee vibaya mtumishi wa Mungu. Mungu yupi?? Huyu huyu muumba wa Mbingu na ardhi?? Wa isaka na yakobo??? Wa ibrahim??? Au mungu wa misukule???

Anaonekana ni mtumishi wa mungu kwa watu ambao hawajapewa macho ya rohoni na kulijua neno kama ninyi. Hampo huru tena. Mmefungwa na nguvu za kishirikina za kurudisha hiyo misukule.

Ibada zenu ni za promotion zaidi kuliko kuwahakikishia waumini wenu ufalme wa Mungu aliye hai. Ibada nzima mnazungumzia misukule. What i know, huwezi cheza ngoma usiyoijua i.e ni lazima mmefanywa kuwa misukule and that`s why hamna akili za kujitambua.

Mnajitahidi Kumpenda Mungu wenu kwa mioyo yenu yote na Nguvu zenu zote lakini HAMTUMII AKILI ZENU KUMPENDA MUNGU and thats why MNAANGAMIZWA NA MSIPOBADILIKA NA KUIJUA KWELI NA MAPASTOR WENU FAKE MTAZIDI KUANGAMIZWA.
 
Back
Top Bottom