The Bolsheviks, Dkt. Bashiru, Somo kwa UVCCM na CCM

Umerogwa
 
Kama huoni tofauti yoyote, basi ni kwa hakika ulikua umezimia tangu 2015 na umekuja kujifufukia 2020. Pole sana una safari ndefu sana ya kujua mambo mepesi
 
Unafahamu kwamba hata vyombo vya dola vinagawanyika?,nao wanamitazamo tofauti pia,kwani ukisikia coup imetokea unafikiri ni kwa sababu ipi?

Kila siku nasema mabadiliko ya kweli yatatokea kukitokea machafuko au nchi kupinduliwa. Lakini sioni hayo zaidi ya kuona waoga na viongozi wa dola kugombea nafasi ndani ya CCM. Box la kura haliwezi kuleta mageuzi nchi hii.
 
Nakubaliana na wewe, hakuna namna CCM inaweza kupona within 10 years. Mabadiliko yao ya ndani hayawezi tena kuwaokoa. Mipasuko imefikia hatua mbaya beyond repair.

Tutashuhudia watu wanaanza kujilipua bila uoga kuelekea 2025. Kuna upepo mbaya sana unakuja.
 
Definition ya uchawa ndio wewe.
Nchi ipo gizani , maji hakuna . Ufisadi umetamalaki.
Kipindi cha JPM hayakuepo hayo
 
Kuna wachumiA tumbo hapa Tz ,Bolshevik WA tumbo labda
 
CCM ina miaka michache sana chini ya miaka 10 kuvunjika kwa aibu sana, so vijana kama mnaweza anzeni kujiandaa na maisha bila uchawa na vipesa vidogo vidogo vya Rushwa.
 
Kama huoni tofauti yoyote, basi ni kwa hakika ulikua umezimia tangu 2015 na umekuja kujifufukia 2020. Pole sana una safari ndefu sana ya kujua mambo mepesi
Kuna kazi inafanyika mkuu tena kila kona ya TZ na ni ya maana sana. Kama wewe ni wale wale wa mitandaoni Dar huwezi kuiona na hivyo huwezi kuiheshimu pia.
 
Nimesoma Ukraine nayajua sana hayo mambo mkuu, Bolishevik ina maana ya wengi wao au 'majority' na Menshevik ina maana wachache wao au 'minority'.
Bolishevik ni wajamaa ambao hawakutaka kushirikiana na Watawala (Tsar) na wakataka hatua kali za kimapinduzi zifanyike

Menshevik walikuwa jamaa waliotaka kushirikiana (Tsar) na wakataka soft stance. the same situation is happening in CCM

Kuna wana CCM ambao ni wapebari ndani ya Chama cha kijamaa mfano ni Sera za Samia na watu wake, they are very off the CCM values and virtue na Kuna Wana CCM ambao ni wajamaa hasa ambao kwa Sasa sijaona kama Bashiru.

Tanzania wengi very poor country na Watanzia ni maskini, Bashiru ni upande wa watu wengi
 
Mkuu hawa CCM walishindwa kuiga hizo sera za kirusi. Wanaoitwa wajamaa ni mabepari wakubwa tu. Waafrika tumejawa na unafiki unaotazama maslahi zaidi.

Akiongea jukwaani ni kama mjamaa halisi lakini akishuka tu na kuanza kuishi maisha ya kawaida ni tajiri wa kutupwa.
 
Shukran. Tunahitaji ukweli huu nyakati zote. Kuna watu wanajaribu sana ku-“rationalize” uozo wa siasa za Tanzania na mifumo mikuu ya kiitikadi duniani. Hatuna kitu kama hicho. Tanzania miaka yote inaongozwa na vikundi vya kidikteta vinavyotumia chama dola (CCM) kuibia na kuhujumu taifa kwa maslahi binafsi, period. Vinategemea dola, propaganda, ujinga na uoga wa Watanzania.

Ni Nyerere pekee ndiye hakuwa mwizi au mhujumu uchumi. LAKINI ndiye aliyejenga huu mfumo mbovu wa kidikteta unaompa Rais “absolute power” akitarajia nchi siku zote itatatawaliwa na mtu wa aina yake. Wapi duniani unampata mtu ambaye hana tamaa ya utajiri binafsi? Nyerere hakuwa mtu wa kawaida tena alikuwa mdhanifu (idealist) kweli kweli! Warusi, Wachina, Scandinavians walipata tabu kumuelewa. Marekani Democrats ndio angalau walikuwa karibu naye. Lakini Republicans waliona ni mkomunisti tu.
 
Kuna kazi inafanyika mkuu tena kila kona ya TZ na ni ya maana sana. Kama wewe ni wale wale wa mitandaoni Dar huwezi kuiona na hivyo huwezi kuiheshimu pia.
Mkubwa wangu naomba nikueleze yale uliyo na shaka nayo, JPM alifanya mambo mengi sana makubwa snaa, hakuna kitu mama samia anafanya nje ya kupigana na yale ya jamaa lkn bado yanamshinda kbsa, SGR mpk leo haijaanza kazi, umeme kule stiglers ilitakiwa iwe 2022, lkn unaambiwa mpk 2024. Yan mama kaweka tozo, mikopo mingi, anahangaika sana lkn bado kufikia ile level ya JPM ni ndoto na haiwezekan kbsa huo ndio ukweli. JPM alikua RAISI bwana.. Alikua akihutubia taifa watu tunamsikiliza kwa adabu na nidhamu alikua mbele ya muda, alikua mdadisi sana, alikua na maamuzi na alionyesha njia.

Yani ukirejea uongozi wa JPM unaona kbsa raia walikua na raha sana... Walisema yanayowasibu na hatua zilichukuriwa haraka, leo hii tunalalama mbolea, maji, mifumuko ya bei, umeme, mikopo vyuoni, biashara mtaani zimeharibika sana, uhalifu umeongezeka, ufisadi, umwinyi kwa viongozi, yan nchi hata haierewk kama inaongozwa na CHADEMA, CCM AU ACT wameungana dhidi ya raia.

Enzi za CHUMA nchi kwanza ilikua na msisimko fulani ivi wa kujiamin sana unapotoka nje ya nchi...
 
Hatuwezi kumfufua ajitetee au aongoze nchi yetu zimebakia kumbukumbu. Level ya JPM kufikiwa na Samia ni maoni binafsi.

Kuna watu humu humu wanazo data nyingi tu zenye kuonyesha namna SSH anavyofanya maajabu muda huu huu wakati sisi wengine akili zimenasa kwenye kuwazia jana na mema yake ya JPM.

Kila rais ana karama zake anavyo vitu anavyoweza kufanya na vipo haviwezi kuvifanya. JPM hakwenda zaidi ya Addis Ababa hakuwa na uwezo katika sekta ya kimataifa SSH anaiweza sana sekta hiyo.

Na mahaba niue ni tatizo la baadhi yetu, siamini kama awamu ya tano hakukuwa na wizi serikalini, ulikuwepo sana tu lakini JPM alipenda na aliweza kuitawala media iwe inatoa habari ambazo anaona yeye zinafaa kuwafikia watu.
 

Umeongea ukweli mtupu...

It is very unfortunate kuna mtanzania mwenzako yuko tayari kukupiga mawe kwa ukweli uliousema...
 
Hizo media gan ss unazohisi hazikuongea ukweli, ni wakosefu wa maarifa tu wanaoamin mtu akifa anatakiwa kusahaulika, mbali na kwamba kafa lkn kuishi mema na yale tunayoamin yamesaidia jamii zetu sio vibaya

Sio maoni binafsi kuwa SAMAI hana uwezo kama wa JPM. ni ukwel uliobayana, wala hatutaki hata sababu za Covid sijui vita ili nchi ikae sawa inahitaji sana viongozi shupavu ni dhahir tunahitaj viongozi wadadisi viongozi wenye misimamo na wanaoweza kuchukua hatua.

Inawezekana unampenda SAMAI kwa sababu zako binafsi hilo siwez kuliingilia kwasbb upendo upo moyoni.
Tukitaka tu kuweka hoja mezani ni kwel tupu JPM alikua mbali sana kiuwezo ukimringanisha na bi mkubwa uwezo tu wa kuongoza.

JPM.
NDEGE
SGR
BUS TERMINAL
TARMAC ROADS
DOM CAPITAL CITY
REFERAL HOSPITAL
BRIDGEs
Nyerere dam
Oil pipe line.

Kusafir safir hakujawah kuleta maendeleo kbsa, jamaa hakua akisafir na tulion impact yake, ni kama ilivyo wahi kuwa enzi za SOKOINE.

Kila mmoja anaubora wake na madhaifu yake. Lkn hauwez kufananisha ubora wa JPM na SAMIA. naamin hata mama anaweza kukubali haya.

Kama tutampata BASHIRU anaweza kutusaidia kuturudisha kwenye mstari wa JPM na tukasau upigaji na uchawa wa kijinga na kuliinua taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…