I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
THE BOYS drama ya kimarekani inayohusisha masuperheros au (Mashujaa kwa waswahili). Drama hii inaelezea Superheroes wenye ushawishi kwa umma waliyejiwekeza katika (siasa) wanasiasa, na wakati mwingine hata kuheshimiwa kama miungu.
Lakini hapohapo kuna kundi la ambao wanatumia nguvu zao kwa manufaa ya raia wa kawaida na wengine kujiweka juu ya wote hata juu ya sheria. Je, ni nini kinatokea pale mashujaa wanapofanya uhuni na kuanza kutumia vibaya madaraka yao kwa manufaa yao? Wakati huohuo kikundi kidogo cha watu wasio na uwezo dhidi ya hawa wenye nguvu kubwa, walichojipa jina la "the Boys" wanaanza harakati zao za kishujaa kufichua ukweli kuhusu kundi la superhero wanaojipa ukuu kwa kuficha ukweli wa maovu yao kupitia nguvu za kipropaganda na kiserikali wanaojiita "the seven" chini ya kampuni inayojihusisha nao inayoitwa Vought, kampuni inayotumia nguvu nyingi za kiserikali na kipesa katika kuficha siri zao chafu.