The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Ogah,
Nakwambia kuna vitu ambavyo hata havieleweki kisawasawa!.. sheria moja inapinga nyingine na sielewi ipi inatangulia. Mara utasikia Sheria ya fedha, Sheria ya Kodi na mapato, sheria ya Madini n.k. ambazo alizitumia wakati uleee wa Richmond na tukabishana sana humu kuhusu sheria ipi inatangulia.. mwisho wake hakuna cha sheria wala mjomba wake ni kwamba tulipigwa bao.
Pale Mheshimiwa wetu aliposema Zitto Kabwe amechanganya sheria mbili tofauti (zinazopingana) ina maana kuna kimchezo kinatembea hapa.. inakuwaje sheria mbili ziwe zinapingana ktk mradi mmoja wa Madini, yaani wataalam wetu ktk madini wana sheria tofauti zinatofautiana na Fedha au Kodi na mapato ktk mradi mmoja! Hawa Kamati ya Ushauri wataweza vipi kutoa ushauri wa haki ikiwa hakuna njia moja tu inayoeleweka kisheria.
Labda sikusoma vizuri lakini mjomba inabidi nikubali kitu kimoja.. Uhuni umetumika sana kama ilivyokuwa ktk Richmond na Rada!
 
Tanzania Njema,

Umeona mjadala ulivyonoga??? Ndio tunavyopenda.

Zitto kakosea, Karamagi naye hakupatia ktk majibu yake ila alikuwa mjanja sana kujibu na kuwanunua wabunge kwenye majibu yake, halafu inaelekea ulikuwa ni mkakati uliopangwa.

Kwa kifupi kwa maoni yangu, Zitto alikosea ila adhabu ni kubwa mnoooo!!

Asante

FD
 
Fikiraduni ,

Ni vigezo gani ulivyotumia kusema zito alikosea ?
 
Aliteleza kutumia neno "amedanganya" maana hapo ndipo walipo-capitalize. Na kama wangeishia katika huo mjadala bila ya kuingiza kumsimisha ubunge Zitto basi mechi ingekuwa ngumu kwa watanzania kuamua wapi kuna ukweli. Wangeachwa juu juu tu.

La kumsimamisha na maneno ya kishabiki ya wakina MALECELA, MUDHIHIR na wale vijana wenzangu ndipo wakaingia mkenge kichwakichwa wakidhani wanammaliza Zitto.

Hivyo mwisho wa gemu kisiasa ni kuwa wamejipiga bao la kisigino na Zitto ameibuka mshindi....

Ni vigumu kumweleza mtanzania kuwa eti kuna kuzingatia maslahi ya kitaifa katika mikataba yetu ya madini. Lakini Zaidi kumsimamisha ubunge kijana mdogo aliyethubutu kusema wazi kuwa wanakwiba ni sawasawa na kazi anayofanya muongomuongo humu. Kukejeli madhila ya watanzania.....wamewatia ###### waliojiamulia kulala.....

Tanzanianjema
 
Pole. Mimi sikuwa natazama kujieleza. Kushabikia watu kwa kujieleza ndio kumetufikisha hapa tulipo. Nilisoma hoja kumi na moja za Zitto, nikasoma majibu ya Karamagi kwa kipengele kimoja kimoja cha hoja za Zitto, nikaangalia na viambatanisho vya Karamagi. Nika-conclude kwamba Zitto alikuwa anatuhadaa na alikurupuka kutafuta umaarufu.

Sasa, kwenye kumfungia Ubunge, nilisema toka jana kwamba I thought it was a bad idea. The fact that ameonekana muongo ingetosha. Lakini, well, Bunge lina kanuni nyingi kuliko kanisa.

Jamani mie nadhani si kweli kuwa kusoma na kusikiliza kuna tofauti kwa jinsi Bunge linavyoendeshwa, kwani kilichoandikwa ndicho kilichoelezwa na pande zote mbili na kwa kanuni zao za kibunge huruhusiwi kutoa kichwani hiyo hoja binafsi, una i-table mezani kwa spika, halafu mnaanza kupambana kwa mlichofanya utafiti(mlichoandika). Na kama mtakumbuka wakati wizara ya foreign affairs iliposoma budget yake, msemaji wa kambi ya upinzani alizuiwa kusoma kwa kuwa alichokuwa anasoma si kile kilichokuwa tabled yaani aliongeza manjonjo yake na spika akampiga stop na kumtaka kuendelea na kile alicho table. Tuwe wa kweli katika kujadili hoja. Yaelekea Mugongo Mugongo ana hoja binafsi na Zitto, declare your interest plz!!!
 
MAREKEBISHO KICHWA CHA HABARI

Hoja ya Zitto yatupwa; asimamishwa KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

TUWE WAZALENDO KIDOGO TUSIANDIKE NA KUCHANGIA HOJA KWA ITIKADI TANZANIA YOTE NI YETU NA ZITTO TUNAOMBA UNAPOJIBU HOJA USITUMIE MICHANGO YA MITANDAO KAMA FORUMS AU CHATROOMS FANYIA TAFITI MAJIBU YAKO AU ULIZA KABDA HUJAKURUPUKA

AHSANTE

Bado nasisititiza kuwa Zitto hajakurupuka kwa maoni yangu, hakupewa nafasi ya kuthibitisha kinachodaiwa kuwa kasema UONGO. Ndugu zangu tukumbuke waliosimamishwa kabla ya Zitto, kina Penzi Changa, (wale wabunge wa CUF waliofanya ulaghai na kujipatia passport za watu waliojidai kuwa ni wake zao), pia kina kitine, ndassa kwa ku-forge minutes za kikao kuwa mke wa kitine kafutiwa deni la dola kadhaa alizotumbua huko CANADA, na mwingine ni Mrema kwa issue ya 900 ml na mwingine ni Ndesamburo, halikadhalika Ngawaiya nae, wote hawa kwa wakati wa kesi zao walipewa nafasi ya kujitetea, Why not kwa Zitto liwe suala zito la kumtaka au kumpa muda wa kujitetea kwa analosema, tuache personal interest, na kama una interest katika jambo linalojadiliwa katika forum, plz declare interest first then tusonge mbele!!!
 
Mimi nilivyoona ni kuwa majibu ya Karamagi kweli yalikuwa yamenyooka kiasi kuwa hoja za Zitto zilionekana kuwa hazikufanyiwa maandalizi ya kutosha. Inaelekea aliyaandaa majibu yale kwa muda wa kutosha.
Hata hivyo ninapoyapitia kwa makini majibu yale dhidi ya hoja Zitto na kuchambua facts said:
Sasa Kichuguu kama bado hujazipitia hizo sheria za madini na za fedha,ni vipi umeweza kuzichambua facts kama unavyodai? ni kipi usichokubaliana nacho katika majibu ya waziri?
 
waziri karamagi anasema............

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Spika naomba kuwasilisha kwako vielelezo vya ushahidi wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.

Ukiskia.......UMAFIA ndio huo hapo juu!!

Ogah, Nakuwa na wasowasi kwani JK ni kipindi hiki alinena tanzania hatuna wataalamu wa mikataba sasa nani aliandaa hii mikataba?
 
Yaani Wbunge wetu wamepoteza opportunity ya ajabu- Kuunda tume kuchunguza nani muongo katia ya Waziri Karamagi na Mhe. Zitto.

Kumbe hawa Wabunge wa CCM wanaunga mkono hizi siri za mikataba ya madini. Nimekunguwazwa sana, kama wangekuwa wakweli na wanaitakia nchi hii mustakabali mwema hiyo ilikuwa ni good opportunity ya kuungalia huo mkataba vizuri, kumbe wanapiga kelel bure kutudanganya Watanzania. Wamelishwa yamini, wako tayari ku-support uozo kwa kulishwa carrot na Serikali.

Kwang mimi kama tume ingeundwa, whatever the judgement after matokeo ya uchunguzi wa tume ya Bunge ningefurahi sana; lakini kwa kukwepa kuunda tume basi kuna jambo linafichwa na linajulikana. Bado naamini Zitto amesema ukweli vinginevyo tume ingeundwa na matoke ya uchunguzi wa Tume hiyo nadhani yangebadili mustakablai mzima wa nchi hii, kitu ambacho Wakubwa wetu wanakijua na ndiyo maana wamembania Zitto!

Wana JF, serikali imeshituka ndiyo maana wameizima hoja ya Zitto, tungeona mengi na pengine mwisho wa Walanchi hawa ungefika.

Umesema vyema. Mi kuna jambo silielewi kuhusu baadhi ya watu humu. Ebu wekeni pembeni personal interest zenu za ccm v/s chadema, au karamagi v/s zitto then muwe wakweli kwa nafsi zenu, nini hasa mnachosupport, nchi hii kuendelea kutapeliwa na wageni kumaliza madini yetu kiulaini tukiwa tunaangalia na watu tunabishana sisi wenyewe kwamba ni right/wrong? THINK INSTEAD OF USHABIKI TU.
 
Tanzania Njema,

Umeona mjadala ulivyonoga??? Ndio tunavyopenda.

Zitto kakosea, Karamagi naye hakupatia ktk majibu yake ila alikuwa mjanja sana kujibu na kuwanunua wabunge kwenye majibu yake, halafu inaelekea ulikuwa ni mkakati uliopangwa.

Kwa kifupi kwa maoni yangu, Zitto alikosea ila adhabu ni kubwa mnoooo!!

Asante

FD

Hivi Zitto amekosea wapi lakini?mbona ukiangalie zile hoja zake ni kwamba jamaa alikuwa anahoji kuhusu usahihi na usafi wa huo mkataba? kwa kawaida mambo hayo huwa yanajibiwa watu wakiridhika basi kikao kinasonga mbele, enzi zile za kina Mrema walikuwa wanahoji kishenzi Bungeni na badala ya kusimamishwa hata uwaziri wanapewa. Mhh! Bongo kwa ubabe undava ndio wenyewe, yaani issue ya demokrasia Tanzania is a hopeless one. Lakini tutafika tu, hata kama itachukua miaka 30, ilimradi tu tusimwage damu.
 
1. Hii mpya- ukiwa Mbunge ukihoji Waziri na kama una wasiwasi2 na jambo- hata kama unataka ufafanuzi! Lazima uadhibiwe na usimamishwe????

2. Hii mpya- kwa hiyo Serikali isihojiwe na Wabunge- na wasikae waonyeshe wasi2 laa sivyo- utafuangiwa???

3. Waungwana- mko hapo? Logic na hekima ya Bunge la Tanzania liko wapi? Sasa serikali linaanza udictata na kuwafunga Wabunge midomo?

4. Isije ikatokea sasa Mbunge usipopiga makofi- ukaangaliwa na jicho mbaya ukafungiwa! Mimi siko CHADEMA wala CCM ila kama Mtanzania- fairness iko wapi?

5. CCM yenye wabunge wengi kiasi hicho haina haja kuwaonea wapinzania walio wachache! Otherwise haina haja kuwa na Upinzani kwa sasa! Kumsimamisha Zitto siyo fair!


Mzalendo halisi hapo nakuunga mkona moja kwa moja, hivi mbona zamani hata enzi za chama kimoja, ilikuwa kama hatumsikii mbunge wetu redioni akiihoji serikali basi tunaona kama ni anazembea? Sasa leo hii inakuwaje kukaa kimya na kupiga makofi ndio chati?

Na nchi itaendeleaje kama hamna debate za aina yoyote mahojiano n.k? sasa kama mawaziri hawawezi kuulizwa watetee shughuli zao si watafanya watakalo? na kuipeleka nchi wanavyotaka?

Imagine Malecela ndie angekuwa raisi wetu pale ingekuwaje? hivi mzee wa umri ule si ndio kwanza alitakiwa atumie busara? maana mimi sijawahi kusikia Babu akichapa viboko wajukuu, yeye huwa ni mtu mtulivu wa kugawa busara na kusolve mambo ki-style, sasa yeye na ubabe-ubabe wake na kutoa maonyo ya vitisho kama vile mbeba zege? wakati alishatuhakikishia kuwa yeye sio mbeba zege?
 
Ila Zitto amefanya jambo kubwa sana kwa Tanzania.Nadhani tungekua na baraza huru la vijana basi na sisi tungekua na nguvu kubwa ya kulihoji bunge kwa nguvu zote.Kwa hali hii inayoendelea ingawa siombi jambo hilo litokee,ipo siku watu watasimama kwa nguvu kudai uhuru wao au kudai mamlaka yetu kwa nguvu kwani bunge limekua chombo cha kutuhujumu sisi wenyewe.Kwanini suala la MALIMA vs MENGI, Malima hakupewa adhabu kali ingawa alijulikana kabisa ameongopa na still katika solve hiyo ishu yao kodi zetu mamillion yakapotea.Leo hii Zitto anaongea juu ya Wafisadi,Wala rushwa na wahujumu uchumi wa nchi yetu anaadhibiwa pasipo kufuata taratibu.
Bado wanaibuka vichwa vya panzi huku ka Mugongo wanatetea bila kuweka interest za taifa mbele na Bado unajiita mtanzania.SHAME ON YOU!You dont have a right to call yourself a Tanzanian if you cant save Maslahi ya Tanzania.Oops,give me a brake!
NASEMA IPO SIKU.
 
Mzalendo halisi hapo nakuunga mkona moja kwa moja, hivi mbona zamani hata enzi za chama kimoja, ilikuwa kama hatumsikii mbunge wetu redioni akiihoji serikali basi tunaona kama ni anazembea? Sasa leo hii inakuwaje kukaa kimya na kupiga makofi ndio chati?

Na nchi itaendeleaje kama hamna debate za aina yoyote mahojiano n.k? sasa kama mawaziri hawawezi kuulizwa watetee shughuli zao si watafanya watakalo? na kuipeleka nchi wanavyotaka?

Imagine Malecela ndie angekuwa raisi wetu pale ingekuwaje? hivi mzee wa umri ule si ndio kwanza alitakiwa atumie busara? maana mimi sijawahi kusikia Babu akichapa viboko wajukuu, yeye huwa ni mtu mtulivu wa kugawa busara na kusolve mambo ki-style, sasa yeye na ubabe-ubabe wake na kutoa maonyo ya vitisho kama vile mbeba zege? wakati alishatuhakikishia kuwa yeye sio mbeba zege?
Pedro,
So interesting!!!! Uzee ni hekima na busara- ila sii wezee wote wana maamuzi ya hekima na busara!
 
Katika kusoma document ya Zitto, naona hoja yake ya msingi ilikuwa ni kwa nini Nazir alisaini mkataba mpya huku kukiwa na agizo la Rais la kusimamisha usainiji wa mikataba mipya (moratorium) hadi pale zile kasoro zilikuwepo katika mikataba ya zamani ziwe zimerekebiswa. Kwa hiyo kamati hapa ilipaswa kuchunguza mambo angalau matatu:

i) kama ile moratorium ya Rais ilishaondolewa na kwa mtindo upi ukizingatia kwamba aliitoa katika kadamnasi tena kupitia bungeni
ii) kama mktaba mpya uliosaniwa hauna kasoro zilizokuwepo katika mikataba ya zamani
iii) kama kulikuwa na shinikizo la maslahi binafsi katika uharaka wa kusaini ule mkataba

Sasa alichofanya Nazir katika kujibu hii hoja ya msingi ni kutoa faida zinazotokana na kusainiwa kwa huu mkataba mpya. Hii ni hoja dhaifu kwa sababu kwa vyovyote vile hata kama mapato tutakayopata yana thamani ya mbingu hayawezi kuhalalisha kama makosa yalifanyika.

Kimsingi, hoja zote alizotoa Zitto ni debatable and arguable with a small piece of intellectualism. Sijaona hii hoja ya kwamba amedanganya imetoka wapi. Yeye ameraise doubts zake,ilikuwa wajibu wa bunge na serikali kumtoa huo wasiwasi. Kama wabunge wangeamua kujadili hoja mbili zilizowasiliswa pale bungeni na Zitto na Nazir on the basis of the merits of the two presentations, yote yangeisha na pengine pasingekuwa na haja ya kuunda kamati achilia mbali kumsimamisha Zitto ubunge. Lakini tatizo lilopo sasa ni hawa wenzetu wabunge wa CCM kutanguliza uccm katika kila jambo kuliko akili zao, wananchi na nchi kwa ujumla. Ndio nikasema hiki chama ni kama devil's workshop, kila aingiapo huko ajue kwamba ataubeba tu ushetani kwa sababu evil is infectious and infects badly and so pervasively.

Hata hivyo tushukuru sana Mungu kwamba jambo hili limetokea maana sasa watanzania wameanza kujutia uamuzi wa kurundika madaraka makubwa mikononi mwa wachache yaani CCM. Hapa ndipo sasa ule msemo kwamba 'power corrupts and absolute power corrupts absolutely' unapoingia. Hawa wenzetu wa CCM wamelewa madaraka, tena madaraka makubwa yamewalewesha hasa kiasi kwamba hawasikii, hawaoni wala kunusa. Mifumo yao ya fahamu yote imezibwa kabisa. Ndio maana leo wananchi wote wanashangaa ule uamuzi wa bunge wa kumfungia Zitto lakini viongozi wa CCM nao wanawashangaa wananchi kwa kumkumbatia Zitto. Wamelewa hawa, madaraka yameziba mifumo yao ya fahamu hawawezi kuona, kusikia wala kunusa tena!

Katika hali ya kawaida ni vigumu kupata kile wananchi wanalilia katika bunge letu kama tutaendelea kuchagua wabunge wengi kutoka chama kimoja, lazima ku-balance kama tunataka demokrasia. Hata kama ikitokea chadema tukachaguliwa kwa wingi wa wabunge kama walivyo wa CCM haitakuwa rahisi kukwepa haya tunayoyaona leo. Ndio kusema we need some kind of control katika kushamirisha demokrasia na kuona maana ya bunge.

Kampeni zetu za sasa zingelenga katika kuhakikisha kwamba come 2010 hakuna chama kinacho-dominate bunge as overwhelmingly as is with the situation now.
 
waziri karamagi anasema............

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Mkataba kusainiwa Uingereza, kama nilivyolielezea Bunge lako Tukufu wakati nahitimisha hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2007/08, mkataba huo uliandaliwa Tanzania na wataalamu wetu na ukapitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa ikiwa ni pamoja na kuidhinishwa na Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining Advisory Committee) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mhe. Spika naomba kuwasilisha kwako vielelezo vya ushahidi wa kauli yangu hii. Vile vile uamuzi wa kuingiza mradi wa Buzwagi kwenye miradi ya Barrick Gold Corporation ambayo ni kampuni mama ulihitajika kufanyika kabla ya Machi, 2007, vinginevyo fursa ya uwekezaji katika mradi huu ingepotea.

Ukiskia.......UMAFIA ndio huo hapo juu!!

Je ile tulio ingizwa mkenge ya Mwanzo haikufuata taratibuu, naona majibu ya ka-ramagi yana zuwa maswali mengi zaidi.
 
Nimesikia ofisi ya bunge imetoa onyo kwa vikundi vya kupigania haki za binadamu kuwa makini kutowapotosha wananchi juu ya sakata la kusimamishwa kwa Zitto. Kulikoni bwana katibu wa bunge?
 
Nimesikia ofisi ya bunge imetoa onyo kwa vikundi vya kupigania haki za binadamu kuwa makini kutowapotosha wananchi juu ya sakata la kusimamishwa kwa Zitto. Kulikoni bwana katibu wa bunge?
Bunge wanakosea,
Wananchi wako huru kumuunga mkono Zitto. Maana yake ni kuwa- wananchi wasiwe na uhuru kuhoji maamuzi wa Bunge? Huu sii udictator? Hii habari ipo Mwananchi ya kesho. Hii inazidi kumpandisha Zitto na CHADEMA kisiasa.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=1161
 
Back
Top Bottom