The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Nyani Ngabu,
Kusema kweli mimi ni mmoja kati ya wale waliomshabikia JK ktk Uchaguzi uliopita. Lakini kitu kimoja nakuomba uzingatie ni kwamba tulivutiwa na uzuri wa sura, Kijana na mwana harakati kutoka chuo Kikuu. Kisha muhimu zaidi kwangu ni kwamba tuliambiwa huyu JK alikuwa kipenzi kikubwa cha mwalimu isipokuwa Umri wake tu ndio ulikuwa shaka kubwa la mwalimu kama alivyomtolea nje Salim A Salim wakati wa Mwinyi..... Mkombozi amekuja, hata makanisa na misikiti ilitupa salaam.
Kwa hiyo nilitegemea mengi dhidi ya Mkapa yangetokea na hasa hii mikataba ya Uongo!.. Zuga kubwa alokuja nalo JK lilikuwa kuhusu Mali zetu na hasa madini..
Hakuna Mdanganyika hata mmoja ambaye hakuvutiwa na salaam hizo na kama kuna mtu anayeweza kuleta mabadiliko basi mwanajeshi huyu ndio pekee niliona kuwa choice yangu kati ya wagombea...kumbuka pia Mwaikambo na Kombe walikuwa watu wake wa karibu, kwa hiyo nilikiona kisasi against the Mafia!
Well, I was wrong!, mke ndio kisha ingia ndani kinachofuata ni kutafuta mbinu za Kumtalakia. Moja ya mbinu zangu nimeanza uhusiano wa karibu na familia nyingine - Chadema!

Angalau wewe umekiri kuwa ulivutiwa na sura na tetesi kuwa alikuwa na endorsement ya Mwalimu badala ya kuangalia "issues" na yeye anasimama wapi. Hiyo ua ujana mimi siikubali. Kikwete siyo kijana. Tatizo letu nadhani ni hili: sisi tunazingatia mno ahadi badala ya rekodi....na matokeo yake ndio haya tunayaona sasa.
 
Nyani Ngabu,

Mara nyingi record pia huwa haielezi kitu kwani Uongozi bora hatokani na mambo mengi tunayo yatazamaktk records. Ukitazama nchi za wenzetu hata maisha ya mgombea (private life) huwa yanatazamwa wakati Bongo tunasema havihusiani.
Viongozi wazuri duniani (great leaders) wengi hawana record kama tunayoitazama sisi Tanzania kwani mtu kama Blair, Steven Harper na wengineo wengi tu hawakuwa na record nzito ya Uongozi na pengine hawakujulikana kabisa miaka mitano tu nyuma ya ugombeaji wao. Hawa wamepita kutokana na record za misimamo yao ndani ya vyama kwanza na pili mrengo na sera za chama kufuatia hotuba zao kwa wananchi . Na kikubwa zaidi ni kile wanachokiuza kwa wananchi ndio maana hawa jamaa lazima wakutane na wananchi kila kona kujiuza.
Tanzania hatuna kabisa mfumo huo ndani ya vyama na kitaifa kama unakumbuka JK aliwatolea nje akina Lipumba na Freeman. Na laukama wangeweka vitimoto kati ya wagombea watano wa CCM kwa wananchi nadhani tungekuwa na kingozi mwingine kabisa!.
Kusema kweli kutokana na mabadiliko ya kisiasa nchi, inabidi tufuate utaratibu unaokubalika ktk mfumo huu wa vyama vingi, na gharama zake inakuwa rahisi kichama ama Kitaifa kwani wote wanakuwepo ktk Kanda hizi wakati mmoja. Badala ya kutembelea Mikoa yote hawa viongozi wanaweza kwenda ktk Kanda (majimbo) yetu manane. Na kujianika kwao ktk Luninga na redio kutaweza kutusaidia wengi kuwafahamu watu hawa.

Tulimchagua JK bila kumjua wala kufahamu uwezo wake wa kufikiria haraka pindi swali zito linapohojiwa. kwa hiyo usitulaumu sana zaidi ya kanuni zetu kuwa mbovu, mara nyingi tunapenda kuwarushia wananchi lawama pale sheria ama kanuni zimewafunga kamba ya shingo. Vigumu sana kuwa na uchaguzi mzuri wa mke kama huna ruhusa ya kuendesha mapenzi kwanza kwani dunia ya leo sio ile ya babu zetu.
Hata wao CCM inabidi wafanye mabadiliko haya ya kutoruhusu Kamati kuu kuchagua mgombea na kuwaachia wanachama wa chama hicho kuchagua kati ya walio sajili tena baada ya hotuba zao na kujibu maswali ya wanachama.
 
Unajua mimi nawashangaa hawa watu waliomshabikia Kikwete tokea mwanzoni na sasa wanaanza kum-second guess. Swali langu kwao ni nini kilichowafanya wamshabikie namna hiyo? Kwenye nchi za wenzetu watu huangalia rekodi yako, yale uliyokwishayafanya katika nafasi za uongozi ulizowahi kushika na kuamua wakushabikie au la. Sasa sijui rekodi ya Kikwete kabla ya kuukwaa uraisi ilikuwaje....kuna mtu anayeijua?

Wewe fikiria, mtu toka 'Tanu Youth League,' na kupitia ngazi zote alizopitia katika chama hicho na CCM, hadi kuingia katika serikali kwa nyadhifa mbalimbali, hadi uwaziri kwa miaka yote ile. Na usisahau, watu hawakupata hata chembe ya fununu ya maovu aliyoyafanya huyu bwana wakati wote huo. Kama kulikuwa na mahekalu kule Bagamoyo au Lugoba yote hayo wengi hatukuyajua.

Sasa chukulia timu ile iliyoshiriki katika mchujo wa chama na taratibu zao za kipuuzi, ndio tukaletewa hao tulioletewa; akina Salim wakadondoshwa kwa mizengwe.

Na zaidi ya yote, angalia ile Ilani ya uchaguzi iliyotumika, kweli kuna mtu asiyependa hayo yaliyokuwa yanauzwa kwa kura? Na ukikumbuka historia ya huyu bwana iliyokuwa inaonekana kutokuwa na matatizo makubwa. Wengi tulamini, kama yupo mtu anayeweza kuisimamia na kuitimiza ile "Ilani' ni huyu.

Ushamba wa vyombo vya habari vya hapa kwetu ni kwamba hawana msukumo wa kuchimbua ukweli unaomhusu mtu anayegombea nafasi kubwa ya uongozi ili watu waweze kuwana mwanga wa yupi wamchague kwa sifa za kweli alizonazo. Badala yake wao kazi yao ni kupiga majungu kwa kupewa peremende.

Majuto ni mjukuu: sasa tunajiuliza, hivi ilikuwaje hata tukashindwa kuhoji na kufuatilia rekod ya utendaji kazi wa huyu mtu katika zile wizara alizowahi kuziendesha? Labda hilo lingetupatia mwanga mapema.

Kinachoumiza zaidi, ni huko kunadi mali ya nchi yetu bila ya kuwa na uangalifu unaohitajika. Yeye ndie mtu pekee tunayemtegemea kuwa mali ya taifa letu haitasombwa bure pasipo kutuletea ahueni kidogo katika maisha ya watu wetu.

Bado ninashindwa kuamini kuwa hiyo sio dhamira aliyonayo Kikwete pia. Kama analipa madeni ya fadhira za uchaguzi kwa kusambaza mali zetu, hapo hatukubaliani naye hata kidogo. Na ingekuwa vigumu kutabiri kuwa hivyo ndivyo angegeukia baada ya kuukwa urahisi.

You are right; people should look at the record of performance to judge an individual's ability.
 
Wewe fikiria, mtu toka 'Tanu Youth League,' na kupitia ngazi zote alizopitia katika chama hicho na CCM, hadi kuingia katika serikali kwa nyadhifa mbalimbali, hadi uwaziri kwa miaka yote ile. Na usisahau, watu hawakupata hata chembe ya fununu ya maovu aliyoyafanya huyu bwana wakati wote huo. Kama kulikuwa na mahekalu kule Bagamoyo au Lugoba yote hayo wengi hatukuyajua.

Bado ninashindwa kuamini kuwa hiyo sio dhamira aliyonayo Kikwete pia. Kama analipa madeni ya fadhira za uchaguzi kwa kusambaza mali zetu, hapo hatukubaliani naye hata kidogo. Na ingekuwa vigumu kutabiri kuwa hivyo ndivyo angegeukia baada ya kuukwa urahisi.

Kalamu ulicho sema ni kweli kabisa!
Nikiri ukweli kwamba binafsi nilikuwa kati ya wale walio mshabikia sana muungwana, yaani sasa hivi nimekata tamaa mno, siamini ninacho kiona na kukisikia juu yake!

'AMA KWELI UMDHANIAYE NDIYE KUMBE SIYE' Jamaa Mungu kamjali kipaji cha usanii na yaani kwa kumwaga ahadi na maneno mazuri ya kutia tumaini ambayo huweza teka akili za watu. Kweli alituteka sana walio wengi, na sasa hivi wengi bado tumepigwa na butwaa!tupo gizani!

Labda tusubili hiyo Nuru ya Zitto inayo anza tuangazia kwa mbali pengine itaamsha matumaini yetu yaliyo kwisha potea.
 
THISDAY REPORTER
Kahama

TANZANIANS from all walks of life are now apparently becoming much more aware, and even resentful, of the manner in which the country’s vast mineral wealth is not being equitably used to improve their standard of living - but more to the benefit of foreign investors and just a few, privileged nationals

This was the message that greeted President Jakaya Kikwete on his visit to at least two lucrative gold mining projects as part of his tour of Shinyanga Region this week.

In a sequence of events with little or no direct precedent in the country’s history, the president’s motorcade was slowed down to virtual standstill and blocked from proceeding by hundreds of disgruntled villagers on at least three separate occasions.

And each time, it was clear that the mobs of swarming villagers had no intention of allowing the presidential convoy to pass until their grievances were heard.

On Tuesday, the residents of Kakola, Segese, and Ntobo Villages in Msalala Ward, Kahama District took it in turns to hit the dirt road in droves, surround the passing motorcade and stop it in its tracks.

This was along the route that Mr Kikwete and his delegation took to get from the Bulyanhulu Gold Mine to Buzwagi Village, where the president was to inaugurate a Barrick Gold Corporation project for the construction of new local community houses.

What he witnessed was waves upon waves of disgruntled villagers, many of them with placards in hand, complaining about insufficient local community benefits from the gold mines owned by multinational mining giants like Barrick Gold.

Mr Kikwete was bombarded with questions regarding the continuing absence of basic social services like access to electricity and clean drinking water, the persistently poor roads and the lack of enough job opportunities to go round ? despite the abiding presence and open exploitation of abundant gold resources under the very land on which they live and survive.

At Kakola, the village closest to the giant Bulyanhulu Gold Mine owned by Barrick Gold, the president was told that local residents saw little or no trickle-down effect from the mine’s reported disbursements of $200,000 (approx. 260m/-) each year to the Kahama District Council for the improvement of social services.

’’We have decided to block the (presidential) convoy so that maybe the president can help us. Our own MP has abandoned us since we voted him into office,’’ said one of the villagers when approached for comment by THISDAY.

The MP in question is Ezekiel Maige (CCM) of Msalala constituency where the Bulyanhulu mine is located. However, Buzwagi is in Kahama constituency, whose legislator James Lembeli is on record as having expressed doubts in parliament about the controversial Buzwagi Gold Mine contract signed between Barrick Gold officials and Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi in London in February this year.

Lembeli, who won his seat on a ruling CCM party ticket, queried why the contract was signed ’in secret’ by Karamagi, and asserted that residents of the surrounding villages as well as himself as the area MP were kept in the dark the whole time.

Meanwhile, other villagers along the Bulyanhulu-Buzwagi route expressed confidence in President Kikwete, but declared that his key aides in government were letting him down.

Apart from complaining about the general lack of benefits from mining activities, the villagers also openly accused their local government leaders of misappropriating the district council funds, and asked for the president’s intervention.

Called upon to respond, President Kikwete sought to assure the villagers that he would take up the matter with both district and regional authorities.

At the contentious Buzwagi gold mine project which is also owned by Barrick Gold, Mr Kikwete launched a project for the construction of 207 houses for villagers who were evicted to pave way for the project.

The president also launched a secondary school in Kahama District.

In a related development, renowned law professor Issa Shivji has said in a newly-published paper that Tanzania is beginning to witness the rise of a demand for ’resource democracy,’ in which ’’people are demanding not only that their resources be in the hands of the nationals, but also that the people should control them.’’

Shivji, now retired from the University of Dar es Salaam, notes further that ’’people are fed up with the looting of their resources - whether the looters are nationals or foreigners; white, black, pink, or blue.’’

His paper analyses the recent suspension of opposition legislator Zitto Kabwe (CHADEMA) for demanding a parliamentary probe into the controversial $800m (approx. 1trn/-) Buzwagi deal and minister Karamagi’s involvement in it.

According to Prof. Shivji, the Zitto case has ’’deeply touched the feelings and aroused the discontent of the people.’’

’’He (Kabwe) was giving public expression to private doubts and suspicions. When he was unceremoniously suspended, fuel was added to the fire. Private anguish became public anger,’’ says the retired varsity don.
 
Mkjj

Napenda kujua tafadhali.

- Mbunge wao ni nani?

- Aliongea lolote bungeni kumshukuru Zitto kwa kuleta hoja?

Ndugu zangu, Mbunge wao anaitwa James Lembeli na hakuzungumza lolote kuhusiana na suala la Zitto kutaka kuundwa Kamati Teule, si mwajua tena NIDHAMU ya Chama!!!
 
Ndugu zangu, Mbunge wao anaitwa James Lembeli na hakuzungumza lolote kuhusiana na suala la Zitto kutaka kuundwa Kamati Teule, si mwajua tena NIDHAMU ya Chama!!!

Kwa nini amshukuru wakati yeye mwenyewe alishatoa tahadhari kabla, hansard ziliwekwa hapa JF, mkaona!
 
haya tena TD wanasema $800m, Karamagi $400m,JE TD WANA MKATABA MWINGINE?
 
Najaribu kupiga hesabu za haraka haraka.. hivi

Dola Milioni 400 ni sawa na shilingi ngapi za madafu?
 
Soo la Zitto: PCB wajitosa

2007-08-24 18:34:19
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Hatimaye lile sakata aliloliibua Mhe. Zitto Kabwe bungeni kuhusiana na mkataba wa madini ya Buzwagi limechukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU kujitosa katika uchunguzi wa kile kilichotokea.

Kwa mujibu wa taarifa aliyotoa jana kupitia mahojiano ya kwenye kipindi kimoja cha luninga, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Edward Hosea amesema hivi sasa wameshaanza mchakato wa kufuatilia suala hilo ili kujua kama kuna rushwa ilitembea.

Mhe. Zitto amekuwa akimshutumu waziwazi Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Naziri Karamagi kwamba alikiuka taratibu na kutaka iundwe tume teule ya kuchunguza sababu za Waziri huyo kusaini mkataba wa madini ya Buzwagi Jijini London Uingereza katika namna ambayo aliielezea kuwa ina utata.

Baada ya suala hilo kuzua gumzo kubwa nchini hasa baada ya hoja ya Mhe. Zitto kutupiliwa mbali bungeni na kisha yeye mwenyewe kusimamishwa kwa tuhuma za kusema uongo Bungeni, TAKUKURU imeamua kutojiweka pembeni na badala yake, Bw. Hosea amesema wameanza kulifuatilia kwa kina.

Bw. Hosea ameweka wazi suala hilo wakati wa mahojiano ya kwenye kipindi cha Tuambie kilichorushwa `live` jana usiku na Televisheni ya Taifa, TVT, Redio Tanzania Dar es Salaam na Sauti ya Tanzania Zanzibar.

Mkurugenzi huyo alikuwa akijibu swali la msikilizaji mmoja aliyeuliza kwa njia ya simu kuwa taasisi hiyo inalichukuliaje suala hilo nyeti hasa baada ya kusikia tuhuma zilizotolewa na Mhe. Zitto dhidi ya Waziri Karamagi Bungeni.

Akifafanua zaidi, Bw. Hosea alisema TAKUKURU ina njia mbili kuu ambazo inaweza kuzitumia kufuatilia jambo.

Akasema njia ya kwanza ni ya mbunge mwenyewe au Mtanzania mwingine yeyote kuwasilisha malalamiko na vielelezo muhimu katika taasisi yake.

Lakini akasema njia ya pili ni TAKUKURU yenyewe kujitosa katika jambo lenye maslahi kwa taifa, hasa kutokana na ukweli kuwa nao ni sehemu ya jamii na hivyo imesikia na kufuatilia kila kitu wakati na baada ya mijadala ya Bunge.

``TAKUKURU pia ni sehemu ya Jamii, tumesikia vizuri tuhuma zote tangu kule Bungeni na maoni ya wananchi baada ya vikao vya bunge, tumeona ni wajibu wetu kulifuatilia.... napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa tunalishughulikia suala hili,``akasema Bw. Hosea.

Aidha Bw. Hosea amesema TAKUKURU inapata ubavu wa kuchunguza suala hilo kwa kutumia kifungu cha 16 cha sheria mpya ya kuzuia na kupambana na rushwa ambayo inaipa taasisi hiyo nguvu ya kufanya hivyo.

SOURCE: Alasiri

Hosea anataka kutuletea usanii tu. Tangu lini PCCB wakagusa mambo ya wakubwa??? Aendelee kubanana na police na makatibu kata. Hao ndiyo wala kodi wa TZ
 
Kutokana na jinsi Hosea alivyo onekana na kujibu swali moja kwamba Rais akisema yeye hana ubavu na ilikuwa kuhusu sakata la Mkapa na biashara zake nasema PCCB ni another BS na hakuna lolote .Wote wako kwa ajili ya kuilinda CCM na walaji wao hakuna chombo cha Kitaifa .
 
mbona hata hawahitaji kujitosa. Uchunguzi wao utaonesha hivi:

a. baadhi ya taratibu za kuingiwa mkataba huu hazikuwa wazi sana na hivyo kuacha taswira ya rushwa au ufisadi
b. Kuna baadhi ya mambo ambayo yangeweza kufanywa tofauti na hilo lingechangia kuweka uwazi na ukweli mbele ya wananchi
c. Taratibu ambazo zipo zilifuatwa na Waziri, Mwanasheria mkuu n.k wote walifuata taratibu hizo.

Hivyo basi, PCB wamefikia hitimisho kuwa rushwa haikuhusika.

My take:

Hivi ni wapi Zitto alisema kuna rushwa?
 
(Makala hii ilichapwa na RAI jana alhamisi)
Zitto hakuwatendea wananchi haki
na dkt gideon shoo
”Naomba kutoa
taarifa rasmi kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza
mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini
bila kuzingatia maagizo ya Rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya
kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe
30 Disemba, 2005.Õ Ð Zitto Zubeir Kabwe- Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Julai 16, 2007- Dodoma.
Bila ya kujiuma uma wala kujikwaa kijana huyo
alihakikisha kwamba takriban mwezi mmoja baadaye anaibuka tena katika
hadhara hiyo hiyo ya Bunge huko Dodoma na hoja yake kwapani.Kazi kubwa ambayo
ingemsibu ilikuwa ni kuthibitisha kwamba Waziri muhusika alikiuka
utaratibu na kufanya kinyume na maagizo ya mkuu wake wa kazi au tunaweza
hata kusema maagizo ya aliyempendekeza kuajiriwa na kuwa na wadhifa huo
mkubwa.Ni wazi kwamba anapotokea mwanasiasa, tena mwenye shahada ya chuo
kikuu, kuamua kuleta hoja mbele ya wenzake ambao bila shaka nao si
wazungu wa reli, bila shaka hiyo itakuwa hoja iliyokamilika.Lakini katika
hili la Zitto hoja iliyokuwa ikisubiriwa si ile ambayo ilikuja kuibuka
katika kipindi cha kuelekea mwisho wa kikao cha 9 cha Bunge la
Muungano. Kwa lugha ya mitaani ni kwamba kibao kiligeuzwa na mtuhumu akageuka
mtuhumiwa.Katika kuisukuma hoja tena nzito kama ya Zitto iliyokuwa
ikilenga kuonyesha udhaifu wa baadhi ya watendaji katika Serikali utafiti wa
kina ni muhimu sana. Lakini hata kabla ya utafiti wa kina ni muhimu
kujiridhisha kwamba hoja za msingi unazoziibua ni za msingi kweli kwa
maana ya kuongeza thamani katika kile unachokilenga. Bila shaka Zitto yote
hayo alikuwa amejiandaa nayo na naamini isingelimjia kichwani hata kwa
mbali sana kujaribu kuibua hoja ambayo haina mantiki na wala haina
ushahidi wa kutosha.Zitto alikuwa na ajenda ambayo bila shaka inafanana na
kazi mahsusi ambayo wametumwa kwenda kuifanya Dodoma. Ajenda ya kuibua
mambo ambayo yatasaidia katika kuongeza thamani katika maisha ya
Mtanzania.Kazi ya mbunge anayetambua wajibu wake ni kuingia katika uchambuzi
na uhojaji wa masuala ya msingi na bila shaka Zitto anastahili
kuingizwa katika kundi la wale ambao wanahangaika kutafuta kila chembe ya
nafasi ili kuwathibitishia waliowapigia kura kwamba si bure wakatumwa
kwenda kwenye jumba hilo lenye hadhi ya kipekee. Wana nia na uwezo wa
kuhakikisha kwamba mabadiliko ya kweli yanatokea kwa kumpatia Mtanzania
maisha bora zaidi.Mbunge anapokuwa bungeni anao wajibu kwa wapiga kura wake.
Kwa sababu kama wapiga kura wakigundua kwamba mbunge wao hawatetei
huko Dodoma, sasa ni kwa nini wamchague tena kwenye uchaguzi
unaofuata?Lakini jambo moja ni wazi katika hili la Zitto na wabunge wenzake nalo ni
lile la kutafuta mchawi. Ule usemi kwamba mchawi mkubwa wa mtu ni mtu
mwenyewe umejidhihirisha pale tulipotumbukizwa katika tamthilia ya
kuangalia jinsi hoja ilivyowasilishwa au ilivyokuwa imewasilishwa awali.
Inawezekana kabisa kwamba Zitto alikuwa na hoja na bila shaka bado kuna
hoja na wengi wanaamini kwamba ipo hoja. Katika kukubali ukweli huo ni
muhimu mambo kadhaa yakazingatiwa. La kwanza ni kwamba uzito wa hoja
hauwezi kuongezeka kwa kubandika tuhuma nyingine juu ambazo zina muonekano
wa kulenga mtu au kikundi cha watu fulani.Pili ni wazi kwamba katika
kujenga hoja yenye maslahi kwa umma ni vyema na busara zaidi kuiweka
katika mazingira ya kuilinda hoja yenyewe na tusikubali kuipaka sifa ambayo
inaweza kwa urahisi kabisa kutumika katika kuiua hoja yenyewe ya
msingi. Ikumbukwe kwamba kwa kila hoja kuna mpinga hoja na mpinga hoja
atatafuta kila udhaifu kuhakikisha kwamba anamalizana na hoja tajwa. Kwa
nini isiwe hivyo kama kuna kanuni na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya
utoaji wa hoja zenyewe? Kanuni ambazo zinapovunjwa adhabu zake huwa ni
pamoja na kumtupa mtoa hoja nje ya ulingo yaani kumsimamisha kuhudhuria
vikao kwa muda fulani?Zitto alijaribu kujenga hoja lakini alisahau kwamba
tayari alikwisha kutumia lugha ambayo kama ilivyo ada kwa kila
aliyejiandaa kupangua hoja au hata kuiteteresha lakini ikafanikiwa,
ingelitumika kwa ajili ya kuitupilia mbali hata kama ni kwa muda
mfupi.Kilichomwangusha Zitto pengine ni ujana kwa sababu kuna taarifa kwamba aliaswa
kuepukana na lugha ya tuhuma za moja kwa moja dhidi ya mbunge mwenzake
hata kama huyo mbunge ni waziri.Inawezekana kuhoji, na ni halali kabisa,
kwamba hivi msamiati unawezaje kuua hoja nzito? Unaweza! Hasa
ikizingatiwa kwamba msamiati huo haukuwa wa jumla bali ni mahsusi uliomlenga mtu
maalumu. Hapo ndipo penye shughuli pevu.Kwa upande mmoja kuna Zitto
ambaye anaamini kabisa kwamba kuna hoja nzito katika mkataba wa mgodi wa
Buzwagi. Lakini Zitto huyo huyo akatanguliza dibaji iliyomuhusu
Waziri aliyelengwa katika tuhuma hizo. Ni dibaji hiyo iliyosisitiza kwamba
Waziri kasema uongo au Waziri kaliongopea Bunge.Zitto alitaka kutumia
ushawishi kwa wabunge wenzake bila ya kujali itikadi za kichama kuonyesha
kwamba kuna utata na maslahi ya umma yapo hatarini. Hiyo ni
hoja-tuhuma na ilikuwa haijafikia tamati.Katika Bunge kuna kanuni ambazo
zimekubalika miongoni mwa wabunge. Kanuni hizo zinatoa maelekezo kuhusu jinsi
ya kuwasilisha hoja na pia lugha inayokubalika wakati wa kufanya
hivyo.Katika kuwasilisha hoja uteuzi wa msamiati ni muhimu kwa sababu jambo
linalotangulizwa mbele ni kwamba muulizaji hutaka kutanabahishwa na ndiyo
sababu swali hupitia kwa Spika na kamwe hoja haiwezi kutolewa kama
hukumu kwa mantiki hiyo basi lugha ya kuhukumu haikubaliki. Ndivyo
walivyokubaliana hao wakubwa. Lugha inayotumika katika bunge huwa ni ya
kistaarabu na inayolenga katika dhana kwamba wabunge wote ni sawa na ni
wawakilishi wa wananchi kwa namna moja au nyingine.Kwa mantiki inayotokana
na nafasi yao katika jamii haikubaliki katika bunge kutumia lugha ya
kuhukumu bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha.Ushahidi mzuri kuhusiana na
tuhuma dhidi ya Waziri ye yote ule unatosha si tu kumfukuza muhusika
kutoka katika kiti cha ubunge na kumnyangÕanya uwaziri bali pia unatakiwa
ili kuona ni namna gani muhusika anaweza kushitakiwa katika mahakama
ya kawaida kwa makosa ya kuhujumu uchumi au kudidimiza maslahi ya nchi
au kwenda na kinyume na maadiuli na miiko ya uongozi.Hakuna bunge
linaloweza kuwa na amani kama wajumbe wake wataachiwa kutumia lugha za
kuhukumu tena zinazofisha kwa kiasi kikubwa sifa za mbunge mwingine.Bunge
linaloruhusu lugha za hukumu kama vile kudai kwamba mtu ni mwongo au
fisadi n.k. hali kadhalika kuruhusiwa kwa lugha za kejeli, matusi na hukumu
zisizokuwa na mahakama lazima litaishia kudharaulika kwa sababu ngumi
na makonde ya kila aina vitakuwa ni mambo ya kawaida.Hata hivyo,
inapotokea kwamba mtoa hoja anasimama kidete na kumnyooshea mwenzake kidole
kuhusu tuhuma za tabia za kishenzi, kwamba tuhuma aliyoitoa kuhusu tabia
ya kishenzi, kwa sababu wizi, uongo n.k. ni katika kundi la tabia za
kishenzi, ndivyo hivyo na hakuna simile, basi ili tuhuma hiyo
isichukuliwe kuwa ni matusi ya rejareja ni lazima atoe ushahidi hadharani
kuyathibitisha hayo. Anapodiriki mtu kujitosa na kumtuhumu mwingine hadharani
ni lazima kuwepo na ushahidi wa kutosha kuthibitisha hayo.Ushahidi huo
ni muhimu ili aliyemwingiza muongo huyo kwenye chombo adhimu kama bunge
atambue kwamba hana mtetezi na aliyechaguliwa atambue kwamba
amegundulika udhaifu wake huo usio wa kistaarabu. Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa
na si vinginevyo.Katika hali hiyo basi Zitto alitakiwa, kabla ya
lolote lile kutoa ushahidi wa uongo wa Waziri ili kutoonekana kamba
kamtukana tu bila ya sababu yoyote. Au ili kutenda haki kwa wananchi basi
angeliondoa tuhuma zake hizo walau kwa muda ili kutoa nafasi kwa hoja ya
msingi kuweza kusikilizwa na kusonga mbele kwani kilichomvurugia mambo ni
msamiati ambao angeliweza tu kuuchomoa kama mbinu ya kivita.Pengine
katika kuisaidia demokrasia ya nchi yetu Zitto angelikuja na hoja yake ya
kuhoji uhalali wa mkataba wa Buzwagi na kuwaachia wabunge wenzake
waamue kama kweli hakuna matatizo na kama matatizo hayo yanaweza kuingizwa
katika kundi la uongo. Zitto alishiriki katika kuvuruga mjadala mzuri
ambao pengine ungelitusaidia sisi na wananchi wa Jimbo la Waziri
kujithibitishia kama anafaa au hafai.Kwa mujibu wa kanuni zilizokuwapo hadi
Bunge linamaliza muda wake wa kikao Agosti 17 ilikuwa ni kazi ya Zitto
kuthibitisha hadharani uongo wa Waziri Karamagi. Hakufanya hivyo na badala
yake akashupalia hoja yake na matokeo yake ikawa rahisi sana
kushughulika naye kwa wale ambao walilenga kutafuta njia ya kumpiga dafurau. Na
katika kupigwa dafurau Zitto aliirahisisha mno kazi hiyo kiasi kwamba
wahusika walibaki kumnyooshea kidole na kumwonyesha ni kwa kiasi gani
hajui michezo ya kisiasa.Ni wazi kwa kutosimama na kutaka kufanya mbinu
tofauti katika suala hili Zitto hakuwatendea haki Watanzania ambao
alionekana kama kutaka kuwasaidia pamoja na mambo mengine kutaka kujua jinsi
serikali yao inavyoendeshwa. Pengine jambo kubwa ambalo Zitto
ametusaidia katika kipindi hiki ni kuonyesha kwamba huwezi kupambana na CCM kwa
kupayuka tu. Ili kuweza kuiweka mahali pa kufanya kazi zake kwa
uadilifu zaidi ni lazima akina Zitto wajipange upya na kutambua kwamba siasa
za umaarufu wa reja reja zina hasara zake. Tafakuri ya kina ndio siri
ya mafanikio si ndani ya Bunge bali mahali popote pale kwenye maisha. Kwa makala zaidi, maoni na picha, tembelea; http://mjengwa.blogspot.com
 
TAKUKURU watatuingizia usiku, hawana haja ya kujitosa kwani tayari tunafahamu matokeo ya uchunguzi wao.
 
PCB wanataka kujiiingiza ili wazue vyombo vya habari viache kuendelea kuwasha moto huu, si chochote si lolote, majibu yao tuna yajua!

Wangekuwa na jipya waanze na ANBEM!
 
Naheshimu maoni ya Dk. Shoo. Nadhani naye ataheshimu maoni yangu nitakaposema kwamba hii ni takataka!
 
Back
Top Bottom