Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ziara hii ifuatiwe na UMOJA wa viongozi wote wa vyama vya Upinzani! soo lianze toka sasa wasisubiri CCM ajikusanye upya.
Simfahamu Dr. Shoo, lakini nasikitika kuona Tanzania tuna watu kama hao. Naona baada ya Rai kununuliwa, limekuwa takataka kabisa.
Ingeundwa Kamati kama alivyoomba Zitto, ingechunguza na kusema kama kuna uwongo. Wabunge wa CCM walimhukumu Zitto bila ushahidi. Hadi leo, hakuna ushahidi kwamba Zitto alidanganya. Na sisi tuko naye, tuna imani naye, tunaamini kwamba hakudanganya.
Kuna demokrasia inayoruhusu Waziri kusaini mkataba mkubwa unaoguza uchumi wa nchi bila Rais kufahamu? Hakuna. Kuna Waziri Tanzania anayeweza kusaini mkataba mkubwa bila ruhusa ya Rais? Hakuna.
Si kweli kwamba Waziri Karamagi alisaini mkataba wa Buzwagi bila kibali cha Rais. Hilo ni kuwavunga walalahoi tu. Ndugu zangu wasomi mliopo hapa, msikubali kudanganywa kwamba JK hakuruhusu. Lazima aliridhia, la sivyo Karamagi hangeendelea kuwa Waziri. Na vigogo wa CCM walifahamu kabla, kwa vingine wangeshtuka kiasi cha kuungana na Zitto kumchunguza Karamagi
Augustine Moshi
sio kama nakubaliana na mawazo ya dr shoo lakini zitto alikosea mbunge mmoja hawezi kumuita mbunge mwengine MUONGO. hata hizo nchi zenye demokrasia, wabunge hawaitani LIARS bungeni, seuzi nchi ambayo demokrasia has a long way to go.
neno muongo ni kubwa kimaadili na kimaana, zitto alipaswa kufahamu hilo kabla hajalitamka, au kutafuta ushahidi wa wazi wa uongo huo anaouongelea.
Tatizo hapa ni kwamba kwanza walisimamisha kusaini mikataba ya madini,
Was this gazetted?
hivi kuna ubaya gani mtu akiwa na mawazo tofauti na yenu?
hivi kuna ubaya gani mtu akiwa na mawazo tofauti na yenu?
SOURCE: AlasiriSoo la Zitto: PCB wajitosa
2007-08-24 18:34:19
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Hatimaye lile sakata aliloliibua Mhe. Zitto Kabwe bungeni kuhusiana na mkataba wa madini ya Buzwagi limechukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU kujitosa katika uchunguzi wa kile kilichotokea.
Kwa mujibu wa taarifa aliyotoa jana kupitia mahojiano ya kwenye kipindi kimoja cha luninga, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Edward Hosea amesema hivi sasa wameshaanza mchakato wa kufuatilia suala hilo ili kujua kama kuna rushwa ilitembea.
Mhe. Zitto amekuwa akimshutumu waziwazi Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Naziri Karamagi kwamba alikiuka taratibu na kutaka iundwe tume teule ya kuchunguza sababu za Waziri huyo kusaini mkataba wa madini ya Buzwagi Jijini London Uingereza katika namna ambayo aliielezea kuwa ina utata.
Baada ya suala hilo kuzua gumzo kubwa nchini hasa baada ya hoja ya Mhe. Zitto kutupiliwa mbali bungeni na kisha yeye mwenyewe kusimamishwa kwa tuhuma za kusema uongo Bungeni, TAKUKURU imeamua kutojiweka pembeni na badala yake, Bw. Hosea amesema wameanza kulifuatilia kwa kina.
Bw. Hosea ameweka wazi suala hilo wakati wa mahojiano ya kwenye kipindi cha Tuambie kilichorushwa `live` jana usiku na Televisheni ya Taifa, TVT, Redio Tanzania Dar es Salaam na Sauti ya Tanzania Zanzibar.
Mkurugenzi huyo alikuwa akijibu swali la msikilizaji mmoja aliyeuliza kwa njia ya simu kuwa taasisi hiyo inalichukuliaje suala hilo nyeti hasa baada ya kusikia tuhuma zilizotolewa na Mhe. Zitto dhidi ya Waziri Karamagi Bungeni.
Akifafanua zaidi, Bw. Hosea alisema TAKUKURU ina njia mbili kuu ambazo inaweza kuzitumia kufuatilia jambo.
Akasema njia ya kwanza ni ya mbunge mwenyewe au Mtanzania mwingine yeyote kuwasilisha malalamiko na vielelezo muhimu katika taasisi yake.
Lakini akasema njia ya pili ni TAKUKURU yenyewe kujitosa katika jambo lenye maslahi kwa taifa, hasa kutokana na ukweli kuwa nao ni sehemu ya jamii na hivyo imesikia na kufuatilia kila kitu wakati na baada ya mijadala ya Bunge.
``TAKUKURU pia ni sehemu ya Jamii, tumesikia vizuri tuhuma zote tangu kule Bungeni na maoni ya wananchi baada ya vikao vya bunge, tumeona ni wajibu wetu kulifuatilia.... napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa tunalishughulikia suala hili,``akasema Bw. Hosea.
Aidha Bw. Hosea amesema TAKUKURU inapata ubavu wa kuchunguza suala hilo kwa kutumia kifungu cha 16 cha sheria mpya ya kuzuia na kupambana na rushwa ambayo inaipa taasisi hiyo nguvu ya kufanya hivyo.
If not gazetted whose problem is that?
toba salaleh! ila PCB wanaweza kuchunguza hilo kweli? Hadi hivi sasa sijajua ni kwanini PCB wanaingilia kati wakati hakuna mahali hata pamoja hadharani ambapo Zitto amedai Karamagi kapokea rushwa wala nini.