The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Ziara hii ifuatiwe na UMOJA wa viongozi wote wa vyama vya Upinzani! soo lianze toka sasa wasisubiri CCM ajikusanye upya.
 
FM ES, Mkandara, Kichuguu...tusimlaumu Dr Shoo, ni njaa tuu wakuu!! Tumbo, tumbo, tumbo!!!!! Ndo hivyo tunaaibika siku baada ya siku. Utakuwa humtendei haki Shivji kumlinganisha na watu kama akina Shoo!! Inasikitisha, yaani at times ukianza kufikiria siasa zetu za Tanzania na mstakabali wa taifa letu, unapata mawazo mengine ambayo si vyema kuyaandika! Imagine the so called wasomi ndo wanatumiwa kueneza propaganda kama hizi kuwaridhisha wenye mpini akina Makamba, unategemea nini?

Its sooooo sad waungwana. Labda tutafute demokrasia mbadala inayoendana na mazingira yetu ya Tanzania. Vinginevyo, the future is bleak.
 
Ziara hii ifuatiwe na UMOJA wa viongozi wote wa vyama vya Upinzani! soo lianze toka sasa wasisubiri CCM ajikusanye upya.

Zamani sana nilipokuwa mpigana ngumi, tulikuwa tunafundishwa kuwa ukimpiga ngumi nzuri mpinzani wako akachanganyikiwa kidogo tu, basi mpakie ngumi nyingi sana mfululizo kabla hajajikusanya tena hadi aelemewe na kuharibikiwa kabisa. Ukisubiri akajikusanya atakuja na moto mkali sana na anaweza kukuumiza sana.
 
Simfahamu Dr. Shoo, lakini nasikitika kuona Tanzania tuna watu kama hao. Naona baada ya Rai kununuliwa, limekuwa takataka kabisa.

Ingeundwa Kamati kama alivyoomba Zitto, ingechunguza na kusema kama kuna uwongo. Wabunge wa CCM walimhukumu Zitto bila ushahidi. Hadi leo, hakuna ushahidi kwamba Zitto alidanganya. Na sisi tuko naye, tuna imani naye, tunaamini kwamba hakudanganya.

Kuna demokrasia inayoruhusu Waziri kusaini mkataba mkubwa unaoguza uchumi wa nchi bila Rais kufahamu? Hakuna. Kuna Waziri Tanzania anayeweza kusaini mkataba mkubwa bila ruhusa ya Rais? Hakuna.

Si kweli kwamba Waziri Karamagi alisaini mkataba wa Buzwagi bila kibali cha Rais. Hilo ni kuwavunga walalahoi tu. Ndugu zangu wasomi mliopo hapa, msikubali kudanganywa kwamba JK hakuruhusu. Lazima aliridhia, la sivyo Karamagi hangeendelea kuwa Waziri. Na vigogo wa CCM walifahamu kabla, kwa vingine wangeshtuka kiasi cha kuungana na Zitto kumchunguza Karamagi

Augustine Moshi
 
Blazameni,
Hakuna ubaya kabisa isipokuwa uwe unaitazama shilingi ile ile tunayoitazama sisi na utaje vilivyopo ambavyo hata sisi tunaweza geuza shilingi tukaviona. Huyu msomi kazungumzia shilingi lakini ndio ileee ya enzi za Ujamaa ambayo tayari haina thamani wala haikubaliki benki.
Anayosema yote yana ukweli kwa mtazamo wa Kidikteta! lile bunge la chama kimoja ambako hakuna HOJA ila ni MAOMBI na heshima kwa Mkuu!
 
Simfahamu Dr. Shoo, lakini nasikitika kuona Tanzania tuna watu kama hao. Naona baada ya Rai kununuliwa, limekuwa takataka kabisa.

Ingeundwa Kamati kama alivyoomba Zitto, ingechunguza na kusema kama kuna uwongo. Wabunge wa CCM walimhukumu Zitto bila ushahidi. Hadi leo, hakuna ushahidi kwamba Zitto alidanganya. Na sisi tuko naye, tuna imani naye, tunaamini kwamba hakudanganya.

Kuna demokrasia inayoruhusu Waziri kusaini mkataba mkubwa unaoguza uchumi wa nchi bila Rais kufahamu? Hakuna. Kuna Waziri Tanzania anayeweza kusaini mkataba mkubwa bila ruhusa ya Rais? Hakuna.

Si kweli kwamba Waziri Karamagi alisaini mkataba wa Buzwagi bila kibali cha Rais. Hilo ni kuwavunga walalahoi tu. Ndugu zangu wasomi mliopo hapa, msikubali kudanganywa kwamba JK hakuruhusu. Lazima aliridhia, la sivyo Karamagi hangeendelea kuwa Waziri. Na vigogo wa CCM walifahamu kabla, kwa vingine wangeshtuka kiasi cha kuungana na Zitto kumchunguza Karamagi

Augustine Moshi

Avoidance and Deception is the perfect sin of spin
 
Naona kuna barua hii hapa chini imo kwenye gazeti la Arusha Times la wakati huu (angalia http://www.arushatimes.co.tz/mailbag.htm). Labda PCB wangechunguza kinachoendela hapo vile vile.
=============================================
Are these two individuals authorised to sell Mchuchuma coal reserves?
Dear Editor,

I am a co-ordinator working with Rajmata Vijayarajje Scindia Trust in India.
Ours is a Registered Public Trust dealing in Education, Animal Welfare, Real Estate and Investments.

One man who introduced himself as Karume and his associate Mr Karthik Narayan had visited India 8 days back.

Their visiting cards are attached herewith. ”Mr Karume” claimed to be the son of the President of your country.

He was here to find partners for the Mchuchuma coal reserves . His intention, it seems, was to collect a good amount for himself from the Businessman here on the pretext of leasing out these coal reserves at a nominal cost.

Kindly confirm if he is the son of your President and if he is authorised to deal with these mines.
Regards

Samir Mahagaonkar
samir.mahagaonkar@gmail.com
Cell no -0011919224212276

toba salaleh! ila PCB wanaweza kuchunguza hilo kweli? Hadi hivi sasa sijajua ni kwanini PCB wanaingilia kati wakati hakuna mahali hata pamoja hadharani ambapo Zitto amedai Karamagi kapokea rushwa wala nini.
 
Hawa nao walikuwa wapi? yaani wao mpaka washituliwe ndio wanafanya kazi? wao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kufichua huu usiri usiri unaotufanya wananchi tuwe na maswali mengi.

PCCB hebu badilisheni style ya utendaji wenu muwe proactive jamani!! sio mpaka kila siku akina Zitto wawashitue
 
sio kama nakubaliana na mawazo ya dr shoo lakini zitto alikosea mbunge mmoja hawezi kumuita mbunge mwengine MUONGO. hata hizo nchi zenye demokrasia, wabunge hawaitani LIARS bungeni, seuzi nchi ambayo demokrasia has a long way to go.
neno muongo ni kubwa kimaadili na kimaana, zitto alipaswa kufahamu hilo kabla hajalitamka, au kutafuta ushahidi wa wazi wa uongo huo anaouongelea.
 
we unajuaje kwamba Karamagi si muongo? Pengine ni kweli muongo... hichi kitendawili hakiwezi teguliwa bila kamati huru kuundwa ndo maana tuna yashangaa haya mazingaombwe yakusema Zitto ni muongo kwa kumuita Karamagi muongo!
 
Yale yale ya RICHMOND kujitokeza kwenye hili na ukweli ni kuwa hii taasisis kazi yake ni kuisafisha serikali na sio kukamata wala rushwa hata kidogo. Print this article Send this article

Soo la Zitto: PCB wajitosa

2007-08-24 18:34:19
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Hatimaye lile sakata aliloliibua Mhe. Zitto Kabwe bungeni kuhusiana na mkataba wa madini ya Buzwagi limechukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU kujitosa katika uchunguzi wa kile kilichotokea.

Kwa mujibu wa taarifa aliyotoa jana kupitia mahojiano ya kwenye kipindi kimoja cha luninga, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Edward Hosea amesema hivi sasa wameshaanza mchakato wa kufuatilia suala hilo ili kujua kama kuna rushwa ilitembea.

Mhe. Zitto amekuwa akimshutumu waziwazi Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Naziri Karamagi kwamba alikiuka taratibu na kutaka iundwe tume teule ya kuchunguza sababu za Waziri huyo kusaini mkataba wa madini ya Buzwagi Jijini London Uingereza katika namna ambayo aliielezea kuwa ina utata.

Baada ya suala hilo kuzua gumzo kubwa nchini hasa baada ya hoja ya Mhe. Zitto kutupiliwa mbali bungeni na kisha yeye mwenyewe kusimamishwa kwa tuhuma za kusema uongo Bungeni, TAKUKURU imeamua kutojiweka pembeni na badala yake, Bw. Hosea amesema wameanza kulifuatilia kwa kina.

Bw. Hosea ameweka wazi suala hilo wakati wa mahojiano ya kwenye kipindi cha Tuambie kilichorushwa `live` jana usiku na Televisheni ya Taifa, TVT, Redio Tanzania Dar es Salaam na Sauti ya Tanzania Zanzibar.

Mkurugenzi huyo alikuwa akijibu swali la msikilizaji mmoja aliyeuliza kwa njia ya simu kuwa taasisi hiyo inalichukuliaje suala hilo nyeti hasa baada ya kusikia tuhuma zilizotolewa na Mhe. Zitto dhidi ya Waziri Karamagi Bungeni.

Akifafanua zaidi, Bw. Hosea alisema TAKUKURU ina njia mbili kuu ambazo inaweza kuzitumia kufuatilia jambo.

Akasema njia ya kwanza ni ya mbunge mwenyewe au Mtanzania mwingine yeyote kuwasilisha malalamiko na vielelezo muhimu katika taasisi yake.

Lakini akasema njia ya pili ni TAKUKURU yenyewe kujitosa katika jambo lenye maslahi kwa taifa, hasa kutokana na ukweli kuwa nao ni sehemu ya jamii na hivyo imesikia na kufuatilia kila kitu wakati na baada ya mijadala ya Bunge.

``TAKUKURU pia ni sehemu ya Jamii, tumesikia vizuri tuhuma zote tangu kule Bungeni na maoni ya wananchi baada ya vikao vya bunge, tumeona ni wajibu wetu kulifuatilia.... napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa tunalishughulikia suala hili,``akasema Bw. Hosea.

Aidha Bw. Hosea amesema TAKUKURU inapata ubavu wa kuchunguza suala hilo kwa kutumia kifungu cha 16 cha sheria mpya ya kuzuia na kupambana na rushwa ambayo inaipa taasisi hiyo nguvu ya kufanya hivyo.
SOURCE: Alasiri
 
toba salaleh! ila PCB wanaweza kuchunguza hilo kweli? Hadi hivi sasa sijajua ni kwanini PCB wanaingilia kati wakati hakuna mahali hata pamoja hadharani ambapo Zitto amedai Karamagi kapokea rushwa wala nini.

Mzee Mwanakijiji,

Tamshi lililotolewa na Mkuu wa Barrick (Tanzania) ambaye ni mwananchi, ni kwamba Karamagi aliwaita London wakasaini mkataba. Sasa mkataba ambao ungeweza kusainiwa Wizarani umekwenda kusainiwa HOTELINI London, na wala sio Ubalozini. Kwa nini? Lazima inaashiria mazungumzo ya rushwa. Kwa nini Karamagi ahitaji Meneja anayekaa Dar aende London wakasaini mkataba wa kiserikali hotelini? Alifanya mazungumzo gani ya faragha na huyo meneja kwanza? PCB wanatakiwa wachunguze hayo.

Kama inavyoashiria barua iliyotoka India, (ambayo ipo ukurasa unaotangualia) wakuu wengine wameanza kukazana kuuza MCHCHUMA. Tena kwa siri kama ilivyo kawaida yao!

Nchi inayoingia kwenye makucha ya walafi namna hii, huokolewa na wanafunzi na wafanyakazi. Wana nguvu sana. Tatizo ni kwamba wanafunzi wetu sasa wanajali mikopo yao, full stop. Hawana habari na nchi inakokwenda. Wafanyakazi bado ndio wanajiondoa kwenye tabia ya kuwa sehemu ya chama.

Augustine Moshi
 
Back
Top Bottom