Katika hiyo press conf.. Karamagi mara baada ya kumaliza, aliamua kuondoka bila kupokea maswali, alipokaribia mlangoni, akabanwa, akasema basi atajibu maswali ya kuhusu kesi anayotaka kufungua tu na si vinginevyo.. Akaambiwa basi arudi akae ili maswali yaje vizuri,,..
Alipokaa akasema anataka maswali matatu tu. Swali la kwanza likaulizwa na mwandishi wa Mwananchi, akauliza, "Hoja ya Zitto kuhusu mkataba wa Buzwagi ndio sababu ya Slaa kukuita FISADI, sasa tueleze kuhusu mkataba huu ambao...." akakmkatiza, kwa kusema, "mimi sikuja hapa kuzungumzia Buzwagi wala mkataba. Nimekuja hapa kama Karamagi si kama Waziri. Na Zitto pale Mwembeyanga (Temeke) sikumsikia akinikashifu, kwa hiyo yeye hayumo." Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania na Rai, yanayomilikiwa na rafki yake Karamagi, alikua jasiri zaidi nayeye aliuliza, "Kwa kuwa unataka kutekeleza utawala wa sheria, basi kwanini usijiuzulu ili haki itendeke zaidi?" yeye akajibu, "Hivi wewe ukiitwa mwizi utapelekwa gerezani? Si mkapa mahakama iamue? Sasa basi subiri mahakama itoe uamuzi." Akaja mwandishi wa Daily News, na hapo kukiwa na zogo kutoka kwa waandishi wakitaka ajibu tuhuma za Buzwagi, na mwandishi huyo akasema, "Waziri unatuchanganya.. Taarifa yako umesaini kama Waziri na hapa tupo ukumbi wa WIzara na hapo wataalamu wa wizara umekaa nao, halafu unasema ni binafsi kivipi?".... alipoinuka akawa anasindikizwa na maswali ya kumtaka kuzungumzia mkataba wa Buzwagi na ajiuzulu hadi akapitiliza mlango wa kuingia ofisini kwake huku amezongwa na waandishi na maswali luluki.. Hadi alipovutwa na msaidizi wake na kuingia ofisini...... ILIKUA NI AIBU, KESI YENYEWE HAIJAFUNGULIWA NA HATA NOTISI HAIJATOLEWA NA WANASHERIA, YEYE ANAITISHA PRESS CONF.
TAARIFA NI KWAMBA HILO NI SHINIKIZO KUTOKA JUU AJISAFISHE HARAKA KABLA YA MOTO KUWAKA. HAYA TUTAENDELEA BAADAYE