The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Kweli hii ni hoja muhimu ya kuverify claims,,, nisingependa kuamini kirahisi mpaka nipate upande wa pili, especially from economics and not from a laywer, i could listen if it was from a mathematician at least!

Mheshimiwa Kili,
Kuna mambo ambayo hayahitaji elimu ya kiwango cha shahada ili uweze kuyaelewa; elimu ni elimu tu hata kama ni shahada ya Sayansi Kimu-kitu muhimu ni knowledge tu na uwezo wa kuchambua mambo ambao hauhusiani na elimu ya chuo kikuu bali kufuatilia mambo na kujisomea.

Huo upande wa pili unaosubiri ni Wachumi na Wanasheria gani? Wa CCM na Serikali? Na kama ni CCM na Serikali unategemea wa-support madai ya Lissu?

"If something is bound to go wrong, it will go wrong" Murphy
 
hata aibu hana,kama wenzake kina Mkono na Chenge wanaosadikiwa kuwa wanasheria mahiri wameiogopa mahakama yeye anafikiri atapata kitu gani huko?fine acha aende perhaps atafungua njia for more drama to unfold...now the political situation in bongo is taking a dramatic u-turn...kumbe kuleta mabadiliko huhitaji majeshi,na kundi la mafisadi nyuma yako,all you need is a little bit of Zitto Kabwe you add up with some Dr.Slaa and mix up with strong Tundu Lissu...the result everybody will be fighting for more of that democratic soup...

And ofcourse JF.
 
na hapo i bet mawakili wake watakuwa ni Mkono & Co. Advocates,corum ya majaji sijui Mhe. yule aliyemwachia Nyari na/au Ditto ndo watakaopewa kazi hiyo.....
 
Katika hiyo press conf.. Karamagi mara baada ya kumaliza, aliamua kuondoka bila kupokea maswali, alipokaribia mlangoni, akabanwa, akasema basi atajibu maswali ya kuhusu kesi anayotaka kufungua tu na si vinginevyo.. Akaambiwa basi arudi akae ili maswali yaje vizuri,,..

Alipokaa akasema anataka maswali matatu tu. Swali la kwanza likaulizwa na mwandishi wa Mwananchi, akauliza, "Hoja ya Zitto kuhusu mkataba wa Buzwagi ndio sababu ya Slaa kukuita FISADI, sasa tueleze kuhusu mkataba huu ambao...." akakmkatiza, kwa kusema, "mimi sikuja hapa kuzungumzia Buzwagi wala mkataba. Nimekuja hapa kama Karamagi si kama Waziri. Na Zitto pale Mwembeyanga (Temeke) sikumsikia akinikashifu, kwa hiyo yeye hayumo." Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania na Rai, yanayomilikiwa na rafki yake Karamagi, alikua jasiri zaidi nayeye aliuliza, "Kwa kuwa unataka kutekeleza utawala wa sheria, basi kwanini usijiuzulu ili haki itendeke zaidi?" yeye akajibu, "Hivi wewe ukiitwa mwizi utapelekwa gerezani? Si mkapa mahakama iamue? Sasa basi subiri mahakama itoe uamuzi." Akaja mwandishi wa Daily News, na hapo kukiwa na zogo kutoka kwa waandishi wakitaka ajibu tuhuma za Buzwagi, na mwandishi huyo akasema, "Waziri unatuchanganya.. Taarifa yako umesaini kama Waziri na hapa tupo ukumbi wa WIzara na hapo wataalamu wa wizara umekaa nao, halafu unasema ni binafsi kivipi?".... alipoinuka akawa anasindikizwa na maswali ya kumtaka kuzungumzia mkataba wa Buzwagi na ajiuzulu hadi akapitiliza mlango wa kuingia ofisini kwake huku amezongwa na waandishi na maswali luluki.. Hadi alipovutwa na msaidizi wake na kuingia ofisini...... ILIKUA NI AIBU, KESI YENYEWE HAIJAFUNGULIWA NA HATA NOTISI HAIJATOLEWA NA WANASHERIA, YEYE ANAITISHA PRESS CONF.

TAARIFA NI KWAMBA HILO NI SHINIKIZO KUTOKA JUU AJISAFISHE HARAKA KABLA YA MOTO KUWAKA. HAYA TUTAENDELEA BAADAYE
 
Hii ni nzuri sana ..anataka kujitoa mhanga kwa niaba ya wenzake kujua maji ni marefu kiasi gani...wale wanaosema Slaa hana silaha watajifunza kwake
 
tumeliwa tena mchana kweupe,yaani huu ndio mkataba supa,sasa hiyo mingine sijui hikoje sipati jibu.
Ushauri wa bure kwa wtz ni kuwaondoa waha matofali hakuna faida tunayoipata kutoka kwao.na huyo karamagi sijui tufanye nini ,tumchape viboko mbele ya mkewe au sijui ni aje
 
Waungwana, this is just beyond human imagination! Hivi Tanzania tumemkosea nini Mungu jamani? Siamini kwamba kiongozi mwenye akili timamu anaweza kuingia kwenye mkataba kama huu wa Buzwagi.

Jamani, mi nadhani, itafika point tushikane mashati tuu, maana hawa jamaa hawatasikia chochote isipokuwa dhahama. Hapana his is too much, too much, way to much for poor economy like ours to afford! Hapana, na its high time, we stood up and said, ENOUGH IS ENOUGH.
 
Mahakimu na majaji wengi wa Tz ni wala rushwa na wezi tu like Kikwete na timu yake...... usishangae kusikia matokeo ya hii kesi....

Nitakuwa reserved kidogo kwenye hili....... yatakuwa yale yale ya nyari, dito, kiula, na wenzake
 
Katika hiyo press conf.. Karamagi mara baada ya kumaliza, aliamua kuondoka bila kupokea maswali, alipokaribia mlangoni, akabanwa, akasema basi atajibu maswali ya kuhusu kesi anayotaka kufungua tu na si vinginevyo.. Akaambiwa basi arudi akae ili maswali yaje vizuri,,..

Alipokaa akasema anataka maswali matatu tu. Swali la kwanza likaulizwa na mwandishi wa Mwananchi, akauliza, "Hoja ya Zitto kuhusu mkataba wa Buzwagi ndio sababu ya Slaa kukuita FISADI, sasa tueleze kuhusu mkataba huu ambao...." akakmkatiza, kwa kusema, "mimi sikuja hapa kuzungumzia Buzwagi wala mkataba. Nimekuja hapa kama Karamagi si kama Waziri. Na Zitto pale Mwembeyanga (Temeke) sikumsikia akinikashifu, kwa hiyo yeye hayumo." Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania na Rai, yanayomilikiwa na rafki yake Karamagi, alikua jasiri zaidi nayeye aliuliza, "Kwa kuwa unataka kutekeleza utawala wa sheria, basi kwanini usijiuzulu ili haki itendeke zaidi?" yeye akajibu, "Hivi wewe ukiitwa mwizi utapelekwa gerezani? Si mkapa mahakama iamue? Sasa basi subiri mahakama itoe uamuzi." Akaja mwandishi wa Daily News, na hapo kukiwa na zogo kutoka kwa waandishi wakitaka ajibu tuhuma za Buzwagi, na mwandishi huyo akasema, "Waziri unatuchanganya.. Taarifa yako umesaini kama Waziri na hapa tupo ukumbi wa WIzara na hapo wataalamu wa wizara umekaa nao, halafu unasema ni binafsi kivipi?".... alipoinuka akawa anasindikizwa na maswali ya kumtaka kuzungumzia mkataba wa Buzwagi na ajiuzulu hadi akapitiliza mlango wa kuingia ofisini kwake huku amezongwa na waandishi na maswali luluki.. Hadi alipovutwa na msaidizi wake na kuingia ofisini...... ILIKUA NI AIBU, KESI YENYEWE HAIJAFUNGULIWA NA HATA NOTISI HAIJATOLEWA NA WANASHERIA, YEYE ANAITISHA PRESS CONF.

TAARIFA NI KWAMBA HILO NI SHINIKIZO KUTOKA JUU AJISAFISHE HARAKA KABLA YA MOTO KUWAKA. HAYA TUTAENDELEA BAADAYE

Hii safi sana, sasa naona waandishi nao wameanza kuamka na kucharuka pesa za peremende zimekwisha.
 
MUNGU akulinde Tundu..

nchi yote inakuombea mema...... wabaya wako wapate ajali na wavunjike mikono na viuno!

asante kwa mchango wako
 
Tunaendeleza mapambano... wenzie walikuwa smart.. wakaja na majibu ya kisiasa kupoteza lengo.. JK alipotuhumiwa kuwa amepokea fedha za Iran (kwa connection ya RA) alitishia kwenda mahakamani... sasa hivi yuko kwa mjomba Bush.. hamna cha mahakamani wala nini...
 
Hoja nzuri, inaonekana Mh anatapatapa...huku anatumia cheo na ofisi kama waziri na huku anasema sula hilo ni lake binafsi!

naomba kuuliza kama kule hotelini London alisaini pia kama mtu binafsi au kama waziri?
 
hapa kuna kitu kinapikwa,anachotaka kufanya huyu mwizi ni kuingia mahakamani hili kutuliza joto la jiwe kisha kesi inaweza kuchukua hata miaka 20,hivyo wabunge hawatakuwa na uwezo wa kuhoji hili suala pale bungeni.hapa tumefungwa goli la kisigino subirini muone mchezo wa karata tatu
 
Majaji wa kazi kama hizi wapo, itategemea tu dhamira atakayokuwa nayo mwenye inji. Mmemsahau Mh. Hamisi Msumi wa enzi ya Mkapa?
 
Waungwana, this is just beyond human imagination! Hivi Tanzania tumemkosea nini Mungu jamani? Siamini kwamba kiongozi mwenye akili timamu anaweza kuingia kwenye mkataba kama huu wa Buzwagi.

Jamani, mi nadhani, itafika point tushikane mashati tuu, maana hawa jamaa hawatasikia chochote isipokuwa dhahama. Hapana his is too much, too much, way to much for poor economy like ours to afford! Hapana, na its high time, we stood up and said, ENOUGH IS ENOUGH.

Masanja..

Tanzania - CCM wanafanya chochote wapendacho kwa sababu wanajua wananchi hawatafanya chochote kuwauliza... wanafunzi vyuo vikuu wakiandamana wanapigwa na FFU..

wananchi pemba wakiandamana wanapigwa risasi na polisi, watu wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wanapigwa risasi, magazeti yakiandika kuhoji serikali yanafungiwa, and on ....

Watu wasipofikia point waseme NO ..... game itakuwa ile ile mpaka kiama
 
mie nadhani huu mkataba sasa upelekwe tena vijijini ili wakulima wauone,manaake mie nilikuwapo huku mwanza mwanzoni mwa mwezi huu katika kijiji kimoja nikawaeleza kuhusu mambo ya buzwagi..wananchi wakaniuliza "unataka kuchanganyikiwa"?.wanalalamika hawana barabara bora ila bado wanawasifia wasaniii,nikajua yatakuwa madhara ya Moshi wa Mwenge,na wenyewe upigwe marufuku manaake unatumika vibaya,pesa ya mwenge itumike kuhamasisha wakulima juu ya kilimo bora

...Bila Kuwaondoa Mafisadi nchi itayumba..
 
Mahakimu na majaji wengi wa Tz ni wala rushwa na wezi tu like Kikwete na timu yake...... usishangae kusikia matokeo ya hii kesi....

Nitakuwa reserved kidogo kwenye hili....... yatakuwa yale yale ya nyari, dito, kiula, na wenzake

Mwafrika wa kike hapa naweza kupingana kidogo na wewe. Tanzania wanaopokea rushwa na wanaonunulika kirahisi ni mahakimu na sio majaji. Majaji waliowengi ni watu wenye msimamo wanajua wanachofanya, but this does not mean all are good. Lakini tatizo ni kuwa majaji wakienda kinyume na inavyotaka serikali wanawekwa kando, maamuzi yao huwa hayatekelezwi. Serikali yetu huwa inatunga sheria yenyewe kupitia wabunge wa CCM ambao hao hao wengine ni mawaziri, na kuzitafsiri kupitia wabunge wa CCM kama kina Mkono na wengine, na kuzivunja kupitia mawaziri wake. Kama utakumbuka hoja ya mgombea binafsi, pamoja na kuwa mahamaka kuu iliruhusu waziri wa sheria wakati huo S. sitta aliitolea nje.
tatizo ni kuwa mahakama Tanzania isipotendewa haki haina pa kwenda kushitaki, ndio maana serikali inafanya inavyotaka. Kama tungekuwa kwenye Privy coincil labda mahakama ingeheshimiwa kidogo.
Lakini hata hivyo, still naweza kusema sijui JK ameteua majaji wangapi na kama ni majaji wa mambo ya sheria au ni majaji wa siasa. Inawezekana kuwa wameshapiga mahesabau yao na sasa wanaanza utekelezaji wa kumsilence Slaa na upinzani.
 
Kwa muda mrefu sasa kutokana na vyanzo vya kuamini Mahakama za juu zimekuwa zikisubiri sana suala la mikataba liletwe kwao. Majaji kama ilivyokuwa kwenye kesi za Kikatiba za Mtikila wamekuwa wakihoji pembeni ni kwanini "kesi ya namna hiyo haijafunguliwa" ili waweze kuimulika kwa mwanga wa sheria.
 
Back
Top Bottom