The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Naomba Mungu usiku na mchana Karamag aende mahakamani.

Ni kweli kinepi nakuunga mkono Karamagi aende mahakamani. Ila mie naomba kuwa Karamagi apate ajali ya gari kama mnafiki mudhihiri na avunje mbavu zote ili asipate raha wakati anakula hiyo 10% aliyokatiwa na Barrick (haya ni maoni yangu binafsi)
 
Si unajua ana kibri ya hela ndo anaona kila kitu kwake ni kama kumsukuma mlevi.
Hana ata punje ya aibu mahakamani ataenda ongea nini?mtembea na mihuri wa nchi nae ana mbwembwe.
Yetu macho na masikio bwana
 
Kwa habari zisizo rasmi Karamag ameombwa ajiuzulu. Bado wanaofuatilia wanavizia ki memo. Keep eyes open.
 
Mkataba ulishasainiwa na hao wawekezaji watatake advantage ukivunjwa tuu lazima watupeleke mahakama ya kimataifa then yatatusibu kama ya IPTL.
Cha msingi Bw KR ajiuzuru kwa heshima ya watz wote then huo mkataba ubatilishwe ili kuyapa nafasi maslai ya taifa.
Na hao wawekezaji waone haya basi kelele zote izo bado watakuwa wanakomaa kutuibia tuu,basi common sense kwao itakuwa sio common.
I am sure PR wao Mr Mwanyika atakuwa anawaupdate na malalamiko ya watz.
 
Hawa jamaa walimchukua Mwanyika very strategically kwani alijua siri nyingi za Tanzania wakati anafanya kazi serikalini. Na hapo ndo utaona adui wakubwa wa tanzania ni watanzania wenyewe ambao wanajali matumbo yao.

Huu mkataba kubadilishwa inabidi BARRICK waombwe kama walivyoombwa kwenye mikataba waliyosaini mapema kabisa
 
Kwa habari zisizo rasmi Karamag ameombwa ajiuzulu. Bado wanaofuatilia wanavizia ki memo. Keep eyes open.

kaombwa na nani? yeye si anasema yuko safi?

hivi kama atakubali kujiuzuru, then bunge linaweza kumwomba msamaha kabwe? (just thinking in future tens)
 
Masanja..

Tanzania - CCM wanafanya chochote wapendacho kwa sababu wanajua wananchi hawatafanya chochote kuwauliza... wanafunzi vyuo vikuu wakiandamana wanapigwa na FFU..

wananchi pemba wakiandamana wanapigwa risasi na polisi, watu wakiandamana kupinga matokeo ya uchaguzi wanapigwa risasi, magazeti yakiandika kuhoji serikali yanafungiwa, and on ....

Watu wasipofikia point waseme NO ..... game itakuwa ile ile mpaka kiama

Magazeti yanafungiwa na wenye magazeti hayo hupakiziwa kwamba sio Watanzania...A la Jenerali Ulimwengu Style.
 
maindx9.jpg


SIGNATORIES: The minister, Nazir Karamagi (right), and Pangea Minerals Ltd representative Gareth Taylor, who is also executive general manager of Barrick Gold Tanzania Limited in-charge of operations

Picture: Credit Thisday

Kweli waziri amepewa mamlaka makubwa ya kusaini mikataba n.k. Vipi uhalali wa huu mkataba ambao kwanza umefutwafutwa vipengele vyake tena kwa mikono? Je ni nani hasa hapa anahusika, Karamagi inavyoonekana hayuko peke yake katika hili. Je ni mikataba mingapi ambayo imeingiwa kwa kufutwafutwa namna hii? Hivi ni kweli rais wa nchi yuko hapo Hotelini na kuna mkataba wa millioni zaidi ya 400 na rais haambiwi kwamba kuna Sungura hapa tumenasa? Maana yake huu ni mtego mdogo wa kunasa Sungura tu kama anavyosema waziri mkuu. Kama rais wa nchi kweli alikuwa halifahamu hili kwa nini bado hajamchukulia hatua kali waziri Karamagi? Gareth Taylor naye anafahamu nani alikuwepo wakati wanaweka huo mkataba na nani aliamrisha ku-ufutafuta kama vile sisi walipa kodi hamnazo.

Sasa sisi WTZ tunasema ama zao au zetu, huu mkataba uvunjwe kama ni kweli ulisainiwa bila mashahidi na kufutwafutwa bila ridhaa ya stake holders wa Tanzania na kama hilo haliwezi kutokea basi tutafahamu ni nani hasa muhusika katika deal yote hii. Hao wawekezaji itakuwa vigumu kwao kuendelea kukomba mali TZ bila kulipa fedha halali ya ardhi kwani hii ni ya babu zetu sio babu zao. Yale yanayotokea Nigeria Delta kwa mtutu wa bunduki hatuwezi tukakubali yatokee Tanzania na rais ambaye ndiye mlinzi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano lazima sasa aamue, waswahili walisema ukiyavulia maji nguo..............................................Vinginevyo harufu hii inanukia hadi manzese uzuri.
 
Ajiuzulu kabla ya kutueleza percent ngapi alipewa na barrick?
hawa walio kwenye orodha ya Slaa, hawapaswi kujiuzulu tu, wanapaswa wawe Segerea, kifungo cha maisha..si wajiuzulu halafu wkapewe vyeo vingine kama PCCB, TIC n.k.
 
kaombwa na nani? yeye si anasema yuko safi?

hivi kama atakubali kujiuzuru, then bunge linaweza kumwomba msamaha kabwe? (just thinking in future tens)

Hata Mh. Idd Simba zama za serikali ya awamu ya tatu aligoma kuachia ngazi kwa madai kwamba alikuwa ni msafi, lakini baada ya siku chache tulimsikia Mh. Mkapa akisema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa barua ya Mh. Simba akiomba kuachia ngazi, na alikubaliana na ombi lake. Hizo ndiyo politics za Tanzania. Maana kitendo cha yeye kukubali kuachia ngazi kimya kimya bila kusema lolote anahisi kwamba kule BK kiti chake cha Ubunge kitakuwa mashakani na huenda 2010 asiweze kukitetea kwa jinsi matope na nzi walivyomsonga maana hakuna mtu anatamani kumsogelea kwa kashfa nzito alizotupiwa.

Ngoja tutege masikio labda na JK akitoka huko aliko atakuja kutuambia kwamba kwa masikitiko makubwa amepokea barua ya NK akiomba kuachia mchuma!
 
mwanakijiji,dua,mwafrika,kithuku,
..Kikwete ndiye waziri aliyeasisi sera ya uwekezaji madini Tanzania miaka ya mwisho ya 1990.

..Kikwete ndiye aliyeidhinisha kipengele cha Watanzania kupata 3% royalty.

..Watanzania tunapaswa kuwachunguza vizuri hawa watu kabla ya kuwapa uongozi.
 
Naona Donors na WB wamewashika Pabaya, huko hakuna cha siasa wala Usanii.
Usanii watatufanyia Sisi, ambao bado hatuja washika pabaya.
 
Nimefarijika sana kuona maelezo ya Mkataba wa Buzwagi ambao ulipelekea Mh. Zitto kupewa suspension ya miezi mitano ya kutoshiriki kwenye vikao vya Bunge. Ninasubiri kwa hamu jinsi wabunge wa CCM watakavyokutana kwenye kikao kijacho hapo mjini Dodoma kwa ajili ya kuendeleza kijiwe chao cha soga.

Hivi wale wabunge wote wa CCM ambao walisimama kumtetea Karamagi kwa nguvu zote na hatimaye kuunga mkono hoja ya Mh. Mudhihir M. Mudhihir ya kumsimamisha Mh. Zitto, wanajisikiaje pale wanapoona hayo madudu ya kwenye mkataba? Hapa naona kuna bao la pili ya kisigino (la mkono wa Mungu labda), maana sasa ndiyo itadhihirika wazi kwamba ni nani alisema uongo kati ya Mh. Zitto na Mh. Karamagi.

Ninamuonea huruma Mama Makinda ambaye anadai kwamba Zitto alisimamishwa kwa sababu ya kutumia lugha mbaya ambayo haikubaliki Bungeni, lakini hoja yake ilikuwa ya msingi. Swali langu kwa Mama Makinda ni rahisi sana, je, Mh. Zitto alitakiwa atumie lugha gani? Maana alichosema Mh. Zitto ni kwamba Mh. Karamagi alilidanganya Bunge au kuna neno jingine zaidi ya hilo ambalo linam-describe muongo??

Nikitazama kwa mbali ninashawishika kuamini kwamba kitumbua cha mtu fulani kiko mbioni kujaa vumbi na mchanga maana kasi ya kimbunga ni kubwa sana na kitumbua chenyewe kiko wazi kabisa (kimekuwa exposed). Kwa hali ilivyo hata akikifuta namna gani hakiwezi kulika tena labda akakioshe kwa maji na bado hata akiosha na maji utamu na ladha yote ya kitumbua itakuwa imepotea na hakitakuwa kitumbua tena bali ugali wa unga wa mchele!

Nina mashaka kwenye kuvuja huu mkataba kuna mkono wa watu, na lengo likiwa ni kuongeza pressure kwa mfanyabiashara wa sekta binafsi ambaye hapotezi muda wa kusoma mkataba bali anakubali kusaini na kufuta kwa kalam ya wino baadhi ya vipengele vya mkataba ili awahi kutimiza wajibu na asipoteze "opportunity" ya uwekezaji. Hapa naona huu mkataba umevujishwa kwa makusudi kabisa ili NK akose nguvu ya kujitetea kwenye hili na hivyo kulazimika kukubali kuachia ngazi pasipo JK kumwambia wazi kwamba aachie mchuma ili ngoma iendelee kuyeya. Hiyo ndiyo diplomatic way ya jamaa kuondoka kimya kimya bila JK kuonekana mbaya au kamtosa. It was calculated maana JK alisema tangu awali kwamba hakujua kama mkataba ulisainiwa na siyo lazima ajulishwe kila mkataba unaposainiwa, sasa hapo huo msalaba ni wa Karamagi peke yake. Muungwana kajiweka kando na kumwachia ngoma aicheze mwenyewe na ikimshinda basi abwage manyanga.

Ninasubiri kwa hamu sana kuona miniti za kikao cha Kamati ya Ushauri ya Madini, najua nazo zitakuja tu iwapo jamaa ataendelea kuwa mbishi au kung'ang'ania kubaki ofisini. Siku ya kufa nyani miti yote huwa inateleza na hakuna hata kimbilio. Kimbilio pekee lililobaki ni mahakamani ambako nako hatujui kama ataenda kweli au anatikisa kiberiti ili kuona kama kimejaa au kiko pungufu! Kila la heri huko mahakamani maana nahisi hata Jaji atakayesikiliza kesi yake na akakubaliana nae itabidi jamii imshangae kwa hukumu atayotoa!
 
Tumelogwa na mganga mwenyewe ameshakufa!

FD

Mzee nasubiri upande wa pili wa shilingi, maana hiyo comment yako naona kama inaonyesha sura ya mwalimu, ule upande wa pili sijauona!
 
Sina tatizo sana na mheshimiwa Karamagi kufungua kesi dhidi ya Dr. Slaa. Ila nina tatizo sana na kesi dhidi ya gazeti lililoripoti tangazo la Dr. Slaa na kampuni inayochapisha gazeti hilo. Makosa yao ni nini, anataka wasitoe taarifa za matukio mbali mbali kama yanavyotokea? Je kazi ya gazeti ni nini? Litafanya kazi kwa kuripoti maneno ya serikali na CCM tu lakini lisiripoti maneno ya vyama vya upinzani?
 
Back
Top Bottom