The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Kichuguu,
Wanajaribu kutisha magazeti yasiandike yale ambayo wanaona hayawaweki katika mwanga safi. Magazeti yametimiza wajibu wao, pure and simple.
 
Sina tatizo sana na mheshimiwa Karamagi kufungua kesi dhidi ya Dr. Slaa. Ila nina tatizo sana na kesi dhidi ya gazeti lililoripoti tangazo la Dr. Slaa na kampuni inayochapisha gazeti hilo. Makosa yao ni nini, anataka wasitoe taarifa za matukio mbali mbali kama yanavyotokea? Je kazi ya gazeti ni nini? Litafanya kazi kwa kuripoti maneno ya serikali na CCM tu lakini lisiripoti maneno ya vyama vya upinzani?

Mzee Kichuguu tatizo liko kwenye sheria ya magazeti nadhani ya mwaka 1976 ambayo imekuwa ikipigiwa kelele sana na wana habari wa Tanzania. Kulingana na sheria ya kigandamivu, gazeti lolote likiandika habari inayohusu kashfa na mtu aliyekashifiwa akaamua kushitaki mahakamani basi wanaounganishwa kwenye kesi kuanzia mtu aliyetoa hayo maneno, gazeti lililoandika habari hiyo, mchapishaji na ikiwezekana hata msambazaji wa magazeti (yaani wauza magazeti ambao ni vigumu kuwapata na kuwashitaki). Kwa hiyo tatizo liko kwenye hizo sheria ambazo bado zinakumbatiwa na utawala wa CCM na hivyo zinasaidia kuua demokrasia ya kweli kwa kuwa zinanyima fursa watu kupata habari kwa kuwa magazeti hayo yanaogopa kuandika baadhi ya news kwa kuogopa kushitakiwa.

Kama utakumbuka baada ya Mkutano wa Mwembe Yanga kule Tandika magazeti karibu yote hayakutaja majina nadhani labda ni MwanaHALISI pekee ndiyo liliandika majina. Pia HbariLeo lilitaja majina hayo japo halikuweka hizo tuhuma wazi wazi. Ndiyo maana ukisoma news kwenye magazeti mengi huwa wanasema jina linahifadhiwa siyo kwa sababu ya udaku bali wanaogopa kutaja ili kibano kisije kikawashukia na wanakuwa hawana uhakika na habari hiyo.
 
mimi najiuliza huu ndio mkataba uliofanyiwa mabadiliko sasa hiyo mingine si ndio tutapata pulesha na kuzimia kabisa
 
mimi najiuliza huu ndio mkataba uliofanyiwa mabadiliko sasa hiyo mingine si ndio tutapata pulesha na kuzimia kabisa

Kikwete aliposema kwamba ataanza na ku-review mikataba siku alipokuwa anafungua/zindua Bunge la Jamhuri Dec 2005, alikuwa anajua fika madudu yaliyo kwenye hiyo mikataba ya madini. May be kwa kuwa alishawahi kuwa Waziri kwenye hiyo Wizara au kwa kuwa alikuwa kwenye Cabinet ya Mkapa so alijua kila kinachoendelea kwenye sekta ya madini. Kwa hiyo nina uhakika kwa 100% kwamba mikataba ya migodi ile ya awali ni mabomu ambayo mtu akiyaona anaweza kuzimia kwa BP!!!!
 
Hii ndio nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya na Maisha bora kwa kila kiongozi wa chama

Mkataba wa Mgodi Buzwagi kumnufaisha zaidi mwekezaji
Na Mwandishi wetu
Mwananchi

SUALA la uwekezaji wa katika mgodi wa madini wa Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga linazidi kunyumbulika ambapo imebainika kwamba mkataba kati ya serikali na Kampuni ya Barrick ni wa zaidi ya miaka 50.

Kwa mujibu wa mkataba huo, uliosainiwa na Waziri wa Nishati na Madini, Nizar Karamagi na Mwakilishi wa Kampuni ya Barrick, Gareth Taylor, Februari mwaka huu London, Uingereza, kampuni ya Barrick itachimba madini katika mgodi huo kwa miaka 25 na kwamba itaongezewa tena miaka mingine 25 baada ya kipindi hicho.

"Waziri atatakiwa kutoa leseni maalum ya uchimbaji kwa kampuni haraka iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kwa kipidi kisichozidi siku 60 tangu kampuni kuwasilisha maombi ya leseni na leseni atakayotoa waziri itakuwa kwa kipindi cha mwanzo cha miaka 25,

"Kampuni itakuwa na uhuru wa kuongezewa muda wa leseni kwa masharti yale yale kwa kipindi kingine cha miaka 25 na endapo kipidi cha nyongeza kitaisha na kampuni akaomba kuongezewa tena, basi kama waziri ataona ni kwa maslahi ya taifa ataweza kutoa kipindi kingine kwa kampuni atakachoona kinafaa," sehemu ya mkataba huo ambayo Mwananchi imeiona inaeleza.

Kwa upande wa mrabaha, mkataba huo unaonyesha kwamba kampuni hiyo imeruhusiwa kuchimba madini mengi zaidi ya dhahabu.

Kifungu hicho cha mkataba kinaeleza kuwa kampuni Barrick kupitia kampuni yake tanzu ya Pagea italipa asimilia tatu ya mrabaha wa madini yote yatakayochimbwa baada ya kuondoa gharama za uzalishaji, isipokuwa katika madini ya almasi ambayo yatalipiwa asilimia tano.

Kuhusu mapato halisi ambayo yanatarajiwa kupatikana kutoka katika mgodi huo, vifungu vya mkataba huo vinaonyesha kuwa nje ya malipo ya mrabaha na kodi ya zuio, serikali ya Tanzania pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama ulipo mgodi huo, itakuwa inalipwa jumla ya dola za Marekani 583,980 kwa mwaka.

Baadhi ya kodi ambazo zitalipwa ni pamoja na asilimia tatu ya thamani ya madini baada ya kuondoa gharama za uzalishaji kama mrabaha kwa madini yote yanayochimbwa eneo la Buzwagi.

Pia mkataba huo unaonyesha kwamba kampuni hiyo itakuwa ikilipa ushuru wa stempu kama ulivyoanishwa katika Sheria ya Ushuru wa Stempu namba 20 ya mwaka 1972, kuanzia tarehe ya kuanza kwa mkataba wa Buzwagi.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa kampuni ya Pangea Minerals kutolipa hata senti tano kwa ushuru wa stempu kwani kifungu cha 5 (1) cha sheria ya ushuru wa stempu kimsema: "Hakuna ushuru wowote utakaolipwa kutokana na waraka wowote uliosainiwa kwa niaba au kwa taarifa ya serikali," ambapo kama kifungu hiki kisingekuwapo, basi serikali ingekuwa na wajibu wa kulipa ushuru huo kuhusiana na waraka huo.

Agosti 14, mwaka huu Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, lililimsimamisha Ubunge, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kujishughulisha na shughuli zozote za Bunge hadi Januari mwakani baada kubainika kuwa alisema uongo kuhusu uwekezaji katika mgodi wa Buzwagi.

Zitto aliwasilisha hoja binafsi akitaka maelezo kuhusu kusainiwa kwa mkataba huo wa mradi wa mgodi wa Buzwagi kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick, wakati serikali bado inafanya durusu ya mikataba.

Spika wa Bunge, Samwel Sitta, alisema Mbunge huyo atasimamishwa kwa vikao viwili hadi Januari mwakani kushiriki shughuli za Bunge kuanzia siku azimio la Bunge lilipopitishwa, yaani jana, zikiwamo zile za Kamati za Bunge.

Zitto alipotakiwa kujibu hoja, alisimamia msimamo wake wa kwanza na akasema yeye ni mwanademokrasia na kwamba angekuwa tayari kwa uamuzi wowote ambao Bunge lingeuchukua.

Akiwasilisha hoja hiyo, Kabwe alilitaka Bunge likubali kuunda kamati hiyo teule ili kuchunguza mwenendo mzima wa kusainiwa kwa mradi huo kulikofanyika jijini London, Uingereza Februari mwaka huu.

Alidai kuwapo kwa ukiukwaji katika baadhi ya taratibu zinazosimamia kuongoza sekta ya madini nchini ikiwemo haraka iliyomfanya Waziri Karamagi ausaini mkataba huo akiwa nje ya nchi bila kusubiri ripoti ya tathmini ya athari kwa mazingira (EIA) kuhusiana na mradi huo ambao kwa kawaida hutolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc).

Hata hivyo, baada ya Ziito kusimamishwa ubunge vyama vya upinzania vilianza ziara mikoani kuwaeleza wananchi uonevu aliofanyiwa.

Ziara hiyo imesababisha wapinzania kuibua tuhuma nyingine kubwa kwa baadhi ya viongozi wa serikali kwamba wanahusika na ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma.
 
Wakuu sijapata nafasi ya kuila hii topic yote, lakini ninasema kuwa hii ni good move, na ndio tuliyokuwa tunaiombea sasa tukae mkao wa kula maana this thing is going to very interesting and I love it!

Tukutane mahakamni, wakuu sasa ni kujiweka sawa tupate yote yatakayosemwa mahakamni, isije tena ikaanza oooh hakuna waandishi kuingia,

wakuu nitarudi baadaye!
 
Waheshimiwa Board Members,
Nafikiri muda umefika wa kuacha blah blah na kufanya vitendo.
Mambo kama haya tumeyafungia macho kwa muda mrefu sana na kuwafanya hao wafisadi kuota "Meno" na kuamini ya kuwa wako juu ya sheria na katiba ya nchi.

Kuna kitu kinaitwa "PETITION" najua wengi wetu tunajua hii ni nini, well kama hatufahamu basi ni vizuri kueleweshana.

"The right to petition is the freedom of individuals (and sometimes groups and corporations) to petition their government for a correction or repair of some form of injustice without fear of punishment for the same. Although often overlooked in favor of other more famous freedoms and sometimes taken for granted[1], many other civil liberties are enforceable against the government only by exercising this basic right,[2] making it a fundamental right in both representative democracies (to protect public participation)[1] and liberal democracies. The "right to petition," per se, is not mentioned in the Universal Declaration of Human Rights, but the related freedom of assembly and right to "take part in the government" .

Nafikiri kwa mtandao tunaweza kuelimishana na kuwaondoa hawa mafisadi....muda wao umefika.
Lets sign a Petition to remove these "Flease-blood suckas" out of the Public office.
Kama ilivyofanya kazi kwa Balozi Daraja....Natumaini itasafisha wengine.
Hawa ni watumishi wa Serikali kwa ajili ya wananchi.
So technically wananchi tuna sauti na uwezo wa kusema" Enough is Enough".
Shughuli waheshimiwa wajumbe.
 
Siku hizi za internet utamtisha nani? Si walisema mikataba siri? Wao wafanye kazi ambayo WTZ wamewatuma na wameikubali.
 
inawezekana pia hiyo ni tisha toto kwa wengine (mafisadi) kwamba
anataka kwenda mahakamani na huko ukweli waweza fumuka na wakadondoka wengi. hivyo waache kumpiga piston aka presha ya kujiuzuru.
 
Huyu karamagi kwanza ameaibisha kabila langu la wahaya kwa kuwa kwenye list ya mafisadi tena wanayofunga umma wa watanzania kwa mikataba mibovu. Hivi hataki kujifunza kuwa bunge lilimfukuza Zitto likafikiri limemaliza kumbe limezaa akina Zitto kibao pale jangwani, sasa huyu Karamagi atakipata kama ameona wanasheria wenzake wanamzidi mkono anayetetea serikali na ameamua kunyamaza kitakacho mpata atajua mwenyewe pamoja na wanamtandao wenzie wa Chama Cha Mafisadi (CCM)
 
Huyu karamagi kwanza ameaibisha kabila langu la wahaya kwa kuwa kwenye list ya mafisadi tena wanayofunga umma wa watanzania kwa mikataba mibovu. Hivi hataki kujifunza kuwa bunge lilimfukuza Zitto likafikiri limemaliza kumbe limezaa akina Zitto kibao pale jangwani, sasa huyu Karamagi atakipata kama ameona wanasheria wenzake wanamzidi mkono anayetetea serikali na ameamua kunyamaza kitakacho mpata atajua mwenyewe pamoja na wanamtandao wenzie wa Chama Cha Mafisadi (CCM)

Nimeipenda hiyo
CCM = CHAMA CHA MAFISADI
 
k2kn5.jpg


Mambo yameanza. Karamagi at the press conference.


k1av0.jpg




Pictures: Credit Michuzi Blog
Hapo ni mkutano na wanahabari tu macho yamemtoka kama mjusi aliyebanwa na lango. Huko kwa Pilato atakuwaje?
 
kweli JK na timu yake walipitia huo mkataba wakaona mambo safi? au karamagi peke yake ndiye aliye fanya hayo? na hao vibara wabunge wa chama cha mafisadi (CCM) walivyokuwa wanapiga kelele kumtete karamagi wameumbuka vibaya sana
 
Kwako ndio mkataba wa ajabu..kwa Karamagi na wahusika wengine huu ni mkataba safi na upo kwa maslahi ya Taifa.
Wabunge walipiga kula kugawana kanzu ya Zitto kwa kufuata amri kutoka juu.Hawana muda wa kuperuzi makaratasi.

Mwisho,Yule mbunge aliyekatika mkono anatakiwa akabidhiwe habari hii atupe yake machache.
Na wote waliosapoti move aliyoianzisha
 
watanzania tuamke jamani usingizi tulio lala unatosha hao mafisadi tuwawajibishe na kuwatoa ofisini. hivi akina Kingunge, Mramba, Mungai etc wanafanya nini ofisini tangu enzi za uhuru?
 
Kila Mtuhumiwa kwenye List of Shame ana anatuonyesha ujinga wake fursa ya kujifunua ikipatikana. Huyu Mtussi naye kaja na kujikanyaga kwa aibu. Unakuja na kofia ya Uwaziri kisha ukibanwa na maswali unadai kofia ya uwaziri umevaa kama show tu wewe umeenda pale kama Mtusi wa kawaida tu.

Kama kiti moto cha waandishi wa habari ni cha moto kiasi cha Karamagi kujikanyaga hivyo kiti moto cha Mahakamani atakimudu kweli? Huko si ata Differentiate Constant!

Fedha inaleta kiburi cha ajabu. Fedha inawajaza watu Roho ya Uibilisi. Fedha inathubutu hata kukuweka juu ya sheria.
Fedha inaleta mvuto wa kusikilizwa na kubadiri uongo kuwa ukweli.

Iko siku yenye jina na tarehe hawa akina Karamagi watakuwa mahakamani wamenywea kwa mashitaka ya kesi za uhujumu uchumi, sura zao zitatia huruma sana kila mmoja wetu hapa hataamini kwmaba ufahari wao wote ni umekuwa bure.

Najua Karamagi anajivunia jmambo moja tu. Kesi ataifungua Mahakamani itasomwa kisha Mahakama itaendelea kuikali mpaka siku SISIEMU wakifukuzwa kazi. Si unaona Kesi ya Dume la Mbegu Ditto hata kusomwa tu haisomwi. Ditto ni mtu huru kadri ya kanuni na taratibi za Ufisadi wa serikali ya SISIEMU.

Maneno ya MH Tundu Lissu yameniingia sana. Tatizo haliko kwa viongozi wa SISIEMU tu, tatizo lipo kwetu wananchi pia. Tumelala.
Tumelala usingizi na kuwaachia wafanye watakacho .Usingizi wetu umekuwa sumu kwenye utendaji wao ni mpaka tutakapo amka na kusema basi hapo ndipo viongozi wetu wataanza kufanya kazi na kuwajibika kwetu.

Kura ni namna moja ya kuwaondoa SISIEMU madarakani lakini si namna pekee.
Kuna mapinduzi ya kumwaga damu njia ambayo watu wengi hapa JF wanaipinga kwa sababu haitamwaga damu za mafisadi tu bali hata zetu.Pili ni njia itakayo vuruga njia zote za uchumi na maisha ya kawaida ya kila mtu na pengine kudumu kwa vizazi kadhaa.


Kama inabidi na kama suluhisho la mwisho mapambano ya silaha yatatumika kuuondoa UFISADI Tanzania.


Kuna kuandamana na mabango kuzomea viongozi na kuhujumu juhudi zao zote za kuendeleza ufisadi, ni moja katika mbinu za kuiondoa serikali madarakani.Madhara yake ni kupigwa virungu kuuawa kufungwa jela na kupewa vilema vya maisha.

Njia nyingine ya kupambana na UFISDI ni kuwafungulia mashitaka MAFISADI wote mahakamani ya zaidi ya kesi 1.FISADI mmoja anakuwa na kesi zidi ya 10.
Kuanzia Sex Scandal kwa kutumia cheo chake mpaka uhujumu uchumi.

Sisi wananchi wa kawaida
Ndiyo wapiga kura,
Ndiyo tuishio kila kona ya nchi,
Ndiyo tunaoumia kwa kila Shilingi inayoibiwa,
Ndiyo watu wa hali ya chini tusio thaminiwa,
Ndiyo Polisi tuishio kwenye nyumba duni mno,
Ndiyo FFU wapiga virungu wanyonge wenzao,
Ndiyo Mahakimu wa mahakama za mwanzo/
Ndiyo wapelelezi Usalama wa Taifa,
Ndiyo wanajeshi wa vyeo vya kawaida,
Ndiyo watumishi wa serikali ambao fedha tunaisikia tu,
Ndiyo madereva na mafundi wa magari na ndege za waheshimiwa,
Ndiyo manesi na MaDr wa kuwatibu wakipata ajali,
Ndiyo wapishi wa chakula wanachokula kifahari,
Ndiyo makuwadi kwa vimada wao na waficha siri kwa wake zao,
Ndiyo tunaofanikisha ufisadi wao kwa kuwa matarishi,
Ndiyo tujuao siri na nyendo zao zote.
Ndiyo wengi kuliko mafisadi na kwa pamoja tuna nguvu

Sisi wananchi wa kawaida ndiyo wenye uwezo wa kuundoa utarawala Haramu huu. Makundi mbali mbali niliyo yataja hapo juu yana nguvu kubwa ya ajabu ya kuliondoa TABAKA hili chafu. Tabaka la mafisadi kwa kuhonga fedha kichele na kutoa ahadi za uongo za kiuchumi za hapa na pale limefanikiwa kuteza nguvu za wananchi wa kawaida.

Tunauhahkika wa kushinda kwenye mapambano haya kwa sababu Timu ya MAFISADI mpka sasa wanalinda lango lao kwa nguvu zao zote huku sisi tukishambulia kutoka kila kona na kushangiliwa kwa nguvu zote na wananchi.
 
Rubabi,
Hiyo picha ya Madela kama vile anaimba Nkosi sikeleli!
 
Rubabi.

Hii picha niliipiga mika kaa 7 hivi ilopita nje kidogo ya jiji la Dar katika eneo moja maarufu kwa uchamji mkaa linaitwa KANZAGALE.

Inanikumbusha mengi sana we acha tu.
 
Back
Top Bottom